Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

CCNM ina nafasi kubwa sana ya kushinda 2025.

Wanyonge wanaopenda kuwa wanyonge na kufanyiwa kila kitu kwenye mbeleko na kuchangiwa kodi na wachache pamoja na wingi wao ukweli mchungu ni kuwa wajiandae kulalamikia serikali na kuitukana watakavyopenda.

Wale wafanyabiashara, wafanyakazi na walipakodi kuna nafasi kubwa sana ya kutimiza ndoto zenu kipindi cha samia.

Wanasiasa wasiojua kunufaika na upinzani watapata tabu sana. Hapa naongelea wale wa matusi tu na kuiponda serikali bila kujua kutumia fursa zilizopo.
 
Ndio hapo sasa, alisema kuhusu 2025 wasubiri mpaka huko baadae
Huyu bibi ni mpumbavu sana, kosa aliyofanya Magu ni kumuamini huyu nyoka na kosa kubwa alilofanya ni kusema hadharani ni kusema wenye umri mkubwa hatawapitisha. Mama akaona plan yake inaenda kufeli wakafanya waliofanya
 
samiapiccc

Rais Samia Suluhu Hassan

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wanawake watamuweka madarakani rais mwanamke mwaka 2025.

Samia aliapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli. Kabla ya kupokea kijiti hicho, Samia alikuwa makamu wa Rais wa Tanzania.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais akifia madarakani, makamu wa Rais huapishwa kuwa Rais.

“Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia.

Wanawake bado hatujaweka Rais mwanamke, rais huyu amekaa kwa sababu ya kudra ya Mungu na matakwa ya katiba, tulichochangia sisi na dada zetu na mama zetu ni ile kusukuma hadi mwanamke akawa makamu wa Rais ule ndio mchango mkubwa tulioufanya wanawake, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, " amesema kiongozi mkuu huyo wa nchi leo Septemba 15, 2021 alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya demokrasia dunia.

“Sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana tukimweka rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameaanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia."

ADVERTISEMENT

“Fadhila za Mungu zikija mikononi kwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu ndugu zangu wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hizi, wanawake tumefanaya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hizi, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hizi leo Mungu ametupa baraka mikononi tukiiachia Mungu atatulaani."
 
Lini halimshauri zilitulia , watanzania ni wezi na wavivu

USSR




Sikiliza hilo sakata shida zaidi sio huo ubadharifu tu; mkuu wa mkoa anatilia shaka miradi mingine inayojengwa huko.

Tarehe 20 mwezi August kaandika barua TAKUKURU wakamsaidie kuchunguza zabuni za ajabu ajabu na copy wizarani (barua ipo kwenye link yao ya halmashauri).

Mpaka leo TAKUKURU awajafika na waziri anakwambia yeye hana muda wa kuzunguka Tanzania nzima.

Imebidi mkuu wa mkoa aingie field mwenyewe jana kuchunguza jambo lingine hela iliyoenda majuzi kwa ujenzi wa zahanati ndio kakutana na ivyo vimbanga vya overpricing wakati kuna mkuu wa wilaya na mkurugenzi. Ingekuwa Magufuli kuna mtu hapo kesho hana kazi.

People don’t care.
 



Hii leo yaani huyu ndio waziri ambae unaweza muhurumia anajituma kweli kweli maskini.

Kila siku anapandisha watu kwenye makarandinga na kusimamisha watu kazi, ingekuwa Magufuli ungesikia anaagiza wizara iwachukulie hatua au kuwasimamisha kazi hao ma-engineer.

Mama yetu hana huo muda; hii nchi ni ngumu kutaka kugombea tena ni kuwapa watanzania shida.

Hiyo kazi mama aiwezi hii ni miezi sita tu.
 
Daah kufa kufaana, Janeth anamlikia mume, Hangaya anafurahia cheo..kubaabeki
 
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.


Alisema Rais Samia Suluhu


Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Hapa kazi ipo. Kiukweli Maza kakosea sana!!

Wanaume sasa tukae mkao kujuta. Kwenye Dibaji yu ya hii miezi 6 ya kwanza tumeona jinsi wanawake wanavyoula ..... No wonder anasema katiba isubiri ajenge uchumi. Uchumi anaoujenga ndiyo huu wa kumobilize wanaweke.......!!
 
Habari,

Muda mrefu nimekuwa nikitamani kuweka uzi hapa wa kumsifia dada huyu kwa uchapakazi wake mahiri na ufuatiliaji wa karibu katika utendaji wake ambao kusema ukweli ni wa kipekee sana.Baada ya kusikia minong'ono ya chini kuhusu mgombea mwanamke 2025 Nikakumbuka kwamba nilitamani kuweka uzi wa kuelezea kwa namna utendaji kazi wa Ummy Mwalimu ni wa kipekee,Ila kutokana na mambo kuwa mengi nilijikuta ninasahau,Lakini leo nimekumbuka baada ya kuona utabiri wa mgombea mwanamke 2025.

Ummy Ally Mwalimu ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala cha kisiasa. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015.

Ummy Mwalimu ameshika nafasi mbalimbali katika ulingo wa siasa. Mwaka 2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na mwaka 2014-2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mwaka 2015 alikuwa Naibu waziri wa Sheria na katiba, mwaka 2014/5 alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mazingira na mwaka 2010-2014 alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Pia Ummy Mwalimu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili (2010 hadi 2015 na mwaka 2015 hadi 2020) kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi kupitia Viti Maalum kwa Wanawake.

Mwaka 2007-2015 Ummy alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga na mwaka 2008 hadi 2015 alikuwa mjumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) Tanga. Mwalimu ameshika nafasi nyingi za uongozi katika chama na serikali.

Nitarejea kuendelea
 
ww ndugu hakuna 14 years usiongee usivyovijuaa ..katiba inasema atagombea awamu 3 endapo JPM angekuwa kaongoza nchi more than 3 years ...huyu mama kachukua nchi hata mwaka bado kwahyo atakuwa na vipindi 2 tu vyakuongoza nchi hii jumla miaka 9 na usheee
Nataka ujue sasa anaongoza akiwa sio mgombea!!..2025 atakua mgombea na 2030 pia atakua mgombea panapomajaliwa jumpa Itakua mingapi Ndugu msomi
 
namkubali sana Mama Samia.

Mungu kamtunuku vitu vikubwa viwili.

1.Hekima na

2. Busara kubwa sanaa.

Vitu hivyo viongozi wengi hawana au wanakuwa na kimoja kati ya hivyo ila Rais Mama Samia Katunukiwa vyote hivyo.
 
Back
Top Bottom