Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Manyara katika Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Kwaraa leo tarehe 23 Novemba, 2022
SEHEMU YA HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, SAMIA SULUHU HASSAN
Kilimo, Mabadiliko ya tabianchi na Migogoro ya Ardhi
Babati ni mkoa wa kilimo, ni mkoa unaolima mazao mengi. Niwaombe sana wananchi kuendeleza jitihada za kilimo. Nasi kama serikali tupo nyuma yenu.
Miaka ijayo dunia inaona baalaa la njaa, Tanzania hatuna sababu ya kulia kwa njaa. Tuweke akiba ya kutosha, lakini pia tuwauzie ndugu zetu. Tuongeze jitihada kwenye kilimo.
Nawaomba sana mpunguze migogoro baina ya watu na watu, kuba vitendo vya kuchukua sheria mkononi kati ya mtu na mtu, hasa wakulima na wafugaji. Nawaomba sana mpunguze tabia ya kuchukua sheria mkononi.
Tunashuhudia mabadiliko ya hali ya hewa, tutunze mazingira, turudi kupanda miti na ile iliyopo kwa namna yoyote ile tuache kuikata. Tunashuhudia maziwa yetu kuanza kupungua maji, na yanapojaa husogea hadi makazi ya maji. Wanamazingira, twendeni kushughulikia mazingira yetu.
Swala la mogogoro ya ardhi, nataka nizungumze na wanasiasa. Nasi tusichochee mogogoro, kwasababu wananchi wanapokuwa wanavamia maeneo, wanasiasa hatuwaambii watu ukweli, tunawangalia wakivamia. Na badala yake tunakuja kusimama kutetea wavamizi wa maeneo yale, tunaharibu mipango ya matumizi ya ardhi, tunawachochea waingie lengo uje kupata kura huko baadae, wasikione wewe ni mbaya. unajua kwamba wamevamia na kubaribi mipango ya matumizi ya ardhi, unasimama kutetea ili upate kura.
Niwaombe sana wanasiasa, simameni na Serikali yenu, tupange matumizi bora ya ardhi, kila mwananchi apate ardhi ya kutumia, anayefuga afuge, lakini tusichochee wananchi kwenda kuvamia maeneo ambayo hayakupangwa kwa matumizi hayo ambayo hayakupangwa.
Tusichochee migogoro kwa sababu kwanza migogoro sababu inapoteza muda mwingi lakini pia linatuchelewesha kwenye maendeleo.
Ukatili wa Kijinsia
Nilipokea ripoti iliyotengenezwa mwaka jana lakini ofisini kwangu imengia mwaka huu. Kwa ujumla, mkoa huu wa manyara una kesi 3641. La kusikitisha zaidi kesi ni nyingi, kama 792 ni mashambulio ya kimwili, wenye nguvu wanawashambulia wasio na nguvu.
Lakini kesi 708 ni kesi za unyanyasaji wa watoto kingono, siyo kijinsia, Ki ngono. Hii siyo rekodi nzuri, wala siyo sifa kwa mkoa wetu. Niwaombe watu wote wanaohusika na hili, majaji, watu wote kwenyr halmashauri zetu, watu wa maendeleo ya jamii, watu wa ustawi wa jamii, kulisimamia hili. Kutoa elimu ya kutosha, manyara inabadilika kimaendeleo, tubadilikeni pia kitabia. Naomba sana tubadilike kwenye hilo.
Usajili wa Wakulima
Tumeleta usajili wa wakulima tutambue mkulima gani yupo wapi, namba yake ni hii ili zinapokuja huduma za wakulima tujue tuna wakulima wangapi, kwenye eneo gani, wanahitaji huduma zipi.
Lakini napata tetesi mmavunjwa moyo kujisajili na kwamba mnaambiwa ukisajiliwa tu TRA hawa hapo wanakuja kukusanya kodi. Si kweli, usajili huu ni kwa faida yenu, si kwa ajili ya kulipa kodi. Nendeni mkajisajili, vinginevyo zitakuja huduma kwa wakulima mbakie mnalalamika kwamba hamkupata kumbe haupo kwenye daftari la wakulima.
Mfumo mpya wa Mita za maji
Kuna masikitiko ya bei za maji, tunakuja na suluhu, siyo suluhu mimi, suluhu ya kutatua tatizo. Ya kwamba tunachotaka, mita za maji za kununua, unafungiwa mita yako unanunua maji kwa mita, unacholipa ndiyo huduma utakayopata. Pesa yako ikikatika na maji yanakatika, hiyo itakuwa haina malalmiko.
Lakini uwezo wetu wa kusambaza mita hizo nchi nzima bado haujawa mkubwa. Niwaombe sana lipeni bili za maji zinazokuja.