Rais umekosea kuwakilishwa na Balozi kwenye mkutano wa EAC kuhusu Congo

Rais umekosea kuwakilishwa na Balozi kwenye mkutano wa EAC kuhusu Congo

Rais wetu ametumia busara kutokwenda huko , issue ya congo imekuwa influenced the Rwanda ambaye ni mwanachama wa EAC , then unataka tukae chini kuzungumza nini ,??????
'Whether', uamzi wake wa kutokwenda kwenye kikao hicho ni shauri ya Rwanda (nina mashaka juu ya hili), au mambo mengine yanayoendelea sasa hivi(ikiwa ni pamoja na malori), ninapongeza uamzi wa kutoshiriki kwake katika upuuzi ule.
 
Rais hapa kakosea na tumekuwa wazembe sana na wavivu kama nchi. Congo DRC ni sehemu muhimu sana lakini tumekuwa wazembe sana na tunawaachia nchi za nje wanatumia mbinu za kuwagombanisha ili tu wachukue madini. Tanzania kama nchi kubwa tulikuwa na uwezo mkubwa sana kuanzia enzi za kabila kuifanya Congo kuwa sehemu yenye usalama na kusaidia nchi yetu.

Kwenye mkutano wa Kenya, Tanzania imewakilishwa na balozi yaani hata Makamu wa Rais au waziri wa ulinzi ameshidwa kwenda. Ni aibu na ni Rais gani ataongea vitu vya siri kwa balozi? Tusishangae balozi wetu kuwekwa nje wakati wakiongea mambo muhimu.

Ni bora hata Rais Samia angetumia mtandao na sio hivi. Lakini kibaya tunaonekana dhaifu sana kwa Rais wa Congo kwasababu tu tunaogopa kumkasirisha Kagame kwa kupingana naye kwenye hili. Kikwete ndiye aliweza kumsema wazi wazi na Samia hapa kakosea na kuonyesha udhaifu mkubwa kwa majirani zetu.


Tuna vikosi huko mkuu.juzi juzi tu hapa tumeshambuliwa na hao M23 huko Goma.Rais Samia anajua sana ndio maana kaamua kuwakilishwa na Balozi.
 
Back
Top Bottom