Rais Samia: Waliosema nimeuza Bandari na Bahari faida yake ndio hii

 
Hayo mapato yamekusanywa na TPA au ni gawio kutoka kwa mwekezaji DP World? Kama ni kutoka kwa mwekezaji DP World, kwa nini ameipongeza TPA? Kama ni makusanyo ya TPA, kwa nini aseme ni matokeo ya kuuza bandari?
 
Kea hiyo a me kiri kwamba Bandar I kauza.
 
Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini Mh wetu mkuu, Mama yetu amesema hayo maneno. Sijataka hata kufungua hii clip, nimesoma tu andiko ili nisiendelee kusikitika na kuhuzunika.

Hivi unahitaji PhD kutohusisha gawio hili na kuboresheka,kuongezeka kwa efficiency na kuongezeka kwa faida (profits) kwa institution hizi za Serikali. Sitaongelea suala la gawio la mashirika ya umma .e.g TTCL miaka ya mwendazake , kesho yake tukaambiwa wanatemblea makuti karibu na mfilisi kwa deni kubwa la mabillioni, mara zaidi ya tano ya gawio; maana yake hata gawio walilolitoa wametoa kama sehemu ya deni ili kushow-off their contribution (nyie watu wa uhasibu mnajua sijui walitoa kwenye debt account nafikiri inatakiwa gawio litoke kwenye credit)

Sasa mama yetu Watanzania wameamka, sio watu wa zamani, na watanzania wengi sio watu wa Pwani,tunapoingiza Uswahili na vijembe kwenye mambo makubwa of national interest ndipo tunashindwa kuelewa aina ya kiongozi tuliyenaye.

Juzijuzi tu tumeona andiko la kupanda mara zaidi ya 340% kwa kodi bandarini na halikuwahi kupingwa na chombo chochote serikalini kwa hiyo ni kweli soon tunakiona cha moto. Kumbuka ongezeko hili lukuki ni kodi ambayo inakwenda kumuumiza mwananchi wa kawaida moja kwa moja.

Sasa leo tukiona hizi divident (gawio kubwa kubwa ) ni ukweli husiopingika hii ni sanaa, sasa basi snaa hii ingepakwa angalau mafuta, ni sanaa inachezwa kavukavu bila aibu. Jamani nchi yangu Tanzania tunaelekea wapi Jamani? Hivi hakuna wataalamu wa propaganda na high level community hypnotizers ndani ya chama wa kuwashauri nini cha kufanya, nini cha kutofanya au kifanyike vipi? Hii ni kututia aibu Watanzania kutuchukulia woooooote ni mazezeta.
 
Kwani DP World wameanza kazi lini? Je tangu waanze kazi ndo wamechangia hilo ongezeko? Maigizo kama kawaida yetu #BongoM*vi
 
Waulize vyura wa Chadema kama amesema au hajasema πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/reel/C8EyloDMEyk/?igsh=MXFlY3ltMnA0dm85eQ==
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…