My Take
Mlisema Samia ameuza Bandari Kuna bango lenu hili hapa, ni spana tuu Kwa kwenda mbele.
View: https://www.instagram.com/p/C8Ht26kMeDf/?igsh=eWlxY2ljY3I3YnZ6
Tafuteni hoja nyingine 👇👇
“TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) mwaka jana (2023) nina hakika kiwango chenu hakikuwa hiki, lakini kwa mageuzi yaliyotokea bandarini mmeweza kufikia kiwango hiki na mwakani tunatarajia kiwango kikubwa zaidi pengine mara mbili yake ya hiki mlicholeta leo, hakuna sababu kama mtaendesha bandari na sekta iliyopo pale na pale kuna watu wawili ambao tumeshawaruhusu.
Mmeomba maombi zaidi lakini hata wale wawili mwakani mnaweza kuleta mara mbili ya hiki kiwango na huko ndiko tulikuwa tunaelekea ndugu zangu . Wale waliopiga kelele mama kauza bahari sijui mama kauza bandari mama kauza nini mama kauza..mauzo yale faida yake ni hii hapa leo, na huu ni mwanzo tutatarajia kutapata faida kubwa zaidi kwa bandari zetu zote kubwa ambazo zipo ndani ya nchi”- Dkt. Samia.
View: https://www.instagram.com/reel/C8E2TrhNxHA/?igsh=MWNhMXI1cWM2dGVvMQ==