Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 21,788
- 34,782
Mama Samia Mimi ni mfuasi wako ambae sitakua tayari kuona Kuna watu kwa makusudi wanapima kina Cha maji. Mama Samia hawa watu wanaku-beep kila Mara ili kuona Kama upo strong au weak, waonyeshe wewe ni nani.
Waambie wewe ni amiri jeshi mkuu na Mtu makini sana, Wala usiwaonee aibu kwa kuwa unawajua tayari. Na kawaida yao wataanza kukuchafua kwa kila aina ya maneno Ila usijali ndio kazi ya kiongozi hiyo. Kiongozi huwezi kumridhisha kila mtu, Hawa watu wanauchezea mfumo wa GePG kwa makusudi kabisa.
TRA na Sasa TANESCO lugha yao imebadilika na kuwa "system ipo down" , watu wameshindwa kununua umeme majibu ya TANESCO eti wavumilie. System kama ya TANESCO inaharibikaje kirahisi hivi? Hapo inatafutwa namna ili kurudi mfumo wa zamani Kama ilivyotokea kwa TPA eti mfumo wa electronic clearing system upo chini hivyo kutumika wa zamani.
Ni wazi hii ni hujuma na makusudi kwa kuwa haiwezekani mifumo ya taasisi nyeti Kama TRA, TPA na TANESCO yote iwe hivi kwa kipindi Cha mwezi mmoja tu. Mama Samia shusha rungu na wasikuzoee kabisa maana hawahawa wanaokukwamisha ndio watakuwa wa kwanza kusema "umeshindwa kuongoza huwezi uraisi".
Wote mnaoanza kum-beep mama Samia siku zenu zinahesabika, Tanzania sio shamba la Bibi.