Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

Mi niko na wewe. Sijaona shida ya katiba iliyopo zaidi ya shida ya wananchi wenyewe. Ni kupitia Katiba hii mimi wa Nakapanya naweza kwenda Ngara na kuoa, na kupewa Shamba bure na kulima na kufanya maisha na mtoto wangu akaamua kwenda kuishi chakechake peacefully. Nadhani kama nchi tatizo letu sio katiba bali malezi kuanzia ngazi ya familia, unless niambiwe katiba mpya itasaidiaje kuwafanya wahadzabe wasiishi naporini.
Hoja nzito kabisa hii
 
Wazo lako ni sawa na wakulima wanataka kuwekewa mfumo wa Kunywesha mashamba yao wanakataa kwa kusema wasikilizwe kwani Mvua ya Mungu inatosha...
Ninachotaka kusema ni kuwa, rudi darasani au fanya utafiti kujua kwa nini watu wanataka katiba mpya; ukishapata hojazao; utanielewa ninachokisema!
Hata wewe inaonekana unahitaji elimu ya kujua kwamba katiba sio chanzo Cha umaskini wetu Bali uvivu
 
Punga kama wewe huna hoja za kupeleka mahakama, endelea kujifariji tu hapa jf na wajinga wenzio
Jamii forum Haina wajinga kama Kuna mjinga hapa jf wewe ni namba moja
 
Tatizo la wanasiasa haswa vyama vya upinzani wanadhani kuwepo kwa katiba mpya kutawawezesha washike dola!!!!!
Mimi nasema fikra hizo ni za kipuuzi!

Mfano angalia nchi JIRANI ya Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya nzuri lakini kila Uchaguzi Raila analia hakubali matokeo na hakubali maamuzi ya mahakama!!!!

Kwa maana hiyo ni wazi kuwa katiba mpya sio "mwarobaini"

Kwa mtizamo wangu, maadili/uadilifu ndio jambo la msingi ambao hauletwi na katiba mpya bali unajengwa kwa kizazi na kizazi.

Uadilifu na maadili mazuri ya viongozi wetu wote walio pita kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa awamu ya sita ni kutokana na uadilifu wa viongozi wetu, wamejengwa na kulelewa kwenye misingi ya maadili na uadilifu.
Asante sana mkuu elimu hii inatakiwa tuitoe wananchi wanapelekwa pelekwa TU
 
Hakuna kinachopiganiwa hapo zaidi ya maslahi ya wanasiasa
Mkuu naungana na ww wanaopigania katiba walio wengi ni wanasiasa na wafuasi wao,Katiba ina mambo Mengi sana inayazungumzia...ila watu kama chadema kwenye itaji lao la katiba mpya wanataka kipengele tu cha TUME HURU YA UCHAGUZI.
 
Tatizo la wanasiasa haswa vyama vya upinzani wanadhani kuwepo kwa katiba mpya kutawawezesha washike dola!!!!!
Mimi nasema fikra hizo ni za kipuuzi!

Mfano angalia nchi JIRANI ya Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya nzuri lakini kila Uchaguzi Raila analia hakubali matokeo na hakubali maamuzi ya mahakama!!!!

Kwa maana hiyo ni wazi kuwa katiba mpya sio "mwarobaini"

Kwa mtizamo wangu, maadili/uadilifu ndio jambo la msingi ambao hauletwi na katiba mpya bali unajengwa kwa kizazi na kizazi.

Uadilifu na maadili mazuri ya viongozi wetu wote walio pita kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa awamu ya sita ni kutokana na uadilifu wa viongozi wetu, wamejengwa na kulelewa kwenye misingi ya maadili na uadilifu.
Hata wa upande wa pili wanaing’ang’ania hii katiba ili waendelee kushika dola !!! Ukweli hutuweka huru wajameni 😂🙏
 
Duh...!. Mkuu Mganguzi , kwanza nikupongeze kwa bandiko hili na kuheshimu uhuru wa maoni na uhuru wa kijieleza, yaani freedom of expression and freedom of speech.

Dunia ilipoumbwa, hakuna aliyejua dunia ni duara, watu wote kwa kutokujua kwao wakajua umbo la dunia ni umbo bapa.

Galileo Galilee alipogundua telescope na kuliona umbo la dunia kupitia kivuli cha kwenye mwezi, alipotangaza kuwa dunia ni duara, Galileo Galilee aliuwawa kwa kosa la kumkufuru Mungu kwa kitendo chake cha kusema dunia ni duara!.

Ukiwa hujaonja embe dodo ukiambiwa tunda tamu kuliko yote ni pera utaamini mpaka utakapoonja embe dodo ndio utagundua kumbe tunda tamu ni embe dodo.

Ukionja zabibu unagundua ni zabibu, ukionja nanasi unagundua ni nanasi, ukionja tende unagundua ni tende, ukionja asali ndipo utagundua asali ndio funga kazi ya utamu!.

Wewe ni mmoja wa Watanzania wasiojua katiba wala Umuhimu wa katiba mpya, hivyo wameridhika sana na hii katiba pera iliyopo, bila kuonjeshwa katiba embe, katiba nanasi, katiba tende na katiba asali, kamwe hauwezi kujua Umuhimu wa katiba mpya.

Hili la Watanzania kutujua katiba, hata Rais Samia amelisema

Hivyo watu kama akina sisi tuliobahatika kajiuwezo ka kusoma sheria na kuijua katiba, tumejitolea kuwaelimisha wengine Umuhimu wa katiba mpya kwanza kwa kuwaelimisha Watanzania wenzetu elimu ya katiba ili waifahamu katiba.

Angalia bandiko hili elimishi kuhusu kuijua katiba ni la lini na limechangiwa na watu wangapi ili kupata picha ya Watanzania wanavyotaka kuijua katiba Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio ila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
Just imagine mtu unajitolea kuelimisha umma kuhusu katiba halafu responses ndio hii!, utaendelea kweli?.

Hivyo watu kama nyinyi mnapojitokeza kusema hamuhitaji katiba mpya, hatuwashangai bali tunawahurumia!.

Laiti ungelijua tungekuwa na katiba bora, Tanzania tungekuwa wapi, ndipo ungeweza kujua tofauti ya utamu wa pera na asali!.

Kama una muda karibu pande hizi
P

Asante kwa ufafanuzi mzuri,Mungu akubariki.
 
Katiba mpya ipi hiyo haifai ?? Usitangulize mkokoteni mbele ya Punda uwe unavuta Punda, utakuwa mpumbavu. Subiri hiyo katiba mpya itakayopendekezwa ndio ukatembee mtaani kuwaambia wananchi haifai waikate kwenye sanduku la kura za maoni.
Ndio tumeanza Sasa tunaratibu Mikutano tutatembea nchi kuwaambia wananchi katiba mpya haifai
 
Tupo wengi sana. Hata kwa wanaotaka wengi wao ni kufuata mkumbo tu lakini hakuna hoja za msingi za kutaka katiba mpya zaidi ya madaraka ya Rais ambayo yanaweza kurekebishwa bila kuandika katiba mpya.
Kuhusu Muundo wa Serikali ya Muungano,Kinga za Viongozi wa Serikali,Ajira,Elimu na mambo mengine.
 
Naunga mkono Hoja kwa asilimia 100 .Watanzania hatuna haja ya Katiba Mpya .Katiba ya Mwaka 1977 ni Msingi Imara wa Taifa letu. Mambo yote ambayo tumeyafanikisha kama Taifa au Watu binafsi yametokana na Katiba hii.

Wanatokea baadhi ya Watanzania wenzetu kwa maslai ambayo hayako wazi , ovu,potofu na hatarishi wanataka Katiba hii ibadishwe.Kumbukeni mkibadirisha Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 huo ndio utakuwa Mwisho wa utambulisho wa Mtanzania.

Acheni kufanya majaribio kwenye eneo lisilohitaji majaribio hata kidogo.

Matatizo mlio nayo au matatizo tuliyonayo kama Nchi kisiasa,kiuchumi,kiteknojia,kibailojia, kiutamaduni,kitibabu etc hayawezi kutatuliwa kwa kubadilisha Katiba.

Mkifanikisha hili mtakuja na hoja ya kubadilisha VITABU VYA DINI ili kuendana na matakwa yenu.

Yangu Maoni ni hayo kwa ajili ya rejea mbeleni.

ARTICLE.
Wewe bila shaka ni Mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom