Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Kujitoa kwa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kunaweza pia kuwa na athari kubwa kwa upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) barani Afrika, kwani Marekani imekuwa mdau muhimu katika ufadhili wa mipango ya VVU/UKIMWI. Athari kuu zinazowezekana ni:


1. Kupungua kwa Upatikanaji wa ARVs


Marekani kupitia programu kama PEPFAR (President’s Emergency Plan for AIDS Relief) imekuwa chanzo kikuu cha rasilimali kwa ununuzi wa ARVs na miradi ya matibabu ya VVU/UKIMWI. Ikiwa msaada huu utapunguzwa kutokana na kujitoa WHO, mamilioni ya watu wanaotegemea dawa hizi barani Afrika wanaweza kuathirika.


2. Kuzorota kwa Huduma za Matibabu


WHO inasaidia nchi za Afrika kupitia uratibu wa miradi ya afya, mafunzo ya watoa huduma, na usambazaji wa dawa. Kupungua kwa msaada wa Marekani kunaweza kuathiri utoaji wa huduma muhimu, kama vile:


  • Vipimo vya mara kwa mara kwa wagonjwa wa VVU.
  • Ufuatiliaji wa maendeleo ya matibabu.
  • Huduma za kinga na elimu ya afya.

3. Ongezeko la Maambukizi Mapya ya VVU


Kupungua kwa upatikanaji wa ARVs kunamaanisha wagonjwa wengi wanaweza kushindwa kudhibiti kiwango cha virusi mwilini. Hii inaweza kusababisha maambukizi mapya kwa kasi zaidi, hasa kwa watoto wachanga na wenza wa wagonjwa.


4. Athari kwa Watoto na Wajawazito


WHO, kwa msaada wa Marekani, imekuwa ikiratibu upatikanaji wa ARVs kwa wajawazito ili kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kujitoa kwa Marekani kunaweza kudhoofisha juhudi hizi, na kusababisha ongezeko la watoto wanaozaliwa na maambukizi ya VVU.


5. Gharama za Dawa Kupanda


Kupungua kwa rasilimali za kimataifa kupitia WHO kunaweza kulazimisha nchi za Afrika kutafuta suluhisho mbadala, ambazo mara nyingi ni ghali zaidi. Hili linaweza kufanya dawa za ARVs kuwa ghali na hivyo zisifikiwe na walio wengi.


Kwa ujumla, kujitoa kwa Marekani kunaweza kurudisha nyuma maendeleo makubwa yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI barani Afrika, na kuathiri maisha ya mamilioni ya wagonjwa wanaotegemea ARVs kwa matibabu.
Ukimwi wa zamani unarudi, kazi tunayo...
 
Rais Donald J. Trump ametia saini agizo la kuiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) 20 Januari 2025, muda mfupi baada ya kuapishwa kwake

Uamuzi huu umezua mjadala na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wataalam wa Afya duniani.

Rais Donald Trump alitaja sababu kadhaa za Marekani kujiondoa kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO). Moja ya sababu hizo ni tofauti katika michango ya Kifedha, akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400.

Source:USAToday.
=======
My take
Tuamke.
Na sisi tujitoa AU pamoja na EAC
 
Moja ya sababu hizo ni tofauti katika michango ya Kifedha, akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400.
Wachina wana tiba zao za asili tangu kitambo tuliwashuhudia wakiwa wanajenga hii Mkapa Stadium na TAZARA
 
Hapa ndio utajua china sio taifa tajili kabisaa...........utajili wa china uko kwa uwingi wa watu tu na sio pesa...............labda na kutuuzia yale makoro koro yao fake........na kuchukua mitonyo yetu original...........ndio maana mi niliwapenda waliokuwa wanawatandika makontena ya michanga na kuwaambia hizo ni korosho
Unaandika ujinga sana
 
Tanzania tunahitaji kuwa na Rais mwenye akili kama za Donald Trump.

GOD BLESS ISRAEL
Mmeanza tena mambo yenu kama mlivyotaka Rais mwenye maamuzi magumu. Vyama vyote viwili vikatuletea watu wawili wa moto kwelikweli toka makabila ya wafugaji watata.
 
akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400.

Nini kimekukimbiza kwa kutoandika kiasi sahihi? 😊
 
Ndio maana mkurugenzi was WHO kaja juzi hapo magogoni kumbe mambo ndio hayo!!

CCM badili mgombea haraka sana!huyo mama hawezi kuongoza nchi inayopitia wakati mgumu!!!
 
"Tuamke"! Unataka na sisi tujitoe kutokana na kuchangia kiasi kikubwa kuliko China!
Hapana mazee. Nasema Tuamke na kuanza kuyathamini madawa yetu ya Asili. Nasema tuamke, tuwe na mikakati itakayowezesha Serikali kuacha Utegemezi kwa hivi vyombo.

Na Uhakika hata hiyo Marekani itarudi tu.🙏
Twafwaa mayo!
Usiogope Mkubwa.
Sisi ugonjwa upo tusaidiwe tunasema haupo! Mara haupo ila ni mtu mmoja tu anaumwa! NHIF inatushinda kuiendesha kwa sababu za udokozi usiokuwa na maana, sasa tutakwisha kwani hatutakuwa na watu wa kudhibiti magonjwa yasisambae.
Mimi iko na konfidenai na NHF katika ufanisi, hatahivyo huo Udokozi ufuatiliwe na Unyongaji wa Wadokozi ama unaonaje?
 
Zile hazihusiani na hili. Ukiseikia PEPFAR na USAID zimeguswa hapo ndiyo ujue pamechangamka, by the way na wenyewe ameshawaambia wajiandae sababu haoni kwanini waendelee kutoa hiyo misaada.
Hapo atakua kakanyaga waya waafrika tutaisoma namba huku.
 
Hapa ndio utajua china sio taifa tajili kabisaa...........utajili wa china uko kwa uwingi wa watu tu na sio pesa...............labda na kutuuzia yale makoro koro yao fake........na kuchukua mitonyo yetu original...........ndio maana mi niliwapenda waliokuwa wanawatandika makontena ya michanga na kuwaambia hizo ni korosho
Kwa maelezo haya ni halali tu Marekani kujitoa WHO maana ni kama wanatoa misaada ya kiafya kwa wajinga.
 
Back
Top Bottom