Rais Samia: Viongozi wa Serikali mjitathmini

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Serikali kujitathmini kwa nafasi zao kama wana maadili ya uongozi.

Rais Samia amezungumza hayo alipofanya mkutano wa faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha leo Machi, 02 2023.

“Watu tunao, ardhi tunayo na siasa safi ipo, suala la kujadili ni kuhusu uongozi bora, baada ya kumaliza kikao kazi hiki kila mmoja ajitathmini kama maadili ya kiongozi bora tuliyoambiwa yapo au laa.” Amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema lengo la kikao hicho ni kuelekezana juu ya kutimiza ipasavyo wajibu wa viongozi na dhamana waliyonayo ya kuwatumikia Wananchi

Rais-Samia.jpeg
 
Nadhani mtu wa kwanza kujitathmini ni yeye, imekuwaje nchi imetekwa tena na mafisadi na majizi yanayosababisha ugumu wa maisha kwa watu wa kawaida?
 
Hivi Chamwino ilijengwa kwa Kazi gani?!... manake kuna kipindi nasikia wanafanya vikao vya Baraza la Mawaziri pale, wakati mwingine wanaapishwa viongozi, na juzi waliapishana pale, na naambiwa Chamwino ni kubwa kuliko ikulu ya Dar, inaelekea Chamwino hakuna Faragha...SAD
 
Nadhani mtu wa kwanza kujitathmini ni yeye, imekuwaje nchi imetekwa tena na mafisadi na majizi yanayosababisha ugumu wa maisha kwa watu wa kawaida?
Uongozi Bora ni pamoja na kutumia rasilimali za nchi kwa umakini mkubwa.
 
Mkutano wa faragha imekuaje umetufikia wananchi.

Makatibu na manaibu wazo, wizara na manaibu wao wote wamekutana arusha kuzungumza.

Nafikiri kunaaja ya serikali kuanza kutumia mifumo ya kidigitali kufanya baadhi ya mikutano kama iyo.
 
Kudekezana Tu, Mpaka Mwisho Yaani Jipya Kuliona Sijui
 
Back
Top Bottom