GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Muheshimiwa Rais,
Bila shaka una taarifa juu ya mauaji yaliyofanywa na maafisa 7 wa Polisi. Ni taarifa ambayo imewashtua wengi kwa kuwa imetoka hadharani lakini tabia hii ya ujambazi na kudhulumu mali za watu haikuanza leo wala Jana na bila kufanya Reform ya Jeshi la polisi mkoa wa Mtwara (huko kwingine sijui) Haitakwisha.
Muheshimiwa Rais, Polisi mkoa wa Mtwara waliwahi kuendesha zoezi la kukamata matajiri au niseme watu ambao wanajiweza kidogo kiuchumi katika wilaya na vijiji vya mkoa wa Mtwara, walifanya hivyo baada ya kunusa information zao mbali mbali za kibenki na kiuchumi kiujumla. Watu hao waliteswa na kutishiwa maisha iwapo wasingetoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kiliombwa na maafisa wa Jeshi la polisi. Walibambikiwa kesi kubwakubwa na mpaka wanaachiwa wengine walirudi wakiwa na athari za kiafya ambazo zilichukua uhai wao.
Katika mji mdogo wa Mahuta yupo mfanyabiashara alikuwa anaitwa Uheche, huyu alikuwa mmiliki wa mabasi ya Mahuta express naye ni miongoni mwa waliokamatwa kadhia ambayo ilipelekea kuharakisha kifo chake kwani alikamatwa akiwa na tatizo la kisukari na kuishi mahabusu mazingira ambayo hayakuwa rafiki kwa tatizo lake.
Wengine ambao wamewahi kukamatwa ni Ibadi wa Newala (mfanyabiashara na mkulima), Uheche (marehemu), Tutu (mkulima mkubwa wa Korosho) na wengi wengineo.
Pamoja na kamatakamata ya pikipiki ya kila siku pia Polisi hasa wilaya ya Tandahimba na Newala wamekuwa na tabia ya kuiba vifaa vya pikipiki zinapokamatwa na kukaa vituoni.
Si hivyo tu Polisi kutoka Mtwara mjini baadhi ya siku huanzisha operesheni za ghafla za Kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa na kuanza kukamata pikipiki kuku wakiweka kiwango cha elfu 90 mpaka laki na nusu bila kujali makosa na pesa hizo huchukuliwa wakati mwingine bila risiti.
Muheshimiwa Rais, tayari tuna matatizo ya mpakani ambayo kwa kiasi kikubwa yamedhibitiwa na Jeshi la wananchi, Hili la polisi tunaomba msaada wako.