Katika hali ya utani, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wazo lililotolewa na wachekeshaji la kucheza mchezo wa ‘upatu’ linaweza kuwa zuri endapo likibadilishwa na kutafutiwa namna bora ili kusaidia masuala ya kifedha ya nchi za Kiafrika.
Rais Samia amesema wazo hilo likichukuliwa kitofauti litakuwa na mchango wa kujitegemea kifedha, kama wakikubaliana na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuunda mfuko wao.