kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Rais Samia Suluhu amesema hayo wakati aliposhiriki tamasha la utamaduni la Buyalo mkoani Mwanza. Rais Samia Suluhu aliwasisitizia wakulima kuhifadhi chakula ili kiweze kuwasaidia wakati wa uhaba wa chakula. Aidha aliwatania wasukuma kwa kuwaambia wanapoongeza familia akumbuke kuongeza na mashamba ya chakula.
"Ndugu zangu wasukuma mavuno haya tukishauza na bei sasa ziko nzuri, akina baba tutakimbilia kuongeza nyumba za 2, mwenye 2 anakwenda kwenye ya 3, si vibaya hatuna wivu, mnapokumbuka kuongeza nyumba mkumbuke kuongeza na mashamba" -Rais Samia Suluhu