Rais Uhuru aongoza marais kumi wa Afrika katika kupigia debe dawa ya Madagascar

Rais Uhuru aongoza marais kumi wa Afrika katika kupigia debe dawa ya Madagascar

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hii dawa ya Madagascar japo haijatolewa maelezo ya kisayansi vizuri, lakini imebidi ipokelewe maana kuna ushahidi wa watu wachache kupona Corona baada ya kuitumia. Hivyo rais Uhuru na marais wengine kumi wa mataifa ya Afrika wameamua kuhamasisha utumiaji wake, watawekeza nguvu, raslimali, wataalam n.k. katika kuwasaidia Madagascar wazalishe kwa wingi ili itumike Afrika na duniani kote.

WHO bado wameshikilia kwamba ni hatari kutumia dawa yoyote ambayo hawajaidhinisha wao, ila kwa sasa tupo kwenye dharula, hamna muda wa urasimu, hata Marekani juzi wamezindua dawa ambayo hao hao WHO hawajakubali itumike dhidi ya Corona.

Maelfu ya watu wanakufa, hakuna muda wa kusubiri, inabidi kila mmoja afanye chochote anahisi kitamuokoa.

Marais hao ni Cyril Ramaphosa (South Africa), Abdul Fatah El Sisi (Egypt), President Felix Tshisekedi(DRC), Paul Kagame (Rwanda), Ali Bongo (Gabon), Mahamadou Issoufou (Niger), Idris Derby (Chad), Boubacar Keita (Mali) and Andry Rajoelina (Madagascar).

=====

President Uhuru Kenyatta addresses the nation at State House, Nairobi, in April 2020

President Uhuru Kenyatta addresses the nation at State House, Nairobi, in April 2020

President Uhuru Kenyatta was part of a teleconference call involving 10 African Heads of State that discussed the adoption of Covid-19 organic medicine.

The meeting on Saturday, May 2, was held to discuss in detail the efficacy of the Covid Organics Medicine(CVO) that was developed by Madagascar in treating Covid-19 patients.

The President of Madagascar, Andry Rajoelina took to Twitter on Monday, April 20, to claim that the concoction named Covid Organics (CVO) – a form of herbal tea – is curing Covid-19 patients.

World Health Organization (WHO) however in a statement warned against any self-medication and said that it has not recommended any medicine as a cure for the Covid-19.

Malagasy President, chaired the meeting and presented the product to the other Heads of States in the video conference call.

Presidents present in the meeting were, Cyril Ramaphosa (African Union Chairperson and South Africa), Abdul Fatah El Sisi (Egypt), President Felix Tshisekedi(DRC), President Uhuru Kenyatta (Kenya).

Paul Kagame (Rwanda), Ali Bongo (Gabon), Mahamadou Issoufou (Niger), Idris Derby (Chad), Boubacar Keita (Mali) and Andry Rajoelina (Madagascar).

They also formed a Covid-19 Ministerial Response Coordinating Committees on Health, Transport, Finance and Agriculture to respond to the various factors surrounding the Coronavirus pandemic.

The Bureau of Heads of State of the African Union also formulated a continental strategy to better prepare and respond to any new cases of the virus on the continent.

The meeting also shared experimental drugs on the deadly virus, vaccines and clinical trials that have kicked off around the world.


Source: Kenyans.co.ke
 
Ingekua Ni Tanzania CITIZEN na TV Zote za Kenya na Za UFIPA zingeponda

Kwenu huwa mnapondwa kwa jinsi mnapenda kujikanganya, full mikwara isyokua na tija na kauli zisizoendana, mara

- Corona itaungua ikiingia kanisani
- Corona ni kaugonjwa
- Watu wajifukize maana Corona ni futa
- Mara mganga mkuu wa taifa atahadharishe dhidi ya kufukiza
- Msije Dar watu wanapukutika
- Corona inaletwa na barakoa
- Corona inasambazwa kwa kunyunyiza dawa Dar es salaam maana ni upuzi
- Mara sijui yule Mwigulu anasema data zifichwe zitangazwe za wanaopona
- Mara waziri wenu wa afya aseme ameamua kuongea ukweli tangu sasa
- Mara waziri mkuu wenu aseme waliopona ni kumi na mmoja huku rais akisema ni zaidi ya mia

Mara hiki mara kile, hamna kauli moja ya kueleweka ili msiklizwe, kila mmoja anaibuka na lake.
Mjifunze na rais wa Madagascar, yeye ameshikilia kimoja, ameipigia debe dawa yao na hajatetereka sehemu yoyote na kuja na kauli tofauti.
 
Lkn ikija hku kwetu wanasayansi wazawa waifanyie kazi kwanza, manake huwezi kuwa mwansayansi halafu ushindwe kujua km kitu flani ukikitumia kinaweza kuwa na madhara flani au zii
 
Lkn ikija hku kwetu wanasayansi wazawa waifanyie kazi kwanza, manake huwezi kuwa mwansayansi halafu ushindwe kujua km kitu flani ukikitumia kinaweza kuwa na madhara flani au zii

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio maana marais wote kumi wameamua kuwekeza humo kwa kutoa maagizo kwa wataalam wa kila taifa husika waungane na wa hao Madagascar na kuwasaidia kufanikisha shughuli yote nzma.
 
Mbuzi huyo ni ndumilakuwili, alikuwa anasifia dawa ya marekani nikamwambia abt hii dawa akawa anaikandia. Leo boss wake amesifia, anajidai kuirecognize.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulinikaza nianze kushabikia hii ya watu wa Madagascar, leo nimeifungulia uzi baada ya marais kumi kuikubali unaibuka na matusi.

Unafaa ufahamu urais ni taasisi, marais kumi kukubali kitu ina maana wataalam wao wameipitia na kuikubali na kuwashauri waikubali, hivyo sina budi pia kuikubali. Lakini hauwezi ukategemea nikubali kila kitu kinachoangazwa na makajamba wote duniani.
 
Ingekua Ni Tanzania CITIZEN na TV Zote za Kenya na Za UFIPA zingeponda
Safi sana, kumbe mnajua kwamba hamuaminiki? Miaka inasonga tu na bado hadi leo hii hatujapata mrejesho kuhusu kikombe cha babu wa Loliondo.

images
 
Wakati, JPM tayari ameshafanya maamuzi ya kutuma ndege Madagascar kuleta first consignment ya dawa....
 
WHO ni mabeberu.

Wapo kwa maslahi ya mabeberu, kwa hiyo hawawezi kukubaliana na chochote mpaka mission yao itimie.



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom