Raia wa mwisho kuwa Rais wa Tanganyika kutoka Zanzibar alikuwa ndugu Ally Hassan Mwinyi. Baada ya hapo CCM wakaweka kizuizi kwa raia yeyote kutoka Zanzibar asigombee urais na badala yake Zanzibar ikatakiwa iwe inatoa mgombea wa Makamu wa Rais tuu kwa kila Chama Cha siasa hapa nchini.
Imefanyika hivyo Mkapa akiwa mgombea, Kikwete akiwa Mgombea na hata Magufuli akiwa Mgombea Zanzibar kazi yao ni kutoa wagombea wenza tuu. Kwa maana nyingine ni kuwa ili Mzanzibari awe Rais wa Tanganyika itabidi asubirie kudra za mwenyezi Mungu Rais wa Tanganyika akifa.
Ni kwa nini CCM hawataki Rais wa Tanganyika atoke Zanzibar wakati KATIBA inasema sifa ya mtu kuwa Rais ni awe raia wa kuzaliwa wa Tanzania? Hapo ndipo wenye Akili tunapo eleza utata wa Muungano huu feki japo CCM haitaki kueleza wazi kuwa raia wa Zanzibar anakosa sifa ya kuwa Rais wa Tanganyika ila wakaficha maradhi hayo kwa muda mrefu. Waswahili wana msemo kuwa mficha maradhi kifo kitamuumbua na kifo kimewambua kweriii kweriii.
Wiki iliyopita niliandika mada ngumu hapa kuhusu WAZANZIBARI. Nikasema kwa maoni yangu naona wanzanzibari sio Watanzania mada ikafutwa wenye Akili wakanielewa kwa vigezo hivi nilivyo eleza.
Nikaeleza kuwa Zanzibar ilikubali kuungana na Tanganyika ili waunde taifa moja la Tanzania. Lakini Zanzibar ikagoma kuua taifa lao huku Tanganyika ikafa na kuunda Tanzania taifa jipya. Hivyo Tanzania imezaliwa baada kifo Cha kikatili Cha Tanganyika na sio Muungano wa nchi mbili.
Lakini pia nikaeleza kuwa Zanzibar ni nchi huru, yenye mipaka yake, Serikali, Bunge, Mahakama na pia KATIBA na wimbo wa taifa. Zanzibar sio sehemu ya Tanzania Kama CCM wanavyotaka kutuhadaa kutuona wananchi ni mazuzu tusio jitambua. Sehemu yeyote iliyopo Tanzania haiwezi ikawa na Rais, Serikali yake,Bunge Mahakama, KATIBA, wimbo wa taifa lake na Bendera ya taifa.
Ni mwenda wazimu tuu anaweza kuamini kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Ikiwa Bukoba, Iringa, Mbeya, Tanga hizi ni sehemu za Tanzania na hazina Rais wao, Serikari, Bunge, Mahakama, Bendera ya taifa wala wimbo wa taifa basi utakuwa ni ubashite wa hali ya juu kusema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.Hakuna taifa hapa Duniani ni sehemu ya taifa jingine. Sijui mwanipata uzuri ninyi wadanganyika?
Ukweli mchungu ni kuwa WAZANZIBARI sio Watanzania wanalazimishwa tuu kwa malengo mficho. Msema kweli mpenzi wa Mungu na ni lazima tuambiazane ukweriiii.Huu sio wakati wakupakana mafuta kwa mgongo wa chupa. Samia aambiwe ukweli hana sifa za kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika. Akagombee kwao Zanzibar Kama anataka urais.
CCM wanayo kazi moja tuu Mbele kuifanya Zanzibar ikawa ni Jimbo au Mkoa wa Tanzania au kuirudisha Tanganyika zikaundwa Serikali tatu. Hatuwezi kuacha kulidai taifa letu la Tanganyika kwa sababu zozote zisizo na mashiko. Tutaendelea kulidai taifa letu la Tanganyika tena kwa wivu mkubwa.
Back Tanganyika.