Hongera Raisi wetu kwa kazi unayoendelea nayo! Ni ukweli unahitaji kuitiwa moyo pia maana hujipambanii wewe, unapambania watanzania, ijapokuwa mama yetu ni kwamba,
Watanzania tunalia na wasaidizi wako, macho yao walio wengi yapo kiupigaji tu na lugha nzuri wajapo kwako!
Mf, wizara ya mawasiliano haipo sawa na imeshamshinda waziri wake! Kjnachofanywa na wizara hii ni wao na watendaji kujinufaisha!
Je, ipo sababu yoyote ya upandaji wa Matumizi ya Internet? Internet ilipokuwa iko chini, kulikuwepo hasara gani? Hakuna maelezo, huo sio upigaji na kuwapa mzigo watumiaji? Au jambo la internet nalo linataka Liwe linatumiwa na vigogo peke yao na wananchi wa kawaida wasipate tarifa na kupashana Habari kwa njia ya mitandao?
Wizara ya Nishati
Kwa nini siyo wakweli kwenye kutoa tarifa zao kwa wananchi? Tukiambiwa leo kwamba tatizo la kukatika umeme, litaisha baada ya wiki mbili, wiki mbili zikiisha. Lazima waje na sababu zingine tena, shida inabaki palepale, leo hii ipo tarifa ya kufumliwa mtandao wote wa gridi ya Taifa, yaani likiisha hili linazaliwa lingine hapohapo, mambo haya yameleta hasara kubwa sana kwanchi na kwa wawekezaji wetu, si hivyo tu, linafanya wawekezaji kuogopa kuwekeza ktk nchi yetu kwa sababu tu ya kutakuwa makini kwa wizara hii nyeti
lingine ni kwamba; umeweza mengi sana mh na Rais wetu, na bado unaweza!
Lililopo kwa sasa ambalo ndilo maisha ya kila mtu, ni hili la nafaka kuwa ghali sana kiasi kwamba linazidi uwezo wa kipato cha mtanzania kwa sasa!
Jambo hili litazamwe kwa kina! Linajaza hasira wananchi kwa sababu ljnawanyima usingizi, linawalaza njaa na kuwashindisha njaa.
Kwa hili, halina faida yoyote kwa mkulima wala mlaji! Kwa sababu mkulima atauza kweli kwa bei ghali, lakini na yeye mahitaji mengine atayapata kwa bei ghali vilevile.
Ughali wa maisha utafutiwe dawa, penye nia hapakosi njia.