Rais Samia, wakulima wa Miwa wanatishia kukibomoa Kiwanda cha Sukari cha Mbigiri

Sasa mtamfanya huyu mama ikifika 2025 akimbie hicho kiti.
 
Naomba niulize swali:

Hivi hakuna uwezekano wa kuiuza hii miwa ikasindikwe kwenye kiwanda kingine kilicho karibu na sehemu hiyo?
 
Mazindu, nimekuelewa vyema sana na hayo uliyoandika kwenye mstari wako huo wa mwisho.

Na ili ifahamike vyema na kila atakaye kujua: "Serikali haiwezi kufanya biashara"!

Keshokutwa ikiamriwa kiwanda hiki kibinafsishwe, kitageuzwa kiwe 'Godown' la kutunzia sukari iliyoagizwa toka nje!
 
Mada yako umeiharibia hapa.

Hukutumia tafakuri madhubuti kuyaandika haya.

Hili siyo suluhisho; bali ni kuongeza ukubwa wa tatizo lililopo.
 
Kabudi hakufanikisha manunuzi ya korosho,alileta kampuni ambayo ilithibitika kuwa ahina uwezo wa kununua korosho na hazikununuliwa.
 
Mada yako umeiharibia hapa.

Hukutumia tafakuri madhubuti kuyaandika haya.

Hili siyo suluhisho; bali ni kuongeza ukubwa wa tatizo lililopo.
Inawezekana mawazo yako yapo sawa, lakini si sahihi.
 
Ulikuwa ukisoma matangazo ya kazi ya hapo Mkulazi utahisi kiwanda kilifunguliwa siku Nyingi.
Ujanja ujanja mwingi lakini akili hakuna.
 
Naomba niulize swali:

Hivi hakuna uwezekano wa kuiuza hii miwa ikasindikwe kwenye kiwanda kingine kilicho karibu na sehemu hiyo?
Uwezekano hupo, na hata baadhi yao wamefanya hivyo. Maana baada ya hali kuwa mbaya sana ilibidi kipengere fulani cha mkataba kibadirishwe na kuwaruhusu wakauze Mtibwa.

Tatizo ni kwamba;
1. Kiwanda cha Mtibwa hakina huwezo mkubwa maana hata 'outgrowers' wa Mtibwa huwa wanagombea nafasi ya kuuza miwa pale.

2. Gharama ya usafirishaji kutoka Kilosa mpaka Mtibwa ni issue, inaongeza gharama nje ya mkataba.
 
Ulikuwa ukisoma matangazo ya kazi ya hapo Mkulazi utahisi kiwanda kilifunguliwa siku Nyingi.
Ujanja ujanja mwingi lakini akili hakuna.
Ni upuuzi mtupu. Siasa nyingi hakuna hualisia.
 
Ni upuuzi mtupu. Siasa nyingi hakuna hualisia.
Maisha haya fedha nyingi zinapotelea pahala then watu kimyaaa.
Mkoa tu huo wa Morogoro mpaka sasa kuna sehemu hazifikiki ki barabara wala mawasiliano.
Sukari yenyewe kila siku inapanda bei.Roho mbaya za mtu Mweusi ni shida na laana.
 
Na mbaya zaidi sehemu ambazo hazifikiki ndizo "productive" mfano Malinyi, Kisaki, kinole.

Utasikia barabara hii ipo chini ya TARURA.....ni upuuzi mtupu.
 
Na mbaya zaidi sehemu ambazo hazifikiki ndizo "productive" mfano Malinyi, Kisaki, kinole.

Utasikia barabara hii ipo chini ya TARURA.....ni upuuzi mtupu.
Ndani ya Mkoa unakaa masaa kumi na mbili kufika ..halafu unasikia uchumi wa kati.
Malinyi kule wangefikishiwa Lami ya Uhakika au Ilonga huko.Upuuzi mtupu..unaenda kujenga ujinga.Kilombero ,,Mtibwa Kagera na Moshi TPc zinafanya nini?
 
Nchi ngumu sana hii Adrenaline(emegency gland).

Pale Msowero watu wamelima miwa, lakini barabara ya kupita gari likabebe miwa ni mbovu.
Kabudi kaitwa juzi kama mbunge, hakwenda katuma mwakilishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…