Rais Uhuru Kenyatta, William Ruto wafuata nyayo za Rais John Magufuli

Rais Uhuru Kenyatta, William Ruto wafuata nyayo za Rais John Magufuli

Rais wa china haongei kiingereza na anakwenda kukutana na wanaozungumza kiinigereza. Na akikutana nao yeye hupiga kichina chake tu.

Mfano mwengine Umoja wa mataifa, kuna viongozi wanaongea lugha za kwao tu. kwaio Lugha sio sababu ya mtu asiende nje. Tafuta jengine
Unataka siku aliialikwa White House aende na mkalimani wa Kisukuma?😂
Maana siku hizi baada ya kutokuwa fasaha kwa kiswahili na kiingereza ameunda lugha yake ya Kiswanglish . Juzi kawaambia watu wa UN nanukuu.
"...we have surplus of food ya chakula"
 
Unataka siku aliialikwa White House aende na mkalimani wa Kisukuma?[emoji23]
Maana siku hizi baada ya kutokuwa fasaha kwa kiswahili na kiingereza ameunda lugha yake ya Kiswanglish . Juzi kawaambia watu wa UN nanukuu.
"...we have surplus of food ya chakula"
Then aka secure deal la kuuza mazao na kusifiwa na hao UN! Kuna wa hindi wameshika post za maana sana kwenye kampuni zetu hapa na wana piga yai broken ila they make things happen and that is it! Dont be petty

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Then aka secure deal la kuuza mazao na kusifiwa na hao UN! Kuna wa hindi wameshika post za maana sana kwenye kampuni zetu hapa na wana piga yai broken ila they make things happen and that is it! Dont be petty

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
"...we have surplus of food ya chakula" Hii ndio kusema nini mkuu?
 
Eti hajatoka zaidi ya nchi za EAC, hebu tuwe wakweli, lipo tatizo linalomfanya asiende jamani, ngeli ikiwa sabb, huko nje ile unatua uwanja wa ndege unakutana na waandishi wa CNN, BBC, CBN news, AP, Aljazeera na wengine, utatwangwa maswali acha kabisa, sasa ngeli hizi za theee, theee, unaweza kutia aibu
 
Msaada ulikua unaombwa so sioni cha maana cha kumsifia huyu jiwe eti hajasafiri anabana matumizi wakati Nchi bado inanuka njaa tu.
Iyo misaada iliyoombwa ilisaidia nn cha tofauti hukipati hizi enzi za magu.
Magu hasafiri lkn tunaona big results.
 
WAKATI Rais John Magufuli akionesha mfano kwa kubana matumizi katika safari za nje, nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto wamepunguza safari za nje ya nchi kwa asilimia 79 ndani ya miezi tisa.
Kwa Rais Magufuli aliyeingia madarakani kuiongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania kuanzia Novemba 5, mwaka 2015, mpaka sasa hajatoka nje ya ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), licha ya kuripotiwa kuwa na mialiko ya zaidi ya nchi 100.

Ametembelea kikazi Rwanda, Uganda na Kenya ambazo ni sehemu ya nchi za EAC, nyingine zikiwa Tanzania, Burundi na Sudan Kusini.
Kazi nyingine za ndani na nje ya Afrika amekuwa akiwatuma ama Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wakati mwingine viongozi wengine waandamizi serikalini. Mathalani, katika kipindi cha miezi tisa wametumia Sh milioni 36.5 za Kenya kufikia Machi mwaka huu.

Taarifa kutoka kwa Mdhibiti wa Bajeti nchini Kenya zinaonesha kuwa, safari hizo zimeokoa zaidi ya Sh milioni 143.7 za Kenya, kutoka Sh milioni 180.2 zilizotumika katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Uamuzi wa kupunguza safari umeonekana kushika kasi zaidi tangu Rais Kenyatta aanze kuitawala Kenya katika awamu yake ya pili mwishoni mwa mwaka jana. Wakati anaingia madarakani Aprili mwaka 2013, Kenyatta alitumia Sh milioni 75.9 za Kenya kwa safari za nje.

Na tangu hapo, bajeti ya safari ilipaa. Kufikia Machi, 2016, alitumia Sh milioni 167.5 za Kenya kwa safari za nje, ikiwa ni ongezeko kutoka Sh milioni 138.5 zilizotumika katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Aidha, safari za mawaziri, wakuu wa mashirika na taasisi za umma nazo zimeshuka kwa asilimia 33 hadi Sh bilioni 3.07 za Kenya ikilinganishwa na Sh bilioni 4.6 za nchi hiyo zilizotumika mwaka uliopita, jambo linaloashiria kuwa, kazi ya kubana matumizi kwa safari za nje inazaa matunda.
JPM aokoa matrilioni Kwa mujibu wa Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kati ya Nonemba 2015 na Novemba 2016, serikali iliokoa kiasi cha Sh bilioni 902 kutokana na kusitisha safari za nje ya nchi kwa watumishi wa serikali. Ripoti hiyo ilionesha kuwa, Tanzania ilitumia kiasi cha Sh trilioni 1.7 katika safari za nje ya nchi, ikiwa ni sawa na punguzo la trilioni 1.2 ambapo kwa kipindi kama hicho Novemba 2014 hadi Novemba 2015, serikali ilitumia kiasi cha trilioni 2.64 kwa safari za nje ya nchi.

Novemba 6, 2015 ikiwa ni siku moja tangu aapishwe kuishika Ikulu ya Tanzania, Rais Magufuli alisema safari za nje ya nchi zilikuwa zikiigharimu Tanzania fedha nyingi ambazo zingeweza kutumiwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mbali na kuzuia safari za nje ya nchi, Rais Magufuli pia alifuta semina elekezi kwa viongozi, alipiga marufuku kufanyia mikutano kwenye kumbi za hoteli, kufuta sherehe za uhuru na kadhalika na badala yake, fedha za shughuli hizo zilitumika kwa shughuli nyingine za maendeleo.

Kagame, Museveni Wakati Magufuli na Kenyatta wakionekana kushika hatamu katika kubana matumizi ya fedha za umma kwa safari za nje, marais wengine wa ukanda huo, nao wana mtazamo sawa.
Hata hivyo, Rais Paul Kagame wa Rwanda anaonekana kuwa na safari nyingi za nje kutokana na kuwa pia na majukumu ya kimataifa, kwani kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Kwa Museveni, pia safari zake za nje kwa sasa zinachangiwa pia na nafasi yake ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayohitaji safari za mara kwa mara za kikazi kwa ajili ya jumuiya hiyo yenye zaidi ya wakazi milioni 160.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hajaonekana kuwa na safari za nje kwa takribani miaka miwili sasa, wakati Salva Kiir wa Sudan Kusini, naye amekuwa na safari chache, ukiondoa nyingi za safari za ndani ya jumuiya zinazolenga kumkutanisha na wadau wengine katika mchakato wa kusaka amani ya kudumu katika taifa hilo changa zaidi duniani.
Hivi hii single ya kutosafari nje bado ina hit?
 
Kubana matumizi ya serikali ya kenya si kwa kupenda kwao. IMF imeamuru GoK wasitishe matumizi ya pesa kwa miradi mipya na matumizi hovyo lasivyo waondoe Foreign Exchange reserve safety net. Si kwa hiari yao kama vile JPM amefanya mwenyewe
Mbona "yao" zimekua nyingi? We si Gz. mkenya wewe? Usijitoe ufaham. Sema "serekali yetu"!!😂😂😂
 
Hujui hao wanaogopa kusafiri maana hawana uhakika wakiwa nje ya nchi yao, wanaweza kujikuta sio tena viongozi!?
 
Wewe huwezi kuelewa!
Kuna mashirika ya ndege ya nje yamepunguza safari zake na mengine yamefuta kabisa kuja Dar, Maana wateja wao wakubwa walikuwa ni watumishi wa Serikali!
Usiongee vitu ambavyo huvijui kijana mdogo walahi!
That’s all!
Unasafiri ili kuwafaidisha mashirika ya ndege ama unasafiri ili kuiletea manufaa nchi yako. Ndo maana huwa wengine nikiwahurumia huwa nawambia wapumbavu
 
Back
Top Bottom