Rais Samia weka Tanzania mbele, mbona mwenzako Ruto ameweza!

Kwani Kila Kiongozi ananunuliwa V8? Hizo ni chache Kwa viongozi wa ngazi ya Mkoa kwenda Juu.

Unadhani zisiponuniliwa ndio maisha yatakuwa Mazuri? Maana hata bil.100 hazifiki.
Hua nakuheshimu sana Mkuu lakini hata kama ni uchawa sasa umefika kwenye ukunguni kabisa... yaani ung'ang'anizi wa hoja...

Hukupaswa kabisa kutetea hoja ya viongozi kununua magari ya kifahari wakati maelfu kwa mamilioni ya watanzania wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya. Hiyo bilioni 100 ni pesa ndogo??? Inamaana hazitoshi kufanya jambo?? Leo Trump amekata misaada ya "kiafya" kwa Tanzania... Je ulijipanga kwa hilo??? Hizo bilioni 100 ambaomzo unaona chache zisingefanya jambo??? Kama nchi toka zamani ingeacha utegemezi wa namna hii na kuweka mikakati ya kujitegemea unadhani hizo bilioni 100 zisingefaa kitu???

Mkuu think before post!!
 
Huyo muache hivyo hivyo mkuu hana data za kumtosha yeye mwenyewe atakupa data gani za kukusaidia wewe?
 
Hoja Haina mashiko,hata magari waliokuwa wanatumia kina Nyerere Yale unajua bei yake na ulaji wa Mafuta ulivyo?

Hiyo hoja yenu ni ya kijinga Kwa sababu hayo.magari hununuliwa Kwa viongozi kuanzia RC/RAS kwenda Juu sio chini ya hapo ambapo ndio Kuna Watendaji wengi.
 
Unaleta stori za kuuza? Hapo hapana data ila Kuna taarifa,ndio kwanza Mradi wa Taza grid interconnectivity uko kwenye ujenzi .

Hakuna tunaemuuzia umeme ila tunanunua,hujui kitu wewe nyumbu.
Wewe wale wanaonunua umeme kwa unit 1 290 unawajua au huwajui?
 
Sawa
 
Umeibuka na ushindi Mkuu. Hapa ntapoteza muda kabisa... 🤔🤔Stick to it🫡🫡
 

Sijasema ufisadi umeanza na Samia. Nimesema serikali ni wabinafsi waliopita na waliopo. Hakuna sababu kwanini Raisi Samia anafumbia macho ufisadi na kuwachekea chekea mafisadi kila siku. Yaani ni maajabu kwa watu wanajifanya wazalendo halafu wanaiba kura kwa wananchi ambao wanaomba kuwaongoza. Hakuna uzalendo wa aina hiyo. Lakini hata wanao watetea na kujua wazi ukweli huu ni tatizo kwa nchi yetu na hawasaidii nchi bali ni maadui wa kubwa. Hakuna kitu Nyere alichukia kama rushwa.

Sheria wanajitungia kila siku kujipa mafao wa wenza wao. Mimi binafsi nina habari kubwa za ufisadi wa mkwe wa Raisi ambaye ni waziri TAMISEMI iko siko nitaotoa hapa. Akibiasha tutampa voice note na video
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…