Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

IMG_0100.jpeg


Rais wa Marekani Donald Trump leo amesaini executive order ya kuindoa US kwenye uanachama wa Shirika La Afya Duniani (WHO).

Trump aliwahi kutoa shutuma nyingi dhidi ya WHO wakati wa kipindi cha Covid na aliashiria kujitoa.

US inachangia karibia asilimia 18 ya bajeti ya WHO.

Soma zaidi hapa: Donald Trump signs order to withdraw US from World Health Organization
 
Kujitoa kwa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kunaweza kuwa na athari kubwa kwa Afrika, ikizingatiwa jinsi bara hili linavyotegemea msaada wa kimataifa katika sekta ya afya. Athari kuu ni pamoja na:


1. Upungufu wa Rasilimali za Fedha


Marekani imekuwa mmoja wa wafadhili wakubwa wa WHO, ikichangia takriban 15% ya bajeti ya shirika hilo. Kujitoa kwake kungepunguza rasilimali zinazopatikana kwa miradi ya afya barani Afrika, kama vile:


  • Mapambano dhidi ya magonjwa kama malaria, kifua kikuu, na VVU/UKIMWI.
  • Chanjo na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama polio na surua.

2. Kupungua kwa Msaada wa Dharura


WHO ina jukumu muhimu katika kushughulikia dharura za kiafya, kama vile milipuko ya magonjwa na majanga ya asili. Kujitoa kwa Marekani kungeathiri uwezo wa WHO kusaidia nchi za Afrika wakati wa dharura za kiafya, kama ilivyoonekana wakati wa milipuko ya Ebola.


3. Kudhoofika kwa Miradi ya Kinga na Uzuiaji wa Magonjwa


Afrika inategemea sana mipango ya kinga inayoungwa mkono na WHO, kama vile Mpango wa Chanjo Duniani (Gavi). Bila msaada wa Marekani, miradi hii inaweza kukumbwa na changamoto za kifedha, na hivyo kuhatarisha afya ya mamilioni ya watu.


4. Athari kwa Ushirikiano wa Kimataifa


Kujitoa kwa Marekani kunapunguza mshikamano wa kimataifa katika kushughulikia changamoto za kiafya. Afrika inaweza kupata changamoto zaidi kushirikiana na WHO kutokana na upungufu wa rasilimali na ushawishi wa kisiasa.


5. Kuongezeka kwa Utegemezi kwa Mataifa Mengine


Nchi za Afrika zinaweza kulazimika kutegemea zaidi msaada kutoka kwa nchi kama China, Umoja wa Ulaya, au taasisi za kibinafsi, ambazo zinaweza kuwa na vipaumbele tofauti.


Kwa ujumla, kujitoa kwa Marekani kutoka WHO kunaweza kudhoofisha juhudi za kuboresha afya barani Afrika, hasa kwa wale walioko kwenye mazingira magumu zaidi.
Chat GPT
 
Tayari pameshaanza kuchangamka..wale tuliozea dezo huu ndio mwisho
Hapo ni balaa tupu bado anaitaka greenland anasema kwa kuinunua hata kuivamia, bado anasema anaweza chukua ile canal kule america kusini ambayo anadai amerika iliwapatia bure wakati imechimbwa kwenye eneo lao wenyewe sasa huo ubure sijui unatoka wapi.
Ban ya tiktok kaisimamisha jana so tiktok imerejea US.
NATO nao hawaelewi elewi nini kinaweza tokea. Wasiyemtaka kaja.
Sema kilichonifurahisha, trump yeye hajali masuala ya inclusive kazini na meta imefuta rasmi sera zake za ujumuishi sijui wa gender diversity so mashoga na waliobadili jinsia watajibebea wenyewe
 
Sasa Tundu lissu akichukua nchi atakutana na wakati mgumu sana.

Naona pia ARV zitaanza kuuzwa sasa maana WHO wamepungukiwa mchango wa marekani.
ARV siku zote zinauzwa. Wanachokifanya Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR, ni kununua haya madawa kutoka kwenye kampuni kubwa za Madawa halafu wanatugaia kama Msaada as part of their "soft policy" bure. Offcourse baadae lazima upanue.
Au mchango wa marekani wa hizo dola hauna athari?
Athari ni ndogo sana. Almost none. Msaada wa ARV's kutoka marekani ni Direct Funding na hazipitii WHO. Nimehakikishiwa PEPFAR itakuwepo, anagalabu kwa sasa.
Tutakufa kama kuku sasa
Kuku wanakufaje?🤣
 
Inabidi tujitambue, tuache matumizi mabovu kama;
-Goli la mama
-Ununuzi wa magari holela ya viongozi
-Ununuzi wa MABASI YA CCM☹️
-N.K

Kinyume na hivyo tujiandae kuzika/kuzkwa.
Wale wa kuzimu mtabakia kuzimu wale wanaoishi paradiso wataendelea kuishi paradiso
 
Wangemuambia tu China aongeze mchango Jamani 🤭
Kipindi cha COVID19 aliwahi kuonya kuwa ata freez US$400 China akajitutumua kuwa kama US ita freez hela yake basi WHO wasiwe na wasiwasi, wao China wata inject US$ 50😅, halafu WHO wakafurahi.

Viongozi wapigaji WHO hawaoni umuhimu wa mchango wa US sababu wanafanya water tight financial monitoring ya funds zao zisije zikatumika visivyo, every dollar itahtajika maelezo ya namna gani imetumika.

Kila activity lazima iwe justfied, na kila vendor atakayelipwa kwa hela yake ni lazima awe screeed vya kutsha na kufanyiwa background checks ili isije huyo vendor akawa anatafuta hizo pesa ili kuzipeleka kuendesha makundi ambayo ni maadui wa Marekani, au kukawa na conflict of interest na mengineyo.

Lakini hela ya China huwa hata haina ulinzi wa hivyo. Kwanza hutoa kwa ajili ya mambo yanayoihusu, pili hata anapochangia kwenye mambo mengine huwa haulizi mmetumiaje, wala hataki ushahidi wa matumizi. Anachozingatia China ni hata mkipeana mgao, basi maafisa wake wasiwe sehemu ya huo mpango wa kugawiana, maana atawanyonga.
 
Back
Top Bottom