Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenu huwa mnapondwa kwa jinsi mnapenda kujikanganya, full mikwara isyokua na tija na kauli zisizoendana, mara
- Corona itaungua ikiingia kanisani
- Corona ni kaugonjwa
- Watu wajifukize maana Corona ni futa
- Mara mganga mkuu wa taifa atahadharishe dhidi ya kufukiza
- Msije Dar watu wanapukutika
- Corona inaletwa na barakoa
- Corona inasambazwa kwa kunyunyiza dawa Dar es salaam maana ni upuzi
- Mara sijui yule Mwigulu anasema data zifichwe zitangazwe za wanaopona
- Mara waziri wenu wa afya aseme ameamua kuongea ukweli tangu sasa
- Mara waziri mkuu wenu aseme waliopona ni kumi na mmoja huku rais akisema ni zaidi ya mia
Mara hiki mara kile, hamna kauli moja ya kueleweka ili msiklizwe, kila mmoja anaibuka na lake.
Mjifunze na rais wa Madagascar, yeye ameshikilia kimoja, ameipigia debe dawa yao na hajatetereka sehemu yoyote na kuja na kauli tofauti.
Kwenye hotuba ya jana haujamsikia rais wetu akisema wameshaawasiliana na Madagascar ndege itafuata hiyo dawa?
Jifunze kusoma saa ambayo mtu amepost kabla haujajibu, niliweka hilo bandiko kabla ya hotuba ya rais, ila pia ndio yale yale, ongeza hiyo ya kufuata dawa Madagascar kwenye orodha yangu huyo ya jinsi mna kauli za kila aina.
Nikiamua kuweka muendelezo wa kauli na vituko vyenu huko nitajaza server za watu bure, maana jana pekee yake mumeibuka na mengi yakiwemo kupima mbuzi, mapaipai na n.k. Ndio maana kwenye orodha yangu nilihitimisha kwa kusema "Mara hiki mara kile", hiyo imeshikilia vituko vyote mnatakavyoibuka navyo mbeleni.Nimeandika hivyo baada ya kuona hautambui hilo kwenye mwendelezo wa post yako, vinginevyo niwe sijapitia kila ulichokiandika. Ulitakiwa ufanye update kuonyesha jinsi na sie tulivyochukua hatua kuhusu hiyo dawa.
Wakati mie najifunza hilo unakumbuka wakati unapandisha ule uzi kuhusu kupatikana US kwa kuanza na hatimae dawa yapatikana tayari hii ya Madagascar ilikua imeshaanza kutumika?
Lakini bado uliipa kipau mbele na kuipigia debe hiyo dawa ya US kisa FDA yao imeiruhusu itumike.
Nikiamua kuweka muendelezo wa kauli na vituko vyenu huko nitajaza server za watu bure, maana jana pekee yake mumeibuka na mengi yakiwemo kupima mbuzi, mapaipai na n.k. Ndio maana kwenye orodha yangu nilihitimisha kwa kusema "Mara hiki mara kile", hiyo imeshikilia vituko vyote mnatakavyoibuka navyo mbeleni.
Dawa ya Wamarekani ilitolewa maelezo ya kisayansi, ndio maana naipigia upatu hadi leo, kiaina fulani inaelezwa inavyofanya kazi na pia hatua zote zilizofanywa kule Marekani hadi ikaja kukubalika na taasisi ya FDA na kuruhusiwa itengenezwe kwa wingi na kuachiwa ili itumike na mamilioni ya waathirika huko huko Marekani.
Hii ya Madagascar, mpaka sasa nimetafuta kote kwenye mitandao maelezo yake ya kisayansi, au wataalam popote wanaijadili kitaalam, sijafaulu, binafsi mimi sio mtaalam ila nikikuta comments za wataalam wanajadili kitu huwa kiaina fulani napambana hadi kuwaelewa, nimesaka sana comments zozote kuihusu.
Kwa hapa nimelazimika kuikubali tu kisa imekubaliwa na marais kumi, hawa marais wote wana wataalam wengi nyuma yao lazima watakua wamewashauri.
Hao marais ndio wataalam wa madawa? Ikiwa kweli unathamini au kutambua utaalam unahabari hata WHO bado wanaukakasi na dawa ya Marekani?
Wamadagascar hawajataka utumwa wa kifikra, iweje WHO na US watishie matumizi ya dawa yao kiasi cha kusitisha misaada ya kupambana na Corona badala ya kuunganisha juhudi kuifanyia utafiti endapo kweli inatibu na ina madhara?
Pili, kwa kuwa unajinasibu ni mfuatiliaji wa habari za kitaalam, umewahi kusikia hitilafu au mapungufu yeyote ya vipimo vinavyotumika kupima virusi vya Covid 19? Inamaana rais kuhoji usahihi na ufanisi wa hivyo vipimo imekua nongwa? Approach inaweza isiwe sahihi sana, lengo Je?
Mwisho, tutapigizana kelele hapa lakini ikiwa ni madhara au machungu ya Corona kati ya Kenya na Tanzania tupo kwenye chombo kimoja. Hadi sasa hakuna mwenye ahueni.
Unavyotapatapa hehehe!!!
Sijasema marais ni wataalam, nisome tena badala ya kupoteza muda, fahamu urais ni taasisi, nyuma ya rais kuna wataalam wa kila aina wanaompa brief kutoka kila sehemu. Ndio maana rais akiibuka na kauli za kiajabu kama rais wenu (kwamba corona haingii kanisani itaungua) inabidi ajadiliwe dunia yote maana watu wanakosa kuelewa ikawaje wataalam wake wote waboronge kiasi hicho kwenye kumshauri.
Kwa hii ya Madagascar, narudia tena kusema, naipa attention maana imekubaliwa na marais kumi, nyuma yao kuna wataalam maelfu kwenye mataifa yao, hivyo haiwezekani wote wakawa majuha.
Japo kiukweli bado sijaona popote imetolewa taarifa zozote za kisayansi, maelezo yoyote au inafanya kazi vipi, sijakuta popote wataalam wanajibizana kuihusu, maana kidogo nitafaulu kupata mwanga kiaina, hii ipo tu kama some black magic fulani hivi.
WHO wana jukumu la kuikosoa maana wanakwenda kwa kutumia protocols au kanuni na sera ambazo zimewekwa kitaalam na wataalam duniani, hawawezi wakakurupuka kuunga mikono chochote bila kufuata hizo kanuni, na ndio maana hata ile ya Wamarekani bado hawajaidhinisha rasmi.
Wamarekani, walifanya utafiti wao na kutolea kisayansi jinsi gani wamefikia mpaka kwenye hatua za kukubali itumike, hivyo ni jukumu la wanasayansi kukosoa au kuunga juhudi zao mikono, lakini hamna taasisi yoyote yenye uwezo wa kushinikiza taifa lolote kufuata aina fulani ya muongozo, na ndio maana WHO wameisema Tanzania kwenye kutotoa taarifa za waathirika wa Corona kila siku, lakini hawana uwezo zaidi ya hapo, hawawezi wakalazimisha.
Hakuna mwenye uwezo wa kulamisha Watanzania waache ukaidi wa kuendelea na misongamano kwenye vilabu vya pombe, mtasemwa tu lakini inaishia hapo.
Kuuliza maswali ni kutapatapa? Inamaana marais wote ni taasis isipokua wa Tanzania? Ndio maana inakua shida kujadili jambo kitaalam mihemko inapochukua nafasi kubwa ya mjadala. Hadi sasa sijajua tunaongelea mikusanyiko, Dawa ya Covid Madagascar au umathubuti wa marais.
Ndio maana nikasema unatapatapa maana sikuelewi kipi haswa una shida nacho.
Nimesema urais ni taasisi, ikiwemo wa Tanzania, na ndio maana kauli ya rais wenu kwamba Corona itaungua ikiingia kanisani iliibua mjadala mkubwa ikiwemo kutajwa kama "mkaidi", maana watu walishangaa taasisi ya urais Tanzania, wataalam wote humo kwenye hiyo taasisi mbona wanampotosha rais.
Ingekua kweli itaungua ikiingia kanisani, sote tungepanga foleni na kuponea humo badala ya vifo tunavyoviona.
Mimi naona hio aibu iko kwenyu tayari, kuficha maisha kn the ground na denialismEti aongoza marais Africa, hivi nyinyi wakenya mbona mnajiona mna akili sana wakati ni watu wa kawaida tu,hivi mentality, za kikoloni zitawatoka lini,mnawaona waafrika wenzenu ni 2nd class, inasikitisha sana.hii dawa ya Madagascar iliagizwa na nchi ya DRC Kwanza baadae nchi za Afrika magharibi zikafuata,alafu nchi yetu za EAC,ikiwemo Kenya.Na kwa hili swala la Corona, tungenyamaza Kwanza kwa sababu, Corona is here to stay,msijitape na mass testing na curfew, nakuhakikishia,kuna watu wataibika hapa EAC mda si mrefu.
Yes,and the language should be Kiswahili, and not English that has ruined some African's minds and made them think and behave like Zombies!
Nn tumeficha?nyinyi ndio mlianza kutusema kwamba tunarudia enzi za kinjekitile kwa kutumia traditional method kupambana na Corona, sasa nashangaa mnakuja kulekukule mlipokuwa mnapatukana.Mimi naona hio aibu iko kwenyu tayari, kuficha maisha kn the ground na denialism
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata wakiwa maraisi wote wa africa. Dawa hii sijaona ushahidi kuwa inatibu. Wenye uelewa wataomba documentation ( protocol na results) au wataifanyia trials wao wenyewe. Vinginevyo bado ni kikombe cha Babu.Safi sana, kumbe mnajua kwamba hamuaminiki? Miaka inasonga tu na bado hadi leo hii hatujapata mrejesho kuhusu kikombe cha babu wa Loliondo.![]()