TBC kuna tatizo sana. Siamini hadi leo hakuna watu wanaoweza kuchanganya picha za TV zikaleta maana. Sehemu imeonyeshwa bendi ya JKT, watu wakisikia matukio ya kushangilia bila kujua nini kimetokea.
Wageni wanatambulishwa kamera inaonyesha mtu amesinzia upande mwingine.
Hawana hata vi-drone vya kuchukua picha kutoka kona tofauti na wala hawajui nini waonyeshe.
TBC ni mswaiba kubwa. Haya huwezi kuyaona hapo jirani Kenya. Shame on you TBC kwa uzembe uliotukuka.
Ukimsikiliza Mtangazaji hakuna anachomuuliza Afisa wa Jeshi aliyepo studio.
Tulitegemea kusikia maswali yakihusu Gwaride, ni nani anaongoza na cheo gani, kwanini sajenti awe katikati ya maafisa wenye upanga na mambo mengi tu! Watangazaji walikaa kimya wakisiliza matarumbeta.
Hii ni aibu sana kwa Taifa
Hivi hakuna TV nyingine zenye watu wenye weledi wa haya mambo.
Yaani ukiwasikiliza RTD ya akina Seif Mkamba, David Wakati, Sekioni Kitojo, Halima Kihemba, J.Tesha, Mfamao (RIP) na wengine wengi utaona tofauti kubwa. Walifanya home work zao wakijua wanazungumzia nini na nani.
Ikiwa ni gwaride watakupa kila maelezo ya nini kinafanyika na kwanini. Nikitazama TBC nasikia haya
Shame on you TBC, hamna thamani ya kodi zetu. Aibu tupu
Wakubwa njooni tuomboleze TBC
Pascal Mayalla JokaKuu Mag3