Rais si mkweli, Mawaziri si wakweli, Mkuu wa jeshi, mkuu wa polisi na polisi wake SI WAKWELI.

Hahahahaaaaaaaah!! Tena wakati naingia madarakani sukari ilikuwa elfu 5, kwahiyo aliteleza hata kuingia madarakani? Pascal Pascal unapotea kidogi kidogo!?
 
Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa uliogharimu zaidi ya bilioni 45 kule wilayani Chato unauzungumziaje huo uwanja nini athari yake kiuchumi kama taifa?
 
Jeshi hili lenye obsolete equipments kama ndege za mwaka 1965 za shenyang J-6 na J-7 ambazo hazitumiki tena duniani zipo kwenye museum, au helicopters (Eurocopters, bells)ambazo siyo "gunship" kwa strength tupo namba 98 na 99 kwa ubora, level moja na Sudan kusini, tumeshindwa na majirani zetu isipokuwa Burundi tu. (mmmh aisee hiii paragraph imenichekesha sana duuh!!
 
Kama angekuwa mkweli angekili kuwa ni yeye aliyeamuru Ben sa8 auawe, tl ashambuliwe nk.
 
sidhani kama kuna watu waongo hapa nchini kama wanasiasa wa upinzani, waliwahi kutuambia Lowasa ni fisadi baada ya hapo wakabadili angani wakaja na hadithi kuwa lowasa sio fisadi na wakamteua kuwa mgombea wao kwa nafasi ya Urais.
 
Mkuu, hapo kwenye sukari huenda alisema ukweli, si unajua wao hua hawanunui chochote, hununuliwa kila kitu na serikali/sisi so huenda alikua hajui bei ya sukari kabla na baada, this is why!
 
Ahsante sana Paschal kwa maoni. Nilivyosoma andiko lako kidogo ilinishangaza nikajiuliza hivi ni huyu Paschal ninayemfahamu au mtu ame-hack jina lako na password yako au jana jumapili ulitoka happy hour ukachoka kidogo...Hizo ni assumptions zangu tu. Nisamehe kwa mawazo yangu.
(A) Kuhusu pointi yako namba moja ambayo unapingana nayo,
World Bank & African Development Bank wanahusika kufanya overview ya uchumi wote (Micro and Macro) Angalia Tanzania economy outlook ya mwaka 2018 inaonyesha uchumi unakua kwa 6.8% kwenye quarter hii ya mwisho uchumi utakua kwa asilimia 6.5. Kwa sisi watanzania uchumi unakuwa projected na BOT na NBS( National Bureau of Statistics) siyo TBS (Hii ni Tanzania Bureau of Standards ambayo ina kazi nyingine kabisa), Hawa wetu walikazania au walisisitiza kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7.2 na ukipungua utakuwa kwa 7.1% Kimsingi waling'ang'ania kwenye "Status quo" na baada ya kupewa maelekezo kuwa wafanye hivyo (Ninayo hakika na ninayoyasema) au kesho yake watumbuliwe (Unakumbuka yaliyowatokea Ephraim Mafuru na Dr. Mwale Malecela?) Situngi hayo Bw. Paschal...Tukikutana siku moja tutaongea nina imani utanielewa. Niliongea na mkubwa wa Benki ya Dunia mwezi wa August akawa frustrated na jinsi hizo organisation zetu mbili kubwa zinazohusika kufanya overview ya uchumi yanavyofanya kazi.....Alisema "These projections are absolutely a lie" ukuaji wetu wa uchumi upo upande mmoja tu kwenye infrastructure development na utalii kwenye madini na kilimo kumeshuka sana....Hata hiyo 6.8% imekuwa buoyed na Infrastructure, kama tumekopa hizo pesa basi baada ya muda tutakuwa na nakisi kubwa ambayo tutapata shida kuweza kui-offset ukiongeza na hiyo misaada tunayoanza kunyimwa Nakisi lazima iongezeke.
(B) Pointi yako ya kutaka kusema hiyo issue ni ya kijinai na kama nafahamu nikaripoti polisi, hiyo imekosa substance na wewe unalijua hilo..Nikaripoti kwa polisi wa nchi ganii? Mbona hunitakii mema......au na wewe ni katika wale wale jamaa wanaopoteza watu...Hujaona waandishi wenzako wawili wa CPJ waliulizia kuhusu mwandishi mwenzao, walifanywa nini? Hadi dunia nzima ikapiga kelele ndiyo wakaachiwa...sina haja ya kuongelea hilo. Sidhani kama upo out of touch na haya yanayotokea au una sympathy na Msukuma mwenzio? Waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba!
Mbona Makonda aliripotiwa na Meya wa Ubungo Mr. Boniface je hiyo kesi ina mwaka na nusu nini kimefanyika zaidi ya Meya Boniface kupewa vitisho na kunyanyaswa..Makonda amechukuliwa hatua kwa vyeti alivyofoji??? Wewe ni mtu mzima mwenye akili timamu na unaelewa hali ya nchi yetu...Serikali yetu ni double standard, mwizi anamuua raia mwema (very hypocrite government) au hulioni hilo pia? Hata kipofu au kiziwi lazima alione hilo.
Paschal watu wanaogopa hata kwenda kupiga kura wanashikwa kwa just petty issues...au unabisha na hilo haijawahi kutokea wapiga kura wanajitokeza 20% ya waliojiandikisha...wanaogopa nchi imeshakuwa mbaya ni kwamba hawajatangaza Curfew tu.Nchi imeshakuwa mbaya, wewe upo immune kwa sababu ya jina lako.
(C) Mimi siwezi kuwajua wauaji kwa majina kwa sababu sikuwepo hapo walipoyafanya hayo lakini kuna Circumstantial evidence inayoonyesha state organs inahusika kwa 100%, Mfano kule kutekwa kwa Roma Mkatoliki ni kielelezo tosha watekaji ni kina nani wanahusika based na maswali waliyomuuliza na mazingira aliyokuta humo ndani...ashukuru Mungu wasanii walipiga kelele ndiyo ikawa salama yake la sivyo yangempata yaliyompata Ben Saanane au Azzory Gwanda. Ben Saanane alipotea siku mbili baada ya kupata vitisho kwenye simu yake kuwa ataona baada ya kuandika humu akiulizia uhalali wa Ph.D ya Magufuli (angalau bwana mkubwa alitufafanulia kuwa hiyo Ph. D ni halali na anafahamu Kiingereza kwani ndiyo lugha aliyoandikia Thesis/Dissertation yake japo hakuulizwa-Labda alisoma humu Jamiiforums au bado anakumbuka Ben Saanane alichoandika)
Mazingira yote ya mauaji ya watu wanaokotwa baharini kwa makumi kila siku na mamia kwa mwezi inaonekana ni kazi ya state organs hilo halipingiki...Hakuna mtu binafsi (individuals) wenye kuweza kutekeleza mauaji mengi kiasi hicho asifahamike zaidi ya state....MBONA WAKIOKOTA MAITI HIZO WANAZIKIMBIZA HAWATAFUTI NDUGU ZA MAREHEMU????? Walianza kule mto Rufiji kuua kwa execution style watu walivyoanza kuwa na wasiwasi wakasema ni Wa-ethiopia wanaozamia kwenda South Africa...kama hayo ni kweli mbona hawakupeleka maiti hizo au hawakuhusisha ubalozi wa Ethiopia? au UNHCR ? Umesema tuache upelelezi uendelee? UNA UHAKIKA? Hadi leo hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyekwisha patikana.
Yote yametokea na yanaendelea kutokea amiri jeshi mkuu wetu ambaye ndiye msimamizi mkuu wa vyombo vyetu vya usalama amenyamaza kimya...HATA NENO MOJA HAJATAMKA! Halafu anajigamba yeye ni mkristo kweli na tumuombee! Hakuna shaka kabisa wahusika wakuu ni vyombo vyetu vya usalama......Nakumbuka maneno ya Magufuli alivyosema "Wewe unapinga pinga tu halafu uachwe uka-survive tu"? Kisaikolojia unaweza kumjua mtu huyu atafanya nini. Nchi zingine pamoja na kuwa na cheo cha urais, angetakiwa kusaidia upelelezi!
(D) Upoteaji wa wanaompinga Magufuli, upigwaji risasi wa Tundu Lissu, na utekwaji wa Roma Mkatoliki, MO Dewji nk. Hili halihitaji uwe na Professor ndugu yangu Paschal, Lissu alishasema anafuatwa na usalama wa Taifa na mazingira yake ya kupigwa risasi yanaakisi hilo, wote waliokumbana na madhila ya kufuatwa fuatwa na kutekwa wakafanikiwa kurudi masimulizi yao ya kufuatwa na magari yanayotumika yanafanana....Aidha Noah Nyeusi au Nissan Nyeupe. Sehemu yenye ulinzi na askari mlangoni 24/7 na Camera kwenye jengo inakosekana askari halafu Camera inang'olewa....Ilipelekwa wapi? Na hao askari walikwenda wapi? vipi ananyimwa mtu matibabu aliyejeruhiwa akiwa kazini? hadi leo wamemsusa hata Speaker kwenda kumwangalia tu....Mategemeo yao asingepona.....Hilo limechafua hii serikali mno hata mteteaje hilo halitafutika. Halafu Mkuu wa polisi anauliza wananchi kama unavyoniuliza Bw. Paschal kuwa mwenye ushahidi alete!! C'mon' RPC Muroto kama mlikuwa na nia mngefunga barabara moja tu mngewapata hao mnaowatafuta lakini kwa vile mna sababu za kufanya hayo mliyoyafanya hakukuwa na umuhimu wa kuhangaika. KUPANGA NI KUCHAGUA. Paschal hivi unaongea na upo serious au unatania? Yaani upeleke information polisi....Katika mazingira haya wewe uliyepeleka kwa nia njema utakuwa mshtakiwa wa kwanza,bila aibu polisi watakusimamisha mbele ya Camera watanzania wataambiwa kuwa muuaji amepatikana. UNAYAJUA YOTE HAYA PASCHAL SIJUI KWANINI UNA-ACT TOFAUTI LEO.
Angalia tukio la kutekwa kwa MO Dewji, kuna mwenye akili timamu atakubaliana na IGP Sirro kwanza kuhusu mazingira ya kutekwa kwa MO? pili Watekaji kuwa wazungu wakati eye witness amesema ni watu waliojifunika nyuso kama wanne wala siyo wazungu (hao wazungu, Makonda ambaye hakuwepo aliwajuaje au nani alimwambia), na hao polisi walikimbilia kuchukua mkanda wa CCTV hapo Colloseum hotel mara baada ya utekaji huo feki ili waufanyie nini? Camera ya CCTV yenye kuchukua picha kama studio inawezaje kuwa ya kweli....hivi hiyo knowledge ya polisi mbona ipo ndogo namna hiyo......Hata kudanganya hawafahamu? Paschal utathubutu kupeleka information unazozifahamu kwa polisi wa namna hiyo kweli? Sarakasi yake ya kupatikana ni zaidi ya Bongo Movie...Karibu na Ikulu, kama futi 1000 kutoka IKULU yetu tukufu INAYOLINDWA MASAA 24 na askari waliosambaa hadi jirani lakini hawakujua....isitoshe na watekaji wameacha na kazi yao ya utekaji na kurudisha bunduki zao......UWONGO UWONGO UWONGO MTUPU.
(E) Unakumbuka sana alivyosema kuwa ni fedha zetu wenyewe hatusaidiwi....INA MAANA GANI? Kama hukumbuki kwa nini usi-google? Ndiyo maana najiuliza Paschal nini kimekupata leo....I hope hujatekwa ukalazimishwa uandike ulichokiandika. Ukichangia asilimia moja (1%) kama unavyosema hiyo siyo significant hata atakayejitapa atakuwa hanazo kichwani kwa sababu haitaleta maana ya FEDHA ZETU WENYEWE kwa msisitizo.
 
Kuna ukweli
 

RIP Lemutuz
 
Wanasiasa wakishakuwa hivi dawa ni kufanya kama Nigeria au Ghana ya miaka 1960 - 1990s. Ni kubadilishana Majenerali pale Ikulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…