Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona kuna ubabe kuzuia maandamano si atumie Jeshi la Polisi kufuatilia kodi.Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema wanaolipa kodi halisi Nchini ni Watu milioni mbili tu kati ya Watu milioni 65 ambapo amesema idadi hiyo ni ndogo sana hivyo amewataka Watanzania wengi zaidi walipe kodi ili kuchangia uchumi wa Taifa.
Rais Samia amesema hayo leo October 04,2024 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akiizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi.
“Kwa idadi yetu ya Watu, wanaolipa kodi halisi ni Watu wachache, ni Watu kama milioni mbili kati ya Watu milioni 65 sasa ukitoa Watoto na wengine ambao hawapaswi kukatwa kodi hatupungui labda milioni 37 ambao tunaweza kulipa kodi lakini wanaolipa kodi ni milioni mbili, sasa hii idadi ni ndogo, ni ndogo sana, ina maana Watu kidogo wanalipa kwa fursa ya kuwajenga Watu wengi hatuwezi kufika, lazima wote tuchangie kila Mtu kwa kiasi chake ili tuweze kufanya mengi.
Ubabe katika kukusanya Kodi
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna malalamiko kutoka kwa Wafanyabiashara wanaolalamikia weledi kutozingatiwa wakati wa kukusanya kodi ikiwemo matumizi ya nguvu, lugha zisizo na staha na ubabe kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali wanaohusika na utozaji kodi.
Akiongea leo October 04,2024 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi, Rais Samia amesema “Baadhi ya Wafanyabiashara wanalalamikia wingi wa kodi na tozo lakini pia viwango vya kodi kutokuwa rafiki na hii ni kawaida, unajua Mtu ana hiyari kwenda kulipa faini bila kulazimishwa mwenyewe kwasababu faini ni kodi inayotokana na kosa, kwahiyo Mtu analipa ili asiende Jela lakini kodi tunayoizungumzia hapa ni kodi inayotokana na kitu kizuri”
“Sasa Mtu anaona nimefanya biashara nimepata pesa yangu kisha nikaipe Serikali bure lakini anasahau huduma inayotolewa na Serikali kwake na mazingira iliyomjengea kuweza kufanya biashara na kupata faida, kwahiyo ni maumbile ya Binadamu kuona kulipa kodi ni adhabu kumbe kulipa faini ni adhabu na Watu wanakwenda haraka, kwahiyo tuna tatizo ndani ya Nchi, Wafanyabiashara wanaamini hali hii inachangia mianya ya rushwa”
“Kuna malalamiko ya weledi kutozingatiwa wakati wa kukusanya kodi, mfano matumizi ya nguvu, lugha zisizo na staha na ubabe kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali na baadhi ya biashara kutozwa kodi au tozo zinazoshabihiana na Taasisi zaidi ya moja kwahiyo hapa napo kuna mashakamashaka ambayo inatakiwa yakatazamwe”
PIA SOMA
- Nani anamdanganya Rais Samia kuwa kati ya Watanzania mil 65, ni milioni 2 tu wanaolipa kodi?
-Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya, kingi kinaingia mifukoni kwa Wa
Magufuli ndo aliweka utaratibu wwnye akili af tukaona hafai tukamwondoa harakaNjia pekee ya kuongeza tax base kwa kiasi kikubwa ni kupiga marufuku umachinga rasmi, kila mjasiriamali (mkubwa au mdogo) awe na business license na tax ID number
Aliondolewa kivipi mkuu ?Magufuli ndo aliweka utaratibu wwnye akili af tukaona hafai tukamwondoa haraka
Hivyo ndivyo ChoiceVariable anavyoamini!Tozo tunazo katwa kwenye unit za umene sio kodi n sadaka?
Sijui anamaanisha kitu gani anaposema ni “Watu milioni 2 tu ndo wanaolipa kodi”Nimeshindwa kumuelewa Rais anaposema nchi ina watu milioni 65 ila wanaolipa kodi ni watu milioni 2 tu!
Najiuliza sipati jibu!
Anataka WENDAWAZIMU, VICHAA, WASIO NA KAZI, WATOTO, VICHANGA walipe kodi!
Kwamba kila Mtanzania hata akizaliwa leo anatakiwa kulipa kodi1😅😅😅
Kodi ni nyingi mno. Binafsi kila mwezi nailipa serikali mamilioni mengi tu kutokana na huo utitiri wa kodi. Ndo maana sishangai kama mtu akitafuta upenyo wa kukwepa kodi.Kuna
1. Tax (Kodi)
2. Charges (Tozo)
3. Levy (Ushuru)
Watu hawalipi kodi kwasababu charges na levy ni nyingi sana sasa ukiongeza na kulipa kodi ni sawa hiyo kazi unaifanyia serikali na mwenye nyumba labda na maonesho kwamba unaamka asubuhi nawe una mahali unakwenda kushinda basi. Ndio maana watu wana opt wasilipe/wakwepe kodi.
Ushauri japo najua hauwezi fanyiwa kazi. Chagueni kufuta kodi zibaki charges and levy au zifutwe charges and levy ibaki kodi then boom 💥 muujiza makusanyo yataongezeka achana na maigizo ya sasa ya TRA.
Kukatwa Kodi haimaanishi wewe ni mlipa Kodi.Kama huna TIN wewe sio mlipakodi.Tozo tunazo katwa kwenye unit za umene sio kodi n sadaka?
Sasa wewe unatakaje sasa? Ili iweje?wazee wa kuuza mzigo wa milioni risiti ya yaki nne wamulikwe
Rais ameongea utafiti, so inabidi akosolewe kwa tafiti sio kwa threads za JF. Leta utafiti wako wenye orodha ya walipa kodi zaidi ya milioni mbili.Nani anamwandikia Rais hizi Hotuba? Kweli anasema nchi nzima walipa kodi ni Milion 2 tu? Kweli? Au anamaanisha kuna watu wanaenda kwenye kadirisha flani wanalipa kodi wanapewa receipt wanarudi kwao?
View attachment 3116429