Rais Samia usipoangalia mambo mengi ktk Serikali yako kwa jicho la tatu njia itakuwa na miiba mingi sana...

Hili la awamu kurushiana vijembe halijaanza leo; kadri umbilikimo unavyoongezeka katika uongozi wa nchi yetu ndivyo vijembe na mipasho inavyokuwa mtaji wa kujijenga binafsi kisiasa badala ya kujenga nchi! Awamu ya tatu ulishawahi kusikia vijembe dhidi ya awamu ya 2 au 1? Hata mara moja haikutokea. Awamu ya 3 ulishapata kusikia kiongozi akisifia uongozi wake na maendeleo aliyoleta kiongozi mkuu? Hata mara moja hakuna. Badala yake, ilipobidi serikali ndiyo ilisifiwa na siyo kiongozi. Ugonjwa huu wa kujisifu na kupiga wengine vijimbe ulianza kwa mbali awamu ya 4 pale uongozi ulipoanza kuonyesha dalili za kutamani kuipiku awamu iliyotangulia kwa kutoa kipaumbele kwa miradi mipya kabla ya kukamilisha iliyokuwepo. Kwa vile nchi yetu imekuwa ikiongozwa na chama kimoja cha siasa muda huu wote, tunaweza kusema kiini cha matatizo ni hicho chama cha siasa; kimepoteza uwezo wa kusimamia serikali. Sababu ya kupoteza uwezo wa kusimamia serikali ni uwezo mdogo wa kiuongozi wa hao wanaopata uongozi. Kwa bahati mbaya kiongozi mkuu asipokuwa na uwezo wa kutosha mambo mengine mengi huharibika kwani kiongozi mkuu wa chama ndiye huyo huyo mkuu wa serikali. Vyama vya siasa vijitafakari; vione haja ya kugawa madaraka badala ya kumrundikia mtu mmoja. Demokrasia ianzie kwenye vyama. Vinginevyo, atatokea mtu mmoja wa ajabu atajimilikisha kila kitu: chama, serikali, nchi na hata uhai wa raia mmoja mmoja!
 
Tanzania watu ni wavumilivu ila ni uvumilivu unaotokana na makuzi mabaya yaliyojengea watu woga usiokua na maana.

Kiongozi anakosea watu wanamwangalia tu.

Hawamuwajibishi.
Muasisi wa taifa hili alikuwa mtu mwema, mtawala-mwanafalsafa, mzalendo na mtu mwenye upeo mkubwa. Nia yake njema, mapenzi makubwa kwa raia na utu wake vilifanya watu kuwa wa nchi hii kupendana, kuwa wavumilivu na kuuamini sana uongozi kuwa siku zote unao nia njema na uwezo wa kujisahihisha wenyewe bila kupigiwa kelele pale unapokosea. Kama nchi, ilituchukuwa muda mrefu kuona kuwa siyo kweli kuwa uongozi kila wakati unakuwa na nia njema, maono mazuri na uwezo wa kusahihisha makosa yake. Siyo jambo rahisi kwa raia mmoja mmoja kuwajibisha uongozi uliopo madarakani. Kwa kawaida ukosoaji na uwajibishwaji wa raia dhidi ya watawala hufanyika kupitia raia waliojiunga pamoja na kuanzisha vikundi vyao vya kiitikadi, yaani vyama vya siasa. Hapa kwetu kwa msaada mkubwa wa huyo huyo muasisi wa taifa hili, na kama sehemu ya utamaduni wa kujisahihisha alioasisi, tuliamua kama nchi kuurejesha mfumo wa vyama vingi ili raia wautumie kukosoa na kuwawajibisha walioko madarakani. Mwanzoni, walioko madarakani walivipuuza kabisa hivyo vyama na kuendelea na mambo yao kama vile havipo. Lakini pamoja na kupuuzwa vyama shindani viliendelea kufanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kuibua kashfa za serikali na hivyo kujiongezea umaarufu na wafuasi. Walioko madarakani wakabaini kuwa haitoshi tu kuwapuuza washindani; wakabuni mikakati ya kuhujumu wasipate nguvu. Hujuma hizo ni nyingi mno. Lakini pamoja na hujuma hizo bado raia wameendelea kuhitaji vyama shindani na kuviwezesha kukua ingawa kwa kasi ndogo. Hatimaye ikafika mahali walioko madarakani wakaona hujuma peke yake nayo haitoshi; wakaamua kuviua kabisa vyama shindani kwa kutangaza vita hadharani, kutumia nguvu zote za dola waziwazi na hatimaye kupora uchaguzi kwa mtutu wa bunduki! Hivyo tukitaka kweli raia wa nchi hii wachukue nafasi yao ya kuamua namna wanavyotaka kuongozwa, nani awaongoze na kuwasimamia walioko madrakani basi tuhakikishe tunalinda mfumo wa vyama vingi vya siasa. Binfsi naamini baada ya kugundua makosa yetu huko nyuma, Baba wa Taifa hili aliona salama yetu pekee ni vyama vingi vya siasa na kusimamia maono yake hayo kuona kuwa katika uhai wake mfumo huo unarejeshwa, kinyume kabisa na matakwa ya chama alichokiasisi mwenyewe.
 
Nashukuru ila sidhani kama umenielewa. Asante
 
Acha Acha Acha Acha......
Acha kumtisha Rais na mambo ya kishetani na kipumbavu.
Rais ana watu wa kila aina wa kumsaidia, hahitaji mtu kama wewe mpiga ramli.
Waambie na waliokutuma, mmeshindwa.
Mimi namuombea Rais SAMIA awe na afya njema, nampenda sana.
 
Naunga mkono hoja, nakukubali sana.
P
 
Kuna mahali nimemtisha Rais? If yes moderato aufute Uzi ila sijaona mahali nimemtisha Rais soma vizuri
 
Nimeishia hapa siendelei kusoma. Nilifikiriunatoa ushauri mujarabu kumbe wewe ni Sukuma Gang aka Ndumilakuwili? Hamna kitu hapo...una njaa...ukishiba akili zitakurudia.
 
Hana muda wa kusoma huu upupu we katafute kazi nyingine ya kufanya kuliko kupoteza muda hapa
 
Acha Acha Acha Acha......
Acha kumtisha Rais na mambo ya kishetani na kipumbavu.
Issue ni kukubali kuwa kama kuna mambo ya kipumbavu ya kishetani lakini yapo kweli na huwa yanatokea, sio watu wote wamejaaliwa uwezo huo wa kuyaona, hivyo nakushauri usiwadharau watu wenye uwezo huo wanapojitokeza kusaidia kushauri!. Swali la kukuuliza wewe ni moja tuu, "jee unamjua TumainiEl ?, unaujua uwezo wake?. Kama humjui na huujui uwezo wake, nakushauri mtembelee humu umjue!.
Rais ana watu wa kila aina wa kumsaidia,
Ni kweli Rais Samia ana watu wa kula aina wa kumsaidia, swali ni jee hao watu wa kila aina wa kumsaidia waliopo, 1. Wanauwezo wa kunsaidia?. 2. Wanamsaidia?. Hata JPM alikuwa na watu wa kila aina wa kumsaidia, jee walikuwa na uwezo huo wa kumsaidia?, jee walimsaidia?. Msidharau watu!.
hahitaji mtu kama wewe mpiga ramli.
Tofautisha wapiga ramli na watu waliojaaliwa maono!.
Waambie na waliokutuma, mmeshindwa.
Tunawajua waliomtuma?. Msilete dharau!.
Mimi namuombea Rais SAMIA awe na afya njema, nampenda sana.
Hata JPM, watu walimpenda sana, na walimuombea sana awe na Afya Njema... lakini...

P
 
Hana muda wa kusoma huu upupu
Vipi wewe mwenzetu, unaijua ratiba yake how busy she is, hivyo kujua ana muda wa kusoma nini humu na nini hana muda wa kusoma?. Maadam humu anaingia mwenyewe, kama kuna mtu ana jambo lolote la kumwambia, mwache aliseme, sasa kama Mama atalisoma au la, hilo sio letu!.
we katafute kazi nyingine ya kufanya kuliko kupoteza muda hapa
Kuna watu if kwao ni kijiwe cha ku past time,na Luna wengine, jf ndio kazini kwetu!.
P
 
Hizi codes jamaa anatumia ni very spiritual. Ukiwa na ufahamu mdogo wa kiroho huwezi elewa. Mimi nimemuelewa. Vitu vingi alivyosema vinatokea na vitatokea. Period!
Wacha kuwa mjinga, bila shaka nyie ndiyo mnaoibiwa kwa kununua mafuta ya upako na mapapai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…