Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

Hoja nzito kabisa hii
 
Hata wewe inaonekana unahitaji elimu ya kujua kwamba katiba sio chanzo Cha umaskini wetu Bali uvivu
 
Punga kama wewe huna hoja za kupeleka mahakama, endelea kujifariji tu hapa jf na wajinga wenzio
Jamii forum Haina wajinga kama Kuna mjinga hapa jf wewe ni namba moja
 
Asante sana mkuu elimu hii inatakiwa tuitoe wananchi wanapelekwa pelekwa TU
 
Hakuna kinachopiganiwa hapo zaidi ya maslahi ya wanasiasa
Mkuu naungana na ww wanaopigania katiba walio wengi ni wanasiasa na wafuasi wao,Katiba ina mambo Mengi sana inayazungumzia...ila watu kama chadema kwenye itaji lao la katiba mpya wanataka kipengele tu cha TUME HURU YA UCHAGUZI.
 
Hata wa upande wa pili wanaing’ang’ania hii katiba ili waendelee kushika dola !!! Ukweli hutuweka huru wajameni 😂🙏
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri,Mungu akubariki.
 
Katiba mpya ipi hiyo haifai ?? Usitangulize mkokoteni mbele ya Punda uwe unavuta Punda, utakuwa mpumbavu. Subiri hiyo katiba mpya itakayopendekezwa ndio ukatembee mtaani kuwaambia wananchi haifai waikate kwenye sanduku la kura za maoni.
Ndio tumeanza Sasa tunaratibu Mikutano tutatembea nchi kuwaambia wananchi katiba mpya haifai
 
Tupo wengi sana. Hata kwa wanaotaka wengi wao ni kufuata mkumbo tu lakini hakuna hoja za msingi za kutaka katiba mpya zaidi ya madaraka ya Rais ambayo yanaweza kurekebishwa bila kuandika katiba mpya.
Kuhusu Muundo wa Serikali ya Muungano,Kinga za Viongozi wa Serikali,Ajira,Elimu na mambo mengine.
 
Wewe bila shaka ni Mwigulu Nchemba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…