Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.


Alisema Rais Samia Suluhu


Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Samia Suluhu Hassani kwa namna moja au nyingine ana jubilate kifo cha Dokta John Pombe Magufuli au siyo ?
 
Akili ndogo ndiomaana umenichukulia kama mdini, licha ya kuwa nimeongea mengi tu ila umechukua hicho kipande na kunihusisha na Gwajima ambaye hata hakuwa msingi wa hoja yangu.

Wewe kaa usubirie hoja mserereko zinazoendana na level ya ubongo wako,Ili userereke nazo.

Nikupe idadi ya wanaomchukia? Haya Unashindwa hata kupita maoni ya watu?

Haya wewe nipe idadi ya wanaompenda.

Tanzania ina population ya watu zaidi ya m60. Ukisema ufuatilie maoni ya watu mitandaoni wanaomchukia hawafiki hata 1000 wanaomsema vibaya, sawa na idadi ya mtaa/kitongoji.

Samahani kukukwaza kuusu gwajima n.k.
 
Kwangu mimi wote wako sawa,,, kwanza unaposema Mwinyi ana kaubara na ssh hana ubara tayali ushatia kaubaguzi flani ivi.


Ivi ingetokea Gaddafi akaja kuiongoza Tanzania ungekataa? Sasa kwanini umkatae mama samia kwakuwa ni mzanzibari!!!!


Mama yuko poa
Mwinyi yuko poa

Tuendelee kumpa muda,,,nchi itakaa sawa na wenye midomo mirefu waufyata.
Mama nilimpenda sana sana, lakini kanigusa direct na tozo, petroli kupanda miezi michache tu baada ya jiwe kufa, mafuta ya kula nk. Nawaza mpaka 2025 si tutakufa watz!!! Vitu vinapanda hatari.
 
upinzani wangekuwa makini hii ni fursa nzuri sana kwao kwani ccm kundi kubwa hawamtaki yuko hapo kwa matakwa ya kikatiba na jaribio loote la kuzuia wagombea wengine hili yeye agombee litaleta mpasuko mkubwa, hizi nafasi huja kwa nadra sana
 
Nililia sana Jiwe alivyokufa. He was a human being hata kama kuna vitu alikosea sana. Sikuelewa raisi aliyeko madarakani anakufaje! With all the protection, health guidelines etc. ilisikitika mkuu sikufarahia. Unajua hata adui akifa huwa tunasikitika. Huwezi kulinganisha uhai wa mtu na kitu chochote!!!

10 tenaaaa
 
Lakini katiba haimpi nafasi ya kugombea. Labda aibadili.
Unaielewa katiba yako kweli wewe au na bwabwaja tu mitandaoni,katika inamruhusu chief Hangaya kuingiza kwa miaka mitano baada ya kumalizia huu mhula.All the best chief Hangaya
 
Nililia sana Jiwe alivyokufa. He was a human being hata kama kuna vitu alikosea sana. Sikuelewa raisi aliyeko madarakani anakufaje! With all the protection, health guidelines etc. ilisikitika mkuu sikufarahia. Unajua hata adui akifa huwa tunasikitika. Huwezi kulinganisha uhai wa mtu na kitu chochote!!!
Marais wa huko dunia ya Kwanza wanakufa wakiwa madarakani sembuse huku nchi za maskini?
 
Mama nilimpenda sana sana, lakini kanigusa direct na tozo, petroli kupanda miezi michache tu baada ya jiwe kufa, mafuta ya kula nk. Nawaza mpaka 2025 si tutakufa watz!!! Vitu vinapanda hatari.

Kwenye swala la tozo limetugusa wengi mkuu,, lakini naimani nae uyu mama ipo cku ataliweka sawa,,, na uzuli pesa zinazokusanywa za tozo zinawekwa wazi na zinaenda kwenye miradi. Kuusu kupanda bei zsa mafuta navojua mimi mkuu ni duniani kote na co Tanzania tu. Unazani nani anapenda vitu/bidhaa zipande bei!!! Hali ngumu sana,, na corona ndiyo imesababisha vitu kupanda bei, moja wapo mafuta.
 
Watajitokeza wengi kutangaza nia, sasa sijui wataitwa na kamati kuhojiwa kwa kutangaza kabla ya muda? Hii italeta mkanganyiko
 
Mama kaamua kupima oil.

Si tulikubaliana rais ni mwezi wa kwanza imekuwaje tena?
 
Miezi sita tu ameshaanza kutamani kusalia madarakani, uraisi raha jameni.

Kwani kipindi cha kampeni tayari?
 
Kumbe jpm was kudra?? So it's possible and confirmed?? Saw bhana..
Amejichanganya sana kuongea hadharani kauli hiyo ambayo ndio itachochea zaidi inda dhidi yake......kwa sasa watamchimba sana na kumtaka aeleze kwanini wakati mtangulizi wake yuko mahututi anaumwa yeye alianza ziara mikoani? Kwanini hakurejea haraka Dar kuthibitisha taarifa za kifo alichopewa usiku ndio atangaze?

"Carrot or Stick leadership style won't help anything in the forthcoming political battle-field
 
Back
Top Bottom