Rais Samia: Vijana waliopita JKT wanapaswa kubeba uzalendo wa Nchi moyoni na sio mdomoni

Rais Samia: Vijana waliopita JKT wanapaswa kubeba uzalendo wa Nchi moyoni na sio mdomoni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho va Miaka 60 ya JKT katika Uwanja wa Jamhuri - Dodoma leo terehe 10 Julai, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema vijana wanaopita JKT wanapaswa kubeba uzalendo wa Nchi moyoni na sio mdomoni mwao na kuwa tayari kulinda, kupigania na kutetea nchi.

Ameipongeza JKT kwa kuendesha mafunzo mazuri ya utimamu kwa vijana, kuendeleza ujuzi wao pamoja na kutengeneza ajira, kupunguza kiwango cha umaskini pamoja na utegemezi.

Lengo la Serikali ni kuongeza uwezo wa JKT iweze kutekeleza majukumu yake vizuri hasa kwenye nyakati hizi ambazo mwamko wa vijana kujiunga na jeshi hilo umekuwa mkubwa.

View attachment 2683776
Gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) likipita kwa mwendo wa pole na haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

View attachment 2683778
View attachment 2683779
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
View attachment 2683785
Labda jkt ya sasa, lakini ile tuliyopitia ya julius, mmh! Tulihitimu na kufuzu kusema na kufanya uongo, unafiki, wizi, utoro, uzembe, na mambo mengine mabaya yanayofanana na hayo. Kuhakiki hili ninalosema, kwani mafisadi wanaoitesa Nchi si wale " wazalendo" wahitimu wa jkt tena ya julius.
 
Back
Top Bottom