Rais Samia usipoangalia mambo mengi ktk Serikali yako kwa jicho la tatu njia itakuwa na miiba mingi sana...

Rais Samia usipoangalia mambo mengi ktk Serikali yako kwa jicho la tatu njia itakuwa na miiba mingi sana...

Mwerevu hakatai ushauri....

Kuna jambo umegusia "kurusha vijembe kwa awamu ya 5"....

Mh.SSH ni mwanasiasa....na Siasa ina mawanda yake......

Yeye ni zao la awamu ya 5....kama ilivyo wa awamu ya 5 kutoka zao la awamu ya 4....ikiwa wa awamu ya 5 alirusha vijembe kwa baadhi ya awamu ya 4 unataka iwe ajabu kwa mh.SSH kuyafanya hayo?!!!

Kwanini tunakuwa "obsessed" na kurushiwa vijembe kwa awamu ya
5?!!!

Hofu yako ni nini ?!!!!

Hofu yako iko wapi ?!!!

Hivi mh.SSH akiirushia vijembe awamu ya 5....vijembe hivyo havimfikii yeye binafsi kama vilipokuwa vinamfikia hayati Magufuli alipokuwa anairushia vijembe awamu ya 4....

Kwa MUKTADHA huo ,basi hii hofu yako inakuwa si hoja "constructive" bali umepwagaza hisia zako tu"personal psychological conflicts"[emoji1787][emoji1787]

#SiempreJMT[emoji120]
Hili la awamu kurushiana vijembe halijaanza leo; kadri umbilikimo unavyoongezeka katika uongozi wa nchi yetu ndivyo vijembe na mipasho inavyokuwa mtaji wa kujijenga binafsi kisiasa badala ya kujenga nchi! Awamu ya tatu ulishawahi kusikia vijembe dhidi ya awamu ya 2 au 1? Hata mara moja haikutokea. Awamu ya 3 ulishapata kusikia kiongozi akisifia uongozi wake na maendeleo aliyoleta kiongozi mkuu? Hata mara moja hakuna. Badala yake, ilipobidi serikali ndiyo ilisifiwa na siyo kiongozi. Ugonjwa huu wa kujisifu na kupiga wengine vijimbe ulianza kwa mbali awamu ya 4 pale uongozi ulipoanza kuonyesha dalili za kutamani kuipiku awamu iliyotangulia kwa kutoa kipaumbele kwa miradi mipya kabla ya kukamilisha iliyokuwepo. Kwa vile nchi yetu imekuwa ikiongozwa na chama kimoja cha siasa muda huu wote, tunaweza kusema kiini cha matatizo ni hicho chama cha siasa; kimepoteza uwezo wa kusimamia serikali. Sababu ya kupoteza uwezo wa kusimamia serikali ni uwezo mdogo wa kiuongozi wa hao wanaopata uongozi. Kwa bahati mbaya kiongozi mkuu asipokuwa na uwezo wa kutosha mambo mengine mengi huharibika kwani kiongozi mkuu wa chama ndiye huyo huyo mkuu wa serikali. Vyama vya siasa vijitafakari; vione haja ya kugawa madaraka badala ya kumrundikia mtu mmoja. Demokrasia ianzie kwenye vyama. Vinginevyo, atatokea mtu mmoja wa ajabu atajimilikisha kila kitu: chama, serikali, nchi na hata uhai wa raia mmoja mmoja!
 
Tanzania watu ni wavumilivu ila ni uvumilivu unaotokana na makuzi mabaya yaliyojengea watu woga usiokua na maana.

Kiongozi anakosea watu wanamwangalia tu.

Hawamuwajibishi.
Muasisi wa taifa hili alikuwa mtu mwema, mtawala-mwanafalsafa, mzalendo na mtu mwenye upeo mkubwa. Nia yake njema, mapenzi makubwa kwa raia na utu wake vilifanya watu kuwa wa nchi hii kupendana, kuwa wavumilivu na kuuamini sana uongozi kuwa siku zote unao nia njema na uwezo wa kujisahihisha wenyewe bila kupigiwa kelele pale unapokosea. Kama nchi, ilituchukuwa muda mrefu kuona kuwa siyo kweli kuwa uongozi kila wakati unakuwa na nia njema, maono mazuri na uwezo wa kusahihisha makosa yake. Siyo jambo rahisi kwa raia mmoja mmoja kuwajibisha uongozi uliopo madarakani. Kwa kawaida ukosoaji na uwajibishwaji wa raia dhidi ya watawala hufanyika kupitia raia waliojiunga pamoja na kuanzisha vikundi vyao vya kiitikadi, yaani vyama vya siasa. Hapa kwetu kwa msaada mkubwa wa huyo huyo muasisi wa taifa hili, na kama sehemu ya utamaduni wa kujisahihisha alioasisi, tuliamua kama nchi kuurejesha mfumo wa vyama vingi ili raia wautumie kukosoa na kuwawajibisha walioko madarakani. Mwanzoni, walioko madarakani walivipuuza kabisa hivyo vyama na kuendelea na mambo yao kama vile havipo. Lakini pamoja na kupuuzwa vyama shindani viliendelea kufanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kuibua kashfa za serikali na hivyo kujiongezea umaarufu na wafuasi. Walioko madarakani wakabaini kuwa haitoshi tu kuwapuuza washindani; wakabuni mikakati ya kuhujumu wasipate nguvu. Hujuma hizo ni nyingi mno. Lakini pamoja na hujuma hizo bado raia wameendelea kuhitaji vyama shindani na kuviwezesha kukua ingawa kwa kasi ndogo. Hatimaye ikafika mahali walioko madarakani wakaona hujuma peke yake nayo haitoshi; wakaamua kuviua kabisa vyama shindani kwa kutangaza vita hadharani, kutumia nguvu zote za dola waziwazi na hatimaye kupora uchaguzi kwa mtutu wa bunduki! Hivyo tukitaka kweli raia wa nchi hii wachukue nafasi yao ya kuamua namna wanavyotaka kuongozwa, nani awaongoze na kuwasimamia walioko madrakani basi tuhakikishe tunalinda mfumo wa vyama vingi vya siasa. Binfsi naamini baada ya kugundua makosa yetu huko nyuma, Baba wa Taifa hili aliona salama yetu pekee ni vyama vingi vya siasa na kusimamia maono yake hayo kuona kuwa katika uhai wake mfumo huo unarejeshwa, kinyume kabisa na matakwa ya chama alichokiasisi mwenyewe.
 
Mwerevu hakatai ushauri....

Kuna jambo umegusia "kurusha vijembe kwa awamu ya 5"....

Mh.SSH ni mwanasiasa....na Siasa ina mawanda yake......

Yeye ni zao la awamu ya 5....kama ilivyo wa awamu ya 5 kutoka zao la awamu ya 4....ikiwa wa awamu ya 5 alirusha vijembe kwa baadhi ya awamu ya 4 unataka iwe ajabu kwa mh.SSH kuyafanya hayo?!!!

Kwanini tunakuwa "obsessed" na kurushiwa vijembe kwa awamu ya
5?!!!

Hofu yako ni nini ?!!!!

Hofu yako iko wapi ?!!!

Hivi mh.SSH akiirushia vijembe awamu ya 5....vijembe hivyo havimfikii yeye binafsi kama vilipokuwa vinamfikia hayati Magufuli alipokuwa anairushia vijembe awamu ya 4....

Kwa MUKTADHA huo ,basi hii hofu yako inakuwa si hoja "constructive" bali umepwagaza hisia zako tu"personal psychological conflicts"[emoji1787][emoji1787]

#SiempreJMT[emoji120]
Nashukuru ila sidhani kama umenielewa. Asante
 
Acha Acha Acha Acha......
Acha kumtisha Rais na mambo ya kishetani na kipumbavu.
Rais ana watu wa kila aina wa kumsaidia, hahitaji mtu kama wewe mpiga ramli.
Waambie na waliokutuma, mmeshindwa.
Mimi namuombea Rais SAMIA awe na afya njema, nampenda sana.
 
Rais Samia Shikamoo.
na karama ambayo nimezaliwa nayo yakuona kesho au miaka mia inayokuja samahani lakini sijisifu nikipaji nimeona Mungu kanipa kwa faida ya Taifa. Nikipaji ambacho duniani kwa sasa ndio Habari ya mjini uwezo wakuiona kesho nakufanya maamuzi leo au maandalizi leo kabla ya kesho au siku yatukio.

Mh Rais naomba niishie hapa kwa leo nitaendelea ikimpendeza Mungu. Asante
Naunga mkono hoja, nakukubali sana.
P
 
Acha Acha Acha Acha......
Acha kumtisha Rais na mambo ya kishetani na kipumbavu.
Rais ana watu wa kila aina wa kumsaidia, hahitaji mtu kama wewe mpiga ramli.
Waambie na waliokutuma, mmeshindwa.
Mimi namuombea Rais SAMIA awe na afya njema, nampenda sana.
Kuna mahali nimemtisha Rais? If yes moderato aufute Uzi ila sijaona mahali nimemtisha Rais soma vizuri
 
Rais kama yupo mwanasiasa, marafiki au mtu mwenye nguvu ktk siasa zako anakushauri eti kurusha mawe na vijembe na dhihaka kwa awamu ya Tano ndio njia yakupanda kisiasa Mh Rais nakuomba uyatafakari hayo mara Saba sabini sioni picha nzuri kwa wimbi hili na kama nakosea basi pia naomba radhi
Nimeishia hapa siendelei kusoma. Nilifikiriunatoa ushauri mujarabu kumbe wewe ni Sukuma Gang aka Ndumilakuwili? Hamna kitu hapo...una njaa...ukishiba akili zitakurudia.
 
Mh Rais Samia Shikamoo.

Hongera kwa kazi ya ujenzi wa Taifa la Tanzania. Pia Hongera kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke sisi kama watanzania tunajivunia kwa kuwa hii inadhihirisha Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na katiba yetu vipo imara.

Rais sijasomea kutoa ushauri kwa viongozi wakuu wakitaifa wala Sina elimu ya siasa ukiacha elimu nyingine za Dunia na mambo ya uchumi pia na karama ambayo nimezaliwa nayo yakuona kesho au miaka mingi inayokuja samahani lakini sijisifu nikipaji nimeona Mungu kanipa kwa faida ya Taifa langu. Nikipaji ambacho duniani kwa sasa ndio Habari ya mjini uwezo wakuiona kesho nakufanya maamuzi leo au maandalizi leo kabla ya kesho au siku yatukio.

Viongozi huwa na maono pia viongozi huwa na ndoto. Yes huwezi kuwa kiongozi usiwe na ndoto au vision hivyo kwa makala hii leo nakushauri usiidharau ndoto unayo iyota. Narudia tena samahani Mh Rais nakushauri usiidharau ndoto unaiyota na usiyadharau maono unayo yaona hasa wakati wa mchana au kwenye halaiki au kwenye mikutano ya Siri ya kitaifa au usiku wa manane.. Unaweza sema anasema Nini huyu mtoto? Mh Rais nakupa mfano unaweza ukawa imeingia kwenye mkutano nyeti wa kitaifa na mara ghafla ukaona Giza wakati ni mchana na taa zina Waka kama ni usiku Umeme haujakatika.

Rais Giza Hilo lina maana kubwa sana usisema labda uchovu au usingizi nop hapo Kuna shida. Badala yakuendelea na kikao ingia chumba cha Siri muombe Mwenyezi Mungu na utashangaa majibu utayapata. Mfano mwingine unaweza ukawa umeletewa file na kila kitu unaona kipo poa ila shika pen 🖊️ u sign mkono mzito Mh Rais usi sign nakuomba usi Sign hapo Mungu anakushitua kitu na ukitaka prove muite mtu wako wa siri mpe kurudia ile kazi kwa siri na utashangaa majibu utakutana nayo. Usishangae huwo ndio uwezo wa Mungu kwa viongozi.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiti umekikalia sio kiti cha kawaida. Nikiti kizuri chenye utukufu wahapa duniani ila sio ahera. Nikiti kinawala walio kikalia na kuwakausha wanao kigusa kwasababu kina Mamlaka na mwenye Mamlaka nialie kikalia sio anaye kibeba. Unapo ingia Ikulu jiulize wangapi wamekikalia na kwanini wewe umekikalia ili Mungu wako akuonyeshe Yale sisi atuwezi kuyaona ila Wewe tu ulie kikalia. Mh Rais Taifa hili ni kubwa na maoni yangu kutoka sasa embu jaribu kushirikisha jicho la Tatu kwasababu Mimi kwa Imani yangu Nina amini haupo hapo kwa bahati mbaya ila kwa kisudi la Mungu kwa watanzania.

Rais haitowezekana wewe kuwa na Rafiki wa kweli ila wengi nikujikomba na kukulamba miguu wapate mkate wao wasiku wanaweza hata kuvua nguo nakujigarakaza Samia hakuna kama wewe na hata kufikia kusema hata Mungu anajuwa hakuna kama wewe hawa hawa ukiwaona ingia vyumba vya Siri wakabidhi kwa Mungu na umuombe ukuthibitishie semi zao nataka kuhakikisha utakachokiona utaogopa na hukutegemea maana matendo yao na wanachokifanya gizani hata mchawi hawamfiki. Jicho la tatu. Jicho la tatu.

Rais kama yupo mwanasiasa, marafiki au mtu mwenye nguvu ktk siasa zako anakushauri eti kurusha mawe na vijembe na dhihaka kwa awamu ya Tano ndio njia yakupanda kisiasa Mh Rais nakuomba uyatafakari hayo mara Saba sabini sioni picha nzuri kwa wimbi hili na kama nakosea basi pia naomba radhi Mh unaweza kuachia hiyo hali ila kwa maono yangu vile Mungu ananionyesha usipo dhibiti huu upepo mwisho hautokuwa mzuri kama Taifa na hata mpaka sasa naona mpasuko mkubwa unataka kulikumba Taifa kwa kujadili mambo ya awamu ya Tano. Lakini Siri zote mnazo na ukweli wote mnao je mtatengeneza uwasi ndani ya serikali ile ile unaiongoza? Nakama ndivyo Nini kitatokea? Jibu lipo kwenye kuangalia mambo ktk jicho la tatu.

Mh Rais ufa WA Muungano NAUWONA uleeee NAUWONA ulee pale nakusii shirikisha jicho la tatu. Wakati German na Russian wanagonga mvinyo nakufurahia Nodsrim 2 Marekani KUPITIA shirika lake la ujasusi alimuonya German na Ulaya yakuwa Hilo Bomba linaenda kuanzisha vita na hicho ndicho kimetokea. Mh Rais sio kila project ni ya maendeleo ila zipo project usipo shirikisha jicho la tatu utatuacha na tatizo miaka michache ijayo tafakari ktk Hilo. Naikikupendeza watumie majasusi wetu kupata ukweli wakile kinaendelea kama nimapicha ama nikitugani sisi tulioko nje hatuoni dalili nzuri.

Mh Rais wasaidizi wako au watu umewachagua sio rafiki zako ila umewachagua kwa minajili kuwatumikia watanzania. Mh Rais vilio na kelele unazisikia sio ndoto ila nikweli embu jaribu pitia vyema report za watu wako wa siri mara mbili mbili na mapendekezo yao. Chambua mara kuchambua kelele unasikia sio kelele za artificial ila niukweli ambao usipo fanya hard decision leo au kesho itakusumbua mbeleni lakini sio lazima kutekeleza.

Mh Rais je unafurahia government expenditures ilivyo Kaa kwa sasa? Embu fanya analysis ya posho,safari na salary bila kuweka gharama ya maintenance za Mali za serikali Kisha uchukue hatua ipo haja chukua hatua ama nionavyo mm base on project serikali inazo mbele uchumi utakuwa kwenye mkwamo hasa hali ya sasa ya vita isipo pata usuluhishi mapema nchi zetu serikali msipo anza funga mkanda mtashindwa kuajiri na pia mtashindwa lipa mishahara. Mbaya kuliko yote nikukosa nguvu yakufanyia manunuzi ya nje ambapo deni letu ktk USD litakiwa likikwangua ukwasi wa fx ktk hazina yetu. Jambo hili litaleta hatari kubwa kwasababu kama huna mavuno yakutosha maana yake huna chakula jambo litakufanya nunua chakula nje. Kumbuka BOP yetu is not balance means exp is low over importation which is high.

Mh Rais ipo siku utapokea wajumbe, wajumbe hawa hawatokuwa watu wakawaida na watakuja nyakati either ya asubuh au mchana kwenye kati ya mwaka 2024 mwisho au 2025. Mh heshimiwa haya ni maono yangu na sitaki kuamini kama nikweli itatokea ama laa. Ila ushauri wangu yasikilize maneno yao ukamuombe Mungu akusaidie kutegua kitendawili amabcho ktk hali ya kibinadam kitakuwa kigumu sana ila kitakuwa na fumbo la hatima ya Tanzania yetu. Usisahau kusema Asante kwa Mungu maana ndie sababu ya kuwepo kwetu sisi wanadam.

Mh Rais naomba niishie hapa kwa leo nitaendelea ikimpendeza Mungu. Asante
Hana muda wa kusoma huu upupu we katafute kazi nyingine ya kufanya kuliko kupoteza muda hapa
 
Acha Acha Acha Acha......
Acha kumtisha Rais na mambo ya kishetani na kipumbavu.
Issue ni kukubali kuwa kama kuna mambo ya kipumbavu ya kishetani lakini yapo kweli na huwa yanatokea, sio watu wote wamejaaliwa uwezo huo wa kuyaona, hivyo nakushauri usiwadharau watu wenye uwezo huo wanapojitokeza kusaidia kushauri!. Swali la kukuuliza wewe ni moja tuu, "jee unamjua TumainiEl ?, unaujua uwezo wake?. Kama humjui na huujui uwezo wake, nakushauri mtembelee humu umjue!.
Rais ana watu wa kila aina wa kumsaidia,
Ni kweli Rais Samia ana watu wa kula aina wa kumsaidia, swali ni jee hao watu wa kila aina wa kumsaidia waliopo, 1. Wanauwezo wa kunsaidia?. 2. Wanamsaidia?. Hata JPM alikuwa na watu wa kila aina wa kumsaidia, jee walikuwa na uwezo huo wa kumsaidia?, jee walimsaidia?. Msidharau watu!.
hahitaji mtu kama wewe mpiga ramli.
Tofautisha wapiga ramli na watu waliojaaliwa maono!.
Waambie na waliokutuma, mmeshindwa.
Tunawajua waliomtuma?. Msilete dharau!.
Mimi namuombea Rais SAMIA awe na afya njema, nampenda sana.
Hata JPM, watu walimpenda sana, na walimuombea sana awe na Afya Njema... lakini...

P
 
Hana muda wa kusoma huu upupu
Vipi wewe mwenzetu, unaijua ratiba yake how busy she is, hivyo kujua ana muda wa kusoma nini humu na nini hana muda wa kusoma?. Maadam humu anaingia mwenyewe, kama kuna mtu ana jambo lolote la kumwambia, mwache aliseme, sasa kama Mama atalisoma au la, hilo sio letu!.
we katafute kazi nyingine ya kufanya kuliko kupoteza muda hapa
Kuna watu if kwao ni kijiwe cha ku past time,na Luna wengine, jf ndio kazini kwetu!.
P
 
Hizi codes jamaa anatumia ni very spiritual. Ukiwa na ufahamu mdogo wa kiroho huwezi elewa. Mimi nimemuelewa. Vitu vingi alivyosema vinatokea na vitatokea. Period!
Wacha kuwa mjinga, bila shaka nyie ndiyo mnaoibiwa kwa kununua mafuta ya upako na mapapai.
 
Back
Top Bottom