Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kunaweza kuwa na miongozo ya kuchangia kampeni. Ratiba, viwango, uwazi zaidi kwenye matumizi, kutenganisha pesa za kampeni na pesa za mambo mengine.Then what will be happening?
Angalau kunaweza kuwa na point ya kuanzia kushitaki kama kuna uhuni unafanyika.
Hata ikiwa mfumo ni mbaya na watu hawafuati sheria, kuna tofauti kati ya sehemu ambayo kuna sheria na watu hawazifuati, na sehemu ambayo hakuna hata sheria.
Pale ambapo kuna sheria na watu hawazifuati unaweza juanza kulalamika kwamba watu hawafuati sheria, ukaweka utaratibu wa kulazimisha sheria zifuatwe.
Pale ambapo huna hata sheria huwezi kulazimisha watu wafuate sheria, kwa sababu hakuna sheria.