Rais Samia: Wanaolipa kodi Tanzania ni milioni 2 tu

Atuonyeshe mfano, kodi inalipwaje, yeye na ccm wenzie.
 
Apunguze matumizi serikalini!
SGR ipo, watumishi serikalini waitumie vyema tena waende na Economy class. Masafari yasioeleweka futa kule. Yeye naye ajimulike msafara wake ni kufuru!
Bado mianja ya udokozi ipo! Hela zinapigwa bila huruma!
 
Mbona kuna ubabe kuzuia maandamano si atumie Jeshi la Polisi kufuatilia kodi.
 
Kila mtanzania anaelipia huduma analipa kodi lakini inaonekana haitoshi kwa sababu ya matumizi ya hovyo na anasa za waliopewa nafasi pamoja na wizi uliokithili ndio maana tra kila siku wanasema wamevunja rekodi ya ukusanyaji lakini kasi ya kukopa haipungui tuu
 
Njia pekee ya kuongeza tax base kwa kiasi kikubwa ni kupiga marufuku umachinga rasmi, kila mjasiriamali (mkubwa au mdogo) awe na business license na tax ID number
Magufuli ndo aliweka utaratibu wwnye akili af tukaona hafai tukamwondoa haraka
 
Huko tra kuna mambo ya kipuuzi Sana sometimes. Niliwahi fungua biashara na niliamua kua muaminifu kwa kulipa Kodi lakini Kodi niliyokadiliwa ni kubwa na inalingana na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa Sana Wakati Mimi nina mtaji wa milioni mbili tu.

Biashara ikafirisika nikaamua kufunga. Sasa ole wako ununue ardhi kwa mtu halafu unataka kufanya transfer nenda huko tra ukalipe kodi wanavyosumbua utadhani hawataki hiyo kodi
 
Sijui anamaanisha kitu gani anaposema ni “Watu milioni 2 tu ndo wanaolipa kodi”

Je kwenye hao watu ni makampuni pamoja na biashara zote ambazo zimesajiliwa? Je ni pamoja na individual taxes?

Kauli hiyo iko vague kidogo kueleweka na wananchi wa kawaida.

Kwasababu kodi zenyewe ziko tofauti. Kuna “direct and indirect taxes” nk

Biashara zote zinatakiwa kuwa na leseni. Sasa wanashindwaje kujuwa kama siyo mfumo ambao umeweka mianya inayoleta udhaifu?

Hao anaowataka walipe kodi ni watu ambao wana biashara halafu hawalipi kodi?

Maana hii kauli yake kama ndo anavyoongea na Mwigulu Nchemba, siwezi kushangaa tozo zikaongezeka ili kuweza kupata “watu wengi zaidi wanaolipa kodi”

🤦🏾‍♂️
 
Kodi ni nyingi mno. Binafsi kila mwezi nailipa serikali mamilioni mengi tu kutokana na huo utitiri wa kodi. Ndo maana sishangai kama mtu akitafuta upenyo wa kukwepa kodi.

Mfano hiyo service levy ni mauwaji.
 
Shida siyo kulipa kodi.shida ni kwamba hakuna uezeshwaji Kwa walipa Kodi Ili wakupe Kodi directly.asilimia kubwa ya wafanyabiasha hawalipi kodi au kulipisha kodi.watu wengi hawaoni umuhimu wa kulipa Kodi kwa sababu haoni faida ya kulipa Kodi kwa sababu haoni kama Serikali inamsaidiaje kukuza kipato Cha mlipa Kodi.
 
Nani anamwandikia Rais hizi Hotuba? Kweli anasema nchi nzima walipa kodi ni Milion 2 tu? Kweli? Au anamaanisha kuna watu wanaenda kwenye kadirisha flani wanalipa kodi wanapewa receipt wanarudi kwao?

 
Registered tax payers, Walikuwa ml 4, wamepungua Hadi ml 2.

Hapo hapo TRA imekusanya Trillion 3 ndani ya miezi 3 ikidai imevunja rekodi zote za makusanyo.

Hili Giza nchini petu soon litapita na KUTAPAMBAZUKA!!

Naipenda sana Nchi yangu nzuri, tajiri TANZANIA 🇹🇿

Amen.
 
Nani anamwandikia Rais hizi Hotuba? Kweli anasema nchi nzima walipa kodi ni Milion 2 tu? Kweli? Au anamaanisha kuna watu wanaenda kwenye kadirisha flani wanalipa kodi wanapewa receipt wanarudi kwao?

View attachment 3116429
Rais ameongea utafiti, so inabidi akosolewe kwa tafiti sio kwa threads za JF. Leta utafiti wako wenye orodha ya walipa kodi zaidi ya milioni mbili.

Ova
 
Mbona yapo mazingira ambayo hayapo katika mfumo wa biashara lakini yametengenezwa system ya kodi?

Kwa hiyo zile buku jero za kila mwisho wa mwezi tunazokatwa kwenye Luku sio sehemu ya kodi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…