Kama kauli hii kaitoa rais SSH tayari ameshapoteza mwelekeo hakuna atakayemchagua Mbeya, Mwanza, Arusha na Dar Es Salaam
Utajitangazaje utagombea urais wakati una miezi sita tu tangu ushike madaraka ya ngekewa
Kauli gani gani yenye ukakasi kama hii?
Kwa hiyo JPM aliangamizwa na nini ili wadai ni kudra ya menyezi Mungu wachukue nafasi ya urais?
Kwa hiyo hata madai yanayodaiwa kwamba JPM alihujumiwa ni kweli na yeye anajua?
Wanawake anaojifariji watampigia kura ndio hawamtaki kabisa kumsikia lakini wanamg'ong'a
*She will never be voted by anybody nor win the general election race come 2025.
"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana
Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.
Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani"
Hii kauli amewadhalilisha sana wanaume kwa kujiona anauwezo na nguvu cha kufanya chochote kwa raia wa nchi-NO