kiaina nakubaliana na wewe, ila fahamu umuhimu wa lugha ni watu kuelewana. Nikiona Mturkana mwenzangu atanielewa vizuri nikimpa maagizo kwa Kiturkana, basi sioni haja ning'eg'anie Kingereza na Kiswahili. Fahamu hata hicho Kiswahili kuna mtu atakutembelea Tanzania na hakifahamu, sasa ukimtembeza na ukutane na jamaa wako, ina maana mtanyamaziana maana utakua hutaki mgeni wako ahisi vibaya.
Ukiingia ndani ya daladala Kenya, watu wamekaa wakiongea yao kwa lugha zao, huna haja ya kuelewa wanachokisema maana huwafahamu na haikuhusu. Kitu ambacho hakifai ni matumizi ya lugha yako hata kwa masuala official na wakati kuna watu wa lugha zingine karibu. Kwa mfano kuna kipindi nilikerwa sana na afisa wa uhamiaji Kenya kwa kuniongelesha kilugha baada ya kuona majina yangu, ilhali tulikua kwenye foleni na walikuwepo watu wa lugha zingine, hiyo kwa kweli haikunipendeza, na niliona kama amewanyanyasa watu waliokuwepo pembeni.
Lakini hamna kitu kibaya wakati watu wanafurahia asili yao, tatizo ni wakati inatumika vibaya, kwa mfano kwa kuwabagua watu wengine.