#COVID19 Rais Samia: Wanawake wengi waliambukizwa Uviko-19, walibeba mzigo mkubwa

#COVID19 Rais Samia: Wanawake wengi waliambukizwa Uviko-19, walibeba mzigo mkubwa

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho ya 'Siku ya Wanawake Duniani', Zanzibar, hivi ni baadhi ya kauli zake:

"Tunajua kwamba wanawake wengi wanajishughulisha na biashara ndogondogo ambazo hazipo kisheria na hazina kanuni, na sasa tunataka kwenda kurasimisha eneo hili ambayo ni sekta isiyo rasmi.

"Kama tulivyoagizwa na lengo namba nne katika malengo ya millenia kuhusu elimu, tumeendele kuhakikisha tunatoa fursa ya elimu ikiwemo kuwarudisha shuleni wale wote waliokatisha masomo.

"Tunakwenda kuweka mitaji kila mkoa, tumeshalifanyia kazi suala la mitaji na benki za CRDB na NMB zimekubali. Na huu mtaji sio mgao ni mkopo maalum kwa wanawake mbali na ile mikopo ya halmashauri.

"Wanawake walibeba mzigo mkubwa kipindi cha ugonjwa wa Uviko-19, kwani wengi waliambukizwa, waliuguza na hata wengine walipoteza uhai.

"Kama kweli suala la ukatili wa kijinsia linatukera sisi wanawake basi tutalifanyia kazi, Wanawake tutasimama imara kwa serikali zetu zote mbili zielewe kuq sulaa hili linatuudhi na tutaonesha njia.

"Tanzania na dunia kwa ujumla inakabaliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi, waathirika wakuu kabisa katika athari za mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake.

"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumefanya mabadiliko ya sera ya Mazingira mwaka jana na kuongeza suala la mabadiliko ya tabia nchi, mabadiliko ambayo hayakuwepo katika sera hiyo mwaka 2014.”

Source: DarMpya
 
Ukosefo wa Ujira, Umasikini, Uwiano Mbovu wa Keki ya Taifa..., Sera Mbovu na Watu waliopo Madarakani kutokuwajibika (au kula zaidi ya urefu wa kamba zao) ilibebesha, inabebesha na itazidi kubebesha mzigo hawa baadhi ya kina mama kuliko hata huo UVIKO
 
Huu ubaguzi utakuja kumtafuna huyu bibi, wanaompa kiburi atambe ni wanaume, kama wanawake ni jeshi kubwa kwanini JWTZ asilindwe na wanawake wenzake?
 
Huyo ndio aliungana na jiwe kusema Corona haipo!!

Sorry madam president I'm not boarding.
 
Back
Top Bottom