Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kutoa Ushirikiano kwa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, maarufu kama Tume ya Jaji Lila.Amesema hayo leo Ahosti 7, 2026 katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Tume hiyo iliyofanyika leo Agosti 7, 2026 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
"Katika hili niwasihi sana Watanzania wote kutoa ushirikiano unaohitajika na Tume katika kutekeleza majukumu yao. Niwasihi sana Watanzania tuisaidie Tume hii iweze kufanya kazi yake na tusiisumbue katika kufanya kazi zake"