Rais Samia: Wasukuma mnapoongeza wake muongeze na mashamba

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Rais Samia Suluhu amesema hayo wakati aliposhiriki tamasha la utamaduni la Buyalo mkoani Mwanza. Rais Samia Suluhu aliwasisitizia wakulima kuhifadhi chakula ili kiweze kuwasaidia wakati wa uhaba wa chakula. Aidha aliwatania wasukuma kwa kuwaambia wanapoongeza familia akumbuke kuongeza na mashamba ya chakula.

"Ndugu zangu wasukuma mavuno haya tukishauza na bei sasa ziko nzuri, akina baba tutakimbilia kuongeza nyumba za 2, mwenye 2 anakwenda kwenye ya 3, si vibaya hatuna wivu, mnapokumbuka kuongeza nyumba mkumbuke kuongeza na mashamba" -Rais Samia Suluhu

 
Tatizo hifadhi..,
 
Chawa wa mama hapo mbona hawasemi ubaguzi wa kikabila au ubara?
 
Asitupangie maisha yeye kwanza apunguze gharama za kwenda uarabuni zmetugharimu sana
 
Naweka ndani mtoto mbichi wa 3 aliyehitimu la saba mwaka jana. Karibuni ntuzu mwezi Julai mle ubwabwa.🍺🍻🍻. Mahari ishatoka ng'ombe 22 sondeka!😂

Haya turudi kwenye mambo ya msingi.

TUNATAKA BANDARI YETU
 
Anayeandaa hotuba ya maza bora apangiwe kazi nyingine.

Gharama Za Maza kwenda mwanza na msafara wake na kilichoandikwa kwenye hotuba hakina value for money.
 

Attachments

  • FAC1266F-4108-450D-BBFE-68FE3B4EE738.jpeg
    47.8 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…