DCI ametoa report yake kuwa Hamza alikuwa ni gaidi mfia dini.
Hoja zinazojenga haja ya uchunguzi:
1) Magaidi wafia dini hulenga imani za watu wengine tofauti na zao. Tunajua kuwa Hamza alikuwa muislam, kwa hiyo DCI Wambura anataka kutuambia kuwa Hamza ni gaidi mfia dini ya Kiislam aliyelenga dini ya Polisi. DCI atuambie polisi wa Tanzania dini yao ni ipi, maana shambulio lake lililenga polisi tu.
2) Siyo kila muuaji ni gaidi. Polisi wamewahi kuua raia wema wafanyabiashara wa madini. Na pia wameua watanzania wengi wanapokuwa kwenye mahabusu za Polisi. Na hili, Rais Samia amelikemea hivi karibuni. Je, kwa mauaji mbalimbali yaliyokuwa yamefanywa na polisi, inatosha kuthibitisha kuwa polisi wetu ni magaidi?
3) Jeshi la polisi halina historia ya weledi katika kuchunguza matukio tata ya uhalifu, lilishindwa kufanya hivyo kwa tukio la shambulizi dhidi ya Tundu Lisu, Azory Gwanda, Ben Saanane, na wengine wengi, ujuzi huu wa kufanya uchunguzi na kutoa majibu haraka kiasi hiki wameanza kuwa nao lini?
4) Jeshi la polisi limekuwa na sifa ya kuficha na kutetea uovu unaofanywa na jeshi la polisi. Kwenye mauaji ya wafanyabiashara wa madini, taarifa yao ilisema wafanyabiashara wale walikuwa majambazi, wakati ukweli ni kuwa polisi walifanya ujambazi dhidi ya raia kwa kutumia ofisi ya polisi. Kwenye mauaji ya mwanahabati Mwangosi, polisi walisema amepondwa na kitu kizito kutoka juu, picha za video ziliwaumbua, ndipo wakakubali kuwa ni polisi waliomwua. Kwenye tukio la Akwilina, kika mmoja anajua kuwa ni polisi ndio waliomwua lakini mpaka leo wamagoma kuhusika kwao. Kuanzia lini jeshi la polisi limekuwa na credibility ya kuweza kufanya uchunguzi unaosimama katika weledi?
5) Tabia mbaya ya uovu wa polisi katika kubambikia watu kesi imekuwa ndiyo sifa kuu ya jeshi la polisi. Na hili limethibitishwa hata na Rais wa JMT.
6) Ripoti zote kuhusiana na rushwa, polisi ndiyo taasisi ambayo kila mwaka inaongoza kwa ulaji rushwa. Mla rushwa, ana uwezo wa kujichunguza na kutoa ripoti inayoweza kuaminika?
Kamati/Tume ya uchunguzi iangalie mambo yafuatayo:
1) Uwezo wa jeshi la polisi katika kufanya uchunguzi
2) Maadili ya jeshi la polisi katika kusimama katika ukweli
3) Kwa kutegemea majibu ya hoja ya 1 na 2, itoe tamko kama taarifa ya uchunguzi aliyoitoa DCI inatakiwa kuaminika au kupuuzwa. Kama inastahili kupuuzwa, ipendekeze kuundwa kwa chombo kingine kuchunguza tukio la Hamza, na pia kuchunguza uwezo wa polisi kiweledi na kimaadili.