Rais Samia, unda tume huru kuchunguza mauaji ya Hamza

Wewe rejesha milion 400 na madini ya marehemu Hamza kwanza kubla haujaendelea kumbambikia marehemu tuhuma feki za ugaidi wakati yeye aliwaua Asikari wawili huku wengine wakiuana wenyewe kwa wenyewe kwa kutupa risasi hovyo
 
Pesa milion 400 na madini ya marehemu Hamza vipo wapi? ni gaidi gani anashambulia Polisiccm pekee na kuwaacha raia wapita njia
 
Kwa nini isiundwe tume ya kuchunguza mauaji ya polisi?
 
DCI ametoa report yake kuwa Hamza alikuwa ni gaidi mfia dini.

Hoja zinazojenga haja ya uchunguzi:

1) Magaidi wafia dini hulenga imani za watu wengine tofauti na zao. Tunajua kuwa Hamza alikuwa muislam, kwa hiyo DCI Wambura anataka kutuambia kuwa Hamza ni gaidi mfia dini ya Kiislam aliyelenga dini ya Polisi. DCI atuambie polisi wa Tanzania dini yao ni ipi, maana shambulio lake lililenga polisi tu.

2) Siyo kila muuaji ni gaidi. Polisi wamewahi kuua raia wema wafanyabiashara wa madini. Na pia wameua watanzania wengi wanapokuwa kwenye mahabusu za Polisi. Na hili, Rais Samia amelikemea hivi karibuni. Je, kwa mauaji mbalimbali yaliyokuwa yamefanywa na polisi, inatosha kuthibitisha kuwa polisi wetu ni magaidi?

3) Jeshi la polisi halina historia ya weledi katika kuchunguza matukio tata ya uhalifu, lilishindwa kufanya hivyo kwa tukio la shambulizi dhidi ya Tundu Lisu, Azory Gwanda, Ben Saanane, na wengine wengi, ujuzi huu wa kufanya uchunguzi na kutoa majibu haraka kiasi hiki wameanza kuwa nao lini?

4) Jeshi la polisi limekuwa na sifa ya kuficha na kutetea uovu unaofanywa na jeshi la polisi. Kwenye mauaji ya wafanyabiashara wa madini, taarifa yao ilisema wafanyabiashara wale walikuwa majambazi, wakati ukweli ni kuwa polisi walifanya ujambazi dhidi ya raia kwa kutumia ofisi ya polisi. Kwenye mauaji ya mwanahabati Mwangosi, polisi walisema amepondwa na kitu kizito kutoka juu, picha za video ziliwaumbua, ndipo wakakubali kuwa ni polisi waliomwua. Kwenye tukio la Akwilina, kika mmoja anajua kuwa ni polisi ndio waliomwua lakini mpaka leo wamagoma kuhusika kwao. Kuanzia lini jeshi la polisi limekuwa na credibility ya kuweza kufanya uchunguzi unaosimama katika weledi?

5) Tabia mbaya ya uovu wa polisi katika kubambikia watu kesi imekuwa ndiyo sifa kuu ya jeshi la polisi. Na hili limethibitishwa hata na Rais wa JMT.

6) Ripoti zote kuhusiana na rushwa, polisi ndiyo taasisi ambayo kila mwaka inaongoza kwa ulaji rushwa. Mla rushwa, ana uwezo wa kujichunguza na kutoa ripoti inayoweza kuaminika?

Kamati/Tume ya uchunguzi iangalie mambo yafuatayo:

1) Uwezo wa jeshi la polisi katika kufanya uchunguzi

2) Maadili ya jeshi la polisi katika kusimama katika ukweli

3) Kwa kutegemea majibu ya hoja ya 1 na 2, itoe tamko kama taarifa ya uchunguzi aliyoitoa DCI inatakiwa kuaminika au kupuuzwa. Kama inastahili kupuuzwa, ipendekeze kuundwa kwa chombo kingine kuchunguza tukio la Hamza, na pia kuchunguza uwezo wa polisi kiweledi na kimaadili.
 
Magaidi huwa wakarimu sana kwenye hatua za mwanzo km likivyokuwa gaidi Hamzo.

Wakishakomaa kwenye ugaidi huua kila mtu
 
Yaani Police wanajichunguza then tutegemee majibu tofauti na hayo
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Magaidi huwa wakarimu sana kwenye hatua za mwanzo km likivyokuwa gaidi Hamzo.

Wakishakomaa kwenye ugaidi huua kila mtu
Ni ukarimu gani huwa wanaufanya kwenye hatua za mwanzo? Unaweza kutoa mifano?
 
Nawe ni gaidi
1.https://www.jamiiforums.com/threads/rais-samia-unda-tume-huru-kuchunguza-mauaji-ya-hamza.1908681/unread
2. Uchunguzi wa Polisi kuhusu Hamza Mohammed uchunguzwe
3.
Wewe pia gaidi
1. Rais Samia, unda tume huru kuchunguza mauaji ya Hamza
 
Nimeshangaa pale aliposema kuwa marehemu wala hakuwa na uwezo wa kumiliki madini kwa wakati huu maana uwo mgodi unaosemwa ulishaacha kufanya kazi muda sana.pia akasema marehemu hakuwa na uwezo wowote ule wa kifedha kama inavyosemwa.

Lakini cha kushangaza wafanyakazi wa marehemu tuliwasikia wakiwa wanaojiwa na walisema walikuwa wanaendelea na kazi mpaka walipopata taarifa kutoka kwa kaka wa marehemu kuwa jamaa amefariki.

Ukisikiliza hii report kiukweli inatupa wasiwasi juu ya uwezo wa jeshi letu na pia kuna uwezekano wa jeshi letu la polisi likawa linaongozwa na majambazi.ukiangalia hata ndugu walioshikiliwa wengi awakuwa na ukaribu na marehemu kwa muda mrefu ila wamekuwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.kwa ushauri wangu ningependekeza iundwe kamati kutoka jwtz ili kuchunguzwa mwenendo wa jeshi letu la polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe rejesha milion 400 na madini ya marehemu Hamza kwanza kubla haujaendelea kumbambikia marehemu tuhuma feki za ugaidi wakati yeye aliwaua Asikari wawili huku wengine wakiuana wenyewe kwa wenyewe kwa kutupa risasi hovyo
mkiitwa mkatoe maelezo ili uchunguzi ukamilike,mbio mile 500 kwa sekunde.

redio mbao betry mihogo.
 
Pesa milion 400 na madini ya marehemu Hamza vipo wapi? ni gaidi gani anashambulia Polisiccm pekee na kuwaacha raia wapita njia
polisi wako sallenda wengi sana.huku,ubarozi wa ufaransa alikiwa anamtafuta mtu wa kumbebea maji ya kunywa au???
 
Kwa nini isiundwe tume ya kuchunguza mauaji ya polisi?
Ndivyo ilivyokusudiwa, yaani iundwe tume ya kuchunguza mauaji yaliyofanywa na Hamza Hamza. Tunataka kujua sababu za Hamza kuchukua hatua ile. Sidhani kama watu wanaunga mkono mauaji ya Polisi, kwa sababu yoyote ile. Tunataka kuuua sababu. Kama Hamza alifanya mauaji ya kulipiza kisasi, polisi walimfanyia nini? Lengo ni kutusaidia kama Taifa kujua chanzo, na hiyo itatusaidia kuzuia mauaji ya namna hii au mabaya zaidi siku za mbeleni.
 
Hahaaaaha kesi ya wizi wa mahindi ya Ngedere kupelekewa nyani waichunguze hakika wakati ushahidi ukienda kuchunguzwa shamba litabaki babua matupu!
😁😁😁
 
Hivi kwani haiwezekani jeshi la polisi likavunjwa??. Yaani wakuu namaanisha hivi kusiwepo na jeshi la polisi Tanzania hii si inawezekana tu tukaishi bila Hilo jeshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…