mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Kwa baadhi ya mambo, Mama huchukua hatua sio kwa kusukumwa na dhamira njema, bali husukmwa na nafsi ya ngoja niwaonyeshe/nimuonyeshe mimi ni nani au si anajifanya/wanajifanya wajanja ngoja sasa niwaonyeshe.
Kwa kifupi, Mama akihisi(hata kimakosa) kuwa anadharauliwa, watu wanampanda kichwani au anagombanishwa na wananchi, anajenga chuki na kisasi na utaona mtu au watu fulani wanashughulikiwa kitu ambacho sio sahihi.
Kwa kifupi, unaweza fanya mambo ya hovyo ila kama anaamini unamuheshima, basi utabaki salama.
Halikadhalika, unaware kuwa unafanya jambo jema ila kama atahisi unamdharau, unam-pressurize,n.k, ataagiza au atabariki ushughulikiwe.
Kwa maneno mengine, hana au amekosa standard katika utendaji wake(sio mtu wa principle).
Hiki ndio kimemgharimu Kamanda wa Anga ingawa hakuwa na kosa(udhaifu wa Mama unahusika), na ndio sasa kinaanza kuwagharimu kundi la Mwendazake wanaomlinganisha na Mwendazake kwa style ya kuonyesha kuwa Mama hatoshi..
Hata hii vita anayoianzisha sasa ni baada ya kuona aliowalinda ama hawana shukurani au wanataka kumgombanisha na wananchi kuwa hayuko serious vinginevyo wasingeguswa.
Mnaweza msinielewa, ila muda utawasaidia kumuelewa
Nionavyo mimi, kama umekubali kufanya nae kazi Kumheshimu ni jambo moja la lazima litakalokuwezesha kufanya nae kazi na kumshauri kwa yale unayoona yanahitaji ushauri
Ukishamdharau atajua na lazima akushushughulikie maana wewe humfai wala hujawa msaada kwake