Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Sina hakika kama huu ulikuwa muda muafaka kwake kutangaza nia ya urais 2025 kwa sababu watanzania bado wanaomboleza. Nadhani washauri wake hapo wamempotosha, alipaswa achape kazi tu kwa sasa then two or one year before uchaguzi angekuwa na sababu (jamani naombeni mnipe lizaa nimalizie yale ambayo nimeyaanza). Ila kwa sasa inaonekana kama vile yalipangwa yaliyotokea ili yeye iwe hivyo alivyo na ni furaha kwake! Sijui ila inafikirisha sana huo uharaka.
 
Vigazeti vya Chama cha CCM😅😅😅
 
Jiwe na ukatili wake na ubabe wake Ila jasho lilimtoka 2020.
Huyu bibi hangaya Hadi kufika hiyo 2025 atakuwa kishasusa

Mmoja alikuwa anajichosha na masafari na push up nyingi
Mwingine ni mwendo wa ndege tu
Sasa mchoko utoke wapi
Isitoshe hapigi kelele wala hasira


Ujue hasira nyingi zinaleta maradhi
 
"Nataka niwaambie wanawake bado hatujaweka Rais Mwanamke, Rais mwanamke huyu amekaa kwa sababu Kudra ya Mungu, na matakwa ya Katiba...Rais Mwanamke tutamuweka mwaka 2025...wameanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti, Samia hatasimama, nani kawaambia?".Rais Samia.
 
Mwenyezi Mungu amjaarie mama yetu aliongoze taifa hata miaka 30 sawa tuu. Tunakupenda mama samia, mama mwenye huruma, anapenda matajiri, masikini na ni rais wa wanyonge pia,,,
 
Lakini katiba haimpi nafasi ya kugombea. Labda aibadili.
Inampa nafasi ya kugombea ingawa ni kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano.Kwa hiyo ni 2025 had 2030 .Hata hivo anajifrahisha tu Ukweli anaujua hawezi kugombea.
 
Huyu mwanamke nae ana nyodo kweli.Ndo maana akaolewa mke wa tatu.
 
“Rais mwanamke tutamuweka mwaka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia? - Rais Samia Suluhu Hassan

#UnokoNiUzalendo

 
Umesoma Katiba ya wapi? Unaijua Katiba yetu ya 1977 kweli ww?
Kama vile naona hoja kwa mbali!!!
Hivi mtu akisema uchaguzi wa 2020 ndio umetupa huyu rais aliyepo sasa atakuwa sahihi au hapana!?
Kama atakuwa sahihi, si ni kipindi cha pili? ...maana sote tunajua urais ni taasisi na sio mtu. Kama hapana basi msiwabeze wanaotaka hiyo katiba ya wananchi.
 
Wasalaam
Ndugu wanajamii mmesikia huko (wanawake wanaweza)..
Kwa ufahamu wangu na Mungu akitujalia Kwa haya ninayoona hakika 2025 ni Mama Samia

CCM oyeee, Mama oyeee sasa Kazi iliyobaki ni kuweka uwanja Sawa wa kidemokrasia..

Kwa haya ninayoona Kwa Kazi hizi Kwa muda huu mfupi kwakweli nitakua waajabu kama nisiposema
Samia 2025 twende

Nani kama mama hivi kuna linaloshindikana Kwa Mama, nimefurahi kwenye siku hii muhimu kuonyesha mwelekeo wako Mama Samia!!

Hongera Kwa uteuzi wa Mawaziri hawa wapya, tunasubiria wakuu wa mikoa na wilaya pia wakuu wa Idara Mbali mbali za serikali wabadilishwe,hawaendi na maelekezo na dira yako Mama!!
 
Ameshaanza kupandisha mabega anaamini kuwa ameshalisambaratisha Sukuma Gang.
Sukuma gang ni Kama maji.
Huwezi wasambaratisha Labda aungane nao.
Tangu aingie madarakani katembelea Sukuma gang Mara nyingi kuliko hata Msoga kwa mshika usukani.
 
Hata kwa dawa hawezi kupata kura yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…