Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Alaaaah, kumbe wafanyabiashara walichoma soko la Kariakoo wenyewe? Hii ndio sababu hatujui ndani ya kilichokuwemo kwenye ripoti rya tukio la moto ule?
======
Moja ya mambo aliyosema mwenyekiti wa kariakoo katika risala yake ni kuhusu ziara ya Samia Kariakoo, ambako alisema Rais Samia alifika Kariakoo mara moja, wakati haikuwa hivyo. Rais Samia alimrekebisha kuwa alifika mara mbili na kuongezea kuhusu kuungua kwa soko la Kariakoo.
“…. Amesema alinianialika Kariakoo kasema kwamba umekuja Kariakoo mara moja tu nataka nimkumbushe nilikuja Kariakoo kusalimia wafanyabiashara na mara baada ya kuondoka siku 2 baadaye soko mkalitia moto, na mlilitia moto kwasababu nilizisema changamoto za uongozi uliookuwepo na mambo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya soko na kuwataka vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi ndani ya soko
“Sasa ili kupoteza ushahidi mkaamua kutia moto lile soko. Kwahiyo hiyo ilikuwa ziara yangu ya kwanza. Lakini kwa ujasiri nikasema nalijenga tena hili soko.”
Rais Samia ameyasema hayo leo Januari 30, 2025 alipokuwa katika hafla ya chakula cha mchana na waliosaidia kwenye zoezi la uokoaji wakati wa ajali ya kuporomoka soko la Kariakoo.