Ngungenge
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 2,953
- 3,459
Baadhi ya watu wachache tunajulikana na "kujiapiza" kukusemea mazuri na kukuombea kwa Mwenyezi Mungu na hakika Jamii imeanza kuelewa nini hasa umedhamiria kutufikisha.
Ukuaji wa uchumi na ustawi wa maisha ya watu ni kipimo tosha Cha mafanikio unayoyapata katika uongozi wako. Hongera Sana!
Hili jambo lililosemwa bayana na ukakiri kuwa baadhi ya watu hawaitakii mema nchi yetu, watu hao wasio na aibu, wasio na hofu ya Mungu, wasio na hofu na mamlaka ya Rais, wenye ubinafsi huo, roho ya wizi, tamaa za mali na ufisadi, wamethubutu tena bila wasiwasi wowote kuiba, kudanganya, kupanga njama juu ya mali za watanzania. Utafanyaje na watu hawa?
Sio kwamba watanzania wako kimya ila manung'uniko ni mengi kuwa hakuna kitu kitafanyika dhidi ya watu hawa.
Rais Samia, utafanyaje Ili jambo kwa faida ya watanzania na chama chetu CCM?
Utafanyaje Ili wajue angalau kwa hofu waogope kuwa somo limesomeka na wanaokusudia kuiba waogope utafanyaje jambo hili?
Je, kuna hofu zaidi ya hofu ya Mamlaka ya Rais?
Je, bado waendelee kukaa ofisini huko kupanga njama na kuiba bila maumivu yoyote? Utafanyaje jambo hili lisiendelee?
Rais Samia, utafanyaje?