ukinunua hata pipi ya mtoto au nepi za mtoto umesha changia kodi humo !
Hao wafanya biashara ni wakusanyaji tu wa kodi wanao fahamika 😳 !
Bidhaa zao wanazozalisha na wanazoziuza na hata huduma wanazozitoa zote wanaweka na gharama za kodi zao na mpaka faida watakayoipata itatoka kwa hao hao walaji wa hizo bidhaa na huduma wanazozitoa kwa hao walaji wa mwisho !
Maajabu ya tafsiri ya walipa kodi iliyowekwa na wanaoitwa wataalamu wa masuala ya kodi ni kwamba Eti yule mfanyabiashara anayekusanya mauzo kutoka kwa walaji ambayo yameshawekwa na kodi zote kwenye hizo bidhaa na kwenye huduma zote anahesabika yeye ndiye mlipa kodi 😂😂😅 !
Haya kwangu ni maajabu 😱 !