Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema wanaolipa kodi halisi Nchini ni Watu milioni mbili tu kati ya Watu milioni 65 ambapo amesema idadi hiyo ni ndogo sana hivyo amewataka Watanzania wengi zaidi walipe kodi ili kuchangia uchumi wa Taifa.
Rais Samia amesema hayo leo October 04,2024 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akiizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi.
“Kwa idadi yetu ya Watu, wanaolipa kodi halisi ni Watu wachache, ni Watu kama milioni mbili kati ya Watu milioni 65 sasa ukitoa Watoto na wengine ambao hawapaswi kukatwa kodi hatupungui labda milioni 37 ambao tunaweza kulipa kodi lakini wanaolipa kodi ni milioni mbili, sasa hii idadi ni ndogo, ni ndogo sana, ina maana Watu kidogo wanalipa kwa fursa ya kuwajenga Watu wengi hatuwezi kufika, lazima wote tuchangie kila Mtu kwa kiasi chake ili tuweze kufanya mengi.
Ubabe katika kukusanya Kodi
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna malalamiko kutoka kwa Wafanyabiashara wanaolalamikia weledi kutozingatiwa wakati wa kukusanya kodi ikiwemo matumizi ya nguvu, lugha zisizo na staha na ubabe kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali wanaohusika na utozaji kodi.
Akiongea leo October 04,2024 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi, Rais Samia amesema “Baadhi ya Wafanyabiashara wanalalamikia wingi wa kodi na tozo lakini pia viwango vya kodi kutokuwa rafiki na hii ni kawaida, unajua Mtu ana hiyari kwenda kulipa faini bila kulazimishwa mwenyewe kwasababu faini ni kodi inayotokana na kosa, kwahiyo Mtu analipa ili asiende Jela lakini kodi tunayoizungumzia hapa ni kodi inayotokana na kitu kizuri”
“Sasa Mtu anaona nimefanya biashara nimepata pesa yangu kisha nikaipe Serikali bure lakini anasahau huduma inayotolewa na Serikali kwake na mazingira iliyomjengea kuweza kufanya biashara na kupata faida, kwahiyo ni maumbile ya Binadamu kuona kulipa kodi ni adhabu kumbe kulipa faini ni adhabu na Watu wanakwenda haraka, kwahiyo tuna tatizo ndani ya Nchi, Wafanyabiashara wanaamini hali hii inachangia mianya ya rushwa”
“Kuna malalamiko ya weledi kutozingatiwa wakati wa kukusanya kodi, mfano matumizi ya nguvu, lugha zisizo na staha na ubabe kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali na baadhi ya biashara kutozwa kodi au tozo zinazoshabihiana na Taasisi zaidi ya moja kwahiyo hapa napo kuna mashakamashaka ambayo inatakiwa yakatazamwe”
PIA SOMA
- Nani anamdanganya Rais Samia kuwa kati ya Watanzania mil 65, ni milioni 2 tu wanaolipa kodi?
-Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya, kingi kinaingia mifukoni kwa Wa