DOKEZO Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kitaeleweka tu,baadhi ya watu wanajuaga mwanajeshi hasumbuliwi na kikokotoo... Kitaeleweka tu,mtaani kugumu sana,wajiwekezage.Hakuna vita siku hizi,vyakusema yawezekana nikafa muda wowote kwahiyo ninywe pombe na niwatumie wanawake tu,maana muda wowote naweza nikafa... hakuna hicho siku hizi,mtafanya kazi,mtastaafu,mje huku tuliko mkione cha moto.Jiwekezeni.
 
Kuna baadhi ya wastaafu wa kada za askari ukiona maisha wanayoishi utawahurumia , ni kama vile kazi waliyokuwa wanafanya iko na laana
 
Ni huzuni kwa kweli, watu wa vyeo vya chini wanatumika kukandamiza haki za wananchi na CCM, halafu wakistaafu wanaachwa kama takataka!
 
Wajiwekeze vip na wanadai haki yao..

Kwamba kutumikia taifa sio kujiwekeza?

Sasa mtu kafanya kazi miaka 30 anaambiwa alikuwa kibarua, wewe inakuingia akilini?

Unadhani Mwanajeshi wa kawaida anaweza jiwekeza kwenye nini cha kumpa fedha uzeeni?
Embu jaribu ku feel hiyo gap.
 
Madhara ya kuibeba CCM ndiyo haya,wananchi wakitakakufanya mabadiliko mnakuwa wa kwanza kujaza kura fake kwenye maboksi ya kupigia kura na kuwapiga wananchi kwa mabomu,matokeo yake wananchi wanalia na wabeba CCM nao wanaomboleza kivyao.
 
pindueni meza... hamtaki mnajiona nyie ndo mnafaidi mema ya nchi! angalia sasa mmetelekezwa!
 
Ni aibu kwa askari kuilalamikia serikali ambayo pasipo ninyi haiwezi kuwa hapo.

Sisi raia tumedhuliwa sana, tuna hela zetu LAPF na NSSF na hatuwezi kuzitoa
 
Acha mlie tu na Saa 100 asiwasaidie lolote. Miaka yote mmewalinda watesi wetu, wadhulumu wetu, wezi wa kura ili wabaki madarakani. Sasa yamewatokea puani mnalalamika. Mliapa kulinda katiba ya JMT, mmewahi kusimamia hilo?
Baba zetu walikua watumishi pia na wamestaaf na hela kiduchu kutokana na sera mbovu za CCM ambayo nyie masikini wenzetu mlikua mkiwalinda na kututisha.
Au mmesahau Mkapa alivyowapeleka wajeda kule Unguja na Pemba?
Mmesahau.
 
Hivi hawa wazee walipata stahiki zao?
 

Yaani mimi ndiyo JK WA JAMII FORUMS - "Moderator weka mambo hapo" 😂
 
Nakaaga najiuliza Waalimu na wanausalama wao ndio hua msaada mkubwa sana kipindi cha uchaguzi ila cha ajabu wao ndio wanasahaulika😂😂😂 au ndio yale yasemwayo malipo ni hapa hapa duniani. Imagine mtu anaomba hakinyake aliyowekeza kwa muda wote aliofanya kazi na anapangiwa apateje stahiki yake. Muda mwingine afe hajapata na watoto zake wasiipate. Wanajeshi mkiona hamsikilizwi kuomba ni unyonge nadhani mnajua nn cha kufanya.
 
Wasaidiwe
 
Poleni sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Wanatakiwa kuchukua hatua nao tuko nao tunalalamika?

Kwisha habari yetu. Nyie Makamanda wastaafu hata sitawapa pole kuleni za uso tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…