Hiki kilio sio cha wakulima bali madalali na walanguzi,wakulima chakula washamaliza kuuza tokea mwaka jana, sasa hivi wapo mashambani wanalima.
Tatizo la nchi za kiafrika ni kwamba mbumbumbu ndiyo wanakaa mstari wa mbele kushauri.
kilimo kina kitu kinaitwa "chain of production"
hiyo chain inajumuisha wakulima, viwanda vinavyochakata mazao ya wakulima, wachuuzi wa jumla, wachuuzi wa reja reja mpaka kumfikia mkulima.
ukitazama katika chain hiyo mkulima wa Tanzania hana storage, kuna watu wa kati ndo wenye storage. mabadiriko ya bei yanatokea kutoka kwa mlaji wa mwisho.
watu wenye storage ndiyo waathirika wa kwanza kuathirika na bei. kama ni bei kuporomoka sokoni wao wanakuwa washanunua na kuweka kwenye maghala na ndiyo wa kwanza kupata hasara.
kama ni bei kupanda wao wanakuwa washanunua na ndiyo wa kwanza kupata faida.
lakini hawa watu wanapoathirika athari kwao hurudi mpaka kwa mkulima mwanzo. wakipata hasara wakulima wakitaka kuuza lazima bei watakuta mbaya.
na kama wakipata faida basi mkulima naye anapata faida anapokuja kuuza.
hii mifumo inajiregulate labda serikali iweke ukiritimba wa kuwazuia watu na kuwapa exclusive watu.
mfano kama bei ya mahindi dar ikiwa 1,200, na songea ni 500. watu wengi watasafiri kwenda songea kutafuta mahindi.
ila mtu akiona kufuata mahindi bei ni ile ile kama kununua kwa anayeleta kwa jumla hana haja na ataendelea kutumia watu wa kati. dhana ya kwamba watu wa kati ndiyo wanafaidika ni dhana potofu.
tukikuza kilimo, tunaweza kutoa elimu kwa wakulima kujenga vienge, kuwapatia mikopo ili vitu kama shule za watoto zisiwape presha ya kuuza mapema kwa hasara.
tukihakikisha kiasi kizuri cha pesa kinazunguka kwenye sekita ya kilimo. nchi itapiga hatua kubwa.