Rais Samia usimuonee mtu aibu, mifumo ya Serikali inachezewa kwa makusudi

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
21,788
Reaction score
34,782
​

Mama Samia Mimi ni mfuasi wako ambae sitakua tayari kuona Kuna watu kwa makusudi wanapima kina Cha maji. Mama Samia hawa watu wanaku-beep kila Mara ili kuona Kama upo strong au weak, waonyeshe wewe ni nani.

Waambie wewe ni amiri jeshi mkuu na Mtu makini sana, Wala usiwaonee aibu kwa kuwa unawajua tayari. Na kawaida yao wataanza kukuchafua kwa kila aina ya maneno Ila usijali ndio kazi ya kiongozi hiyo. Kiongozi huwezi kumridhisha kila mtu, Hawa watu wanauchezea mfumo wa GePG kwa makusudi kabisa.

TRA na Sasa TANESCO lugha yao imebadilika na kuwa "system ipo down" , watu wameshindwa kununua umeme majibu ya TANESCO eti wavumilie. System kama ya TANESCO inaharibikaje kirahisi hivi? Hapo inatafutwa namna ili kurudi mfumo wa zamani Kama ilivyotokea kwa TPA eti mfumo wa electronic clearing system upo chini hivyo kutumika wa zamani.

Ni wazi hii ni hujuma na makusudi kwa kuwa haiwezekani mifumo ya taasisi nyeti Kama TRA, TPA na TANESCO yote iwe hivi kwa kipindi Cha mwezi mmoja tu. Mama Samia shusha rungu na wasikuzoee kabisa maana hawahawa wanaokukwamisha ndio watakuwa wa kwanza kusema "umeshindwa kuongoza huwezi uraisi".

Wote mnaoanza kum-beep mama Samia siku zenu zinahesabika, Tanzania sio shamba la Bibi.
 
Hii mifumo ya kielectronic ufaa Sana kwa wenzetu wenye package kama motisha na sio kwenye hizi nchi zenye mshahara wa mwezi ni SAwa na posho ya mbunge ya siku system zinataka uaminifu maana ni rahisi sana kuchezewa
 
Mbona maelezo ya TANESCO yanaeleweka, au mwenzetu ni ile kndi la Sukuma gang ambalo kila tatizo mnaona kuwa limetokea kwa kuwa Jiwe limeanguka? Kutokea kwa hitilafu kwenye mfumo wa mawasiliano ni jambo la kawaida na ndio maana TANESCO wameeleza kuwa wataalam wanashughulikia tatizo
 
Kwa hivyo ww unabisha au ww ndio jizi lenyewe
 
Hii mifumo ya kielectronic ufaa Sana kwa wenzetu wenye package kama motisha na sio kwenye hizi nchi zenye mshahara wa mwezi ni SAwa na posho ya mbunge ya siku system zinataka uaminifu maana ni rahisi sana kuchezewa
Tatizo magufuli alilazimisha kampuni/mashirika yote za serikali kuwatumia TTCL kwenye maswala ya mawasiliano wakati TTCL wenyewe hawajiwezi. Tatizo halijaanza leo kwenye mawasiliano ila kwa kuwa haikuruhusiwa kutoa taarifa enzi zake wengi mtaona ni jambo jipya kwa kuwa tu limewagusa wengi (watumiaji hata wa hali ya chini) Watu wanaolipa kodi TRA wameshazoe hali hii mbona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…