Rais wa Cameroon afanya mabadiliko kwenye Bunge na Wizara ya Ulinzi

Rais wa Cameroon afanya mabadiliko kwenye Bunge na Wizara ya Ulinzi

Fafanua zaidi
Mfano mdogo, cameroon kuna vyama vya upinzani zaidi ya 300 na vyote vinafadhiliwa na biya mwenyewe.
Mfano mwingine magenerali wengi wanapewa migao na fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi.
Chama tawala cha biya kina siti 63/70.
Biya pia ana jeshi lake la makomandoo kutoka huko kijijini kwao ambao lengo lake ni kudhibiti jeshi lisifanye mapinduzi ya aina yoyote. Unakumbuka wakati wa idi amin alivyomuweka yule malyamungu kudhibiti jeshi na kuweka nidhamu na utiifu juu yake.
 
nafasi ya kulirekebisha Ndugu yangu.

Haya ndiyo wanayofanya viongozi wa Africa,I believe pamoja na Tanzania,so they deserve ousting and more!

1st clip:Fedha alizokutwa nazo Waziri wa Fedha wa Ali Bongo wakati akijaribu kutoroka nchini.
2nd clip:Fedha zilizokutwa nyumbani kwa Ali Bongo.

Taarifa kuhusu utajiri wa Queen Mangungo upo nao mitandaoni, kama ni kweli she is not any different!

Hata hivyo kwangu mapinduzi yanayo-tokea Africa is a new dawn.Nadhani tawala zote kandamizi ambazo zimeibia watu wao rasilimali wakae mkao wa kula,I mean zote,without exception,ikiwemo Tanzania.

Haiwezekani Tanzania baada ya miaka sitini na tatu ya Uhuru tukiwa na rasilimali nyingi kiasi hiki,bado watu wetu wengi hawana maji,na hata hao wachache wanaopata maji si safi na salama;watu wanakufa kwa sababu hawana huduma za afya,tena kwa magonjwa yanayoweza kutibika;watoto wengine hawasomi kwa kuwa wazazi wao hawawezi kuwapeleka shule kwa kuwa hawana michango,madaftari na kalamu au uniform; Elimu inayotolewa ni chini ya kiwango,shule hazina mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi;watu wetu hawana nyumba bora za kuishi ;watu wetu wanapata mlo mmoja tu kwa siku na wengine hawapati kabisa,na hata huo mmoja wanaopata hauna virutubishi muhimu nk.nk..

No, lazima kama Watanzania tufike mahali tuseme hapana hii haivumiliki tena inatosha,na tufanye kitu ambacho kitatutoa kwenye uonevu huu
 

Attachments

  • VID-20230831-WA0001.mp4
    13.8 MB
  • VID-20230831-WA0000.mp4
    875 KB
  • IMG-20230828-WA0001.jpg
    IMG-20230828-WA0001.jpg
    55.1 KB · Views: 2
Mfano mdogo, cameroon kuna vyama vya upinzani zaidi ya 300 na vyote vinafadhiliwa na biya mwenyewe.
Mfano mwingine magenerali wengi wanapewa migao na fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi.
Chama tawala cha biya kina siti 63/70.
Biya pia ana jeshi lake la makomandoo kutoka huko kijijini kwao ambao lengo lake ni kudhibiti jeshi lisifanye mapinduzi ya aina yoyote. Unakumbuka wakati wa idi amin alivyomuweka yule malyamungu kudhibiti jeshi na kuweka nidhamu na utiifu juu yake.
Hujui kitu, ukijua mapinduzi huwa yanaanzia wapi usingeongea huu upupu
 
Huku mapinduzi yakizidi kuenea ukanda wa Afrika Magharibi, Rais wa Cameroon bwana Paul Biya mwenye umri mwenye miaka 90 amelifanyia mabadiliko Bunge pia amefanya mabadiliko makubwa katika Wizara ya Ulinzi.

Hivi karibuni ameteua watumishi wapya katika huduma za ndani na nje za Wizara.

Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu 1982. Alikuwa Waziri Mkuu kutoka 1975 hadi 1982.
View attachment 2734227
Rais wa Cameroon bwana Paul Biya mwenye umri mwenye miaka 90[emoji3064]
 
Kuna mtu generali mmoja hv akasema ccm Ni vigumu smaa kuachia dola kwa vile utaratibu wao wa kubadilisha uongozi kila baada miaka 10 Ni nzuri hvyo chama Kama ccm Ni vigumu kuvhokwa kwani kila miaka kumi huja na vichwa vingine
Waweke mizani sawa kwenye uchaguzi, tume huru ya uchaguzi, halafu watajua ccm imechokwa au laaa.
 
Haya ndiyo wanayofanya viongozi wa Africa,I believe pamoja na Tanzania,so they deserve ousting and more!

Taarifa kuhusu utajiri wa Queen Mangungo upo nao upo mitandaoni, kama ni kweli she is not any different!

Hata hivyo kwangu mapinduzi yanayo-tokea Africa is a new dawn.Nadhani tawala zote kandamizi ambazo zimeibia watu wao rasilimali wakae mkao wa kula,I mean zote,without exception,ikiwemo Tanzania.

Haiwezekani Tanzania baada ya miaka sitini na tatu ya Uhuru tukiwa na rasilimali nyingi kiasi hiki,bado watu wetu wengi hawana maji,na hata hao wachache wanaopata maji si safi na salama;watu wanakufa kwa sababu hawana huduma za afya;watoto wengine hawasomi kwa kuwa wazazi wao hawawezi kuwapeleka shule kwa kuwa hawana michango,madaftari na kalamu au uniform; Elimu inayotolewa ni chini ya kiwango,shule hazina mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi;watu wetu hawana nyumba bora za kuishi ;watu wetu wanapata mlo mmoja tu kwa siku na wengine hawapati kabisa nk.nk..

No, lazima kama Watanzania tufike mahali tuseme hapana hii haivumiliki tena inatosha,na tufanye kitu ambacho kitatutoa kwenye uonevu huu
Mshahara wake na mapato ya biashara zake ni kiasi gani?
 
Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 90 amefanya mabadiliko muhimu kwenye Wizara ya Ulinzi kwa kuongeza watu kwa ajili ya shughuli za ndani na nje ya Wizara hiyo. Mabadiliko hayo yanatafsiriwa kuwa kama kitendo cha kujihami kwa Rais huyo kufuatia Mapinduzi ya Kijeshi nchini Gabon wiki hii ambayo yameshuhudia Rais Ali Bongo akiondoshwa Madarakani na Wanajeshi wa Taifa hilo.

Rais Paul Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982 akihudumu kwa kipindi cha miaka 41, pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu toka mwaka 1975 hadi 1982. Biya ni Rais wa Pili kwa ukongwe Madarakani barani Afrika.

Wananchi wa Cameroon wameonekana katika mitandao ya kijamii watoa maoni kwa kuandika "Next is Cameroon".

Marais wa nchi nyingine za Afrika wanaoshikilia madaraka kwa muda mrefu. Ni wafuatao;

1. Equatorial Guinea [emoji1095]: Inatawaliwa na Teodoro obiang Nguema Basogo, kuanzia mwaka 1979, na huku mtoto wake wa kiume anayeitwa Teodoro Nguema Obiang Mangue akishikilia nafasi ya Makamu Urais (Vice president). Nchi inaongozwa na Baba na mtoto.

2. Uganda [emoji1254]: Inatawala na Yoweri Kaguta Museveni, aliyeingia madarakani mwaka 1986 baada ya mapinduzi ya kijeshi. Huku mke wake Janeth Musevi akiwa Waziri wa Elimu, na mtoto wake wa kiume alishika nyadhifa za juu jeshini.

3. jamuhuri ya Congo [emoji1077]: Inatawaliwa na Denis Sassou Nguesso ambaye ametawala Jamuhuri ya Congo tangu mwaka 1979 hadi mwaka 1992. Ambapo mwaka 1992, Denis Sassou Nguesso alishindwa uchaguzi vibaya mno kwa jumla ya asilimia ya kura 17% nchi nzima, baada ya kushindwa uchaguzi, miaka inayofuata vilizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 1997, ambapo Denis Sassou Nguesso alirejea tena kwenye madarakani kwa kutumia nguvu ya Jeshi. Na aliporudi alibadirisha katiba ili kusimika nguvu kubwa kwenye urais wake. Toka 1979 mpaka sasa ndiye rais anayetawala.

4. Eritrea [emoji1096]: Inatawaliwa na Isias Afwerk ambaye ametawala tangu mwaka 1993 baada ya Eritrea kupata uhuru kwa kujimega na kujitenga kutoka kwenye nchi ya Ethiopia, kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa ikiendelea ambapo pia Djibouti nayo ilijitenga, pia na hivi sasa tunaona Tigray nayo ikipambana kujitenga kuwa Nchi.

Tangu Isias Afwerk aingie madarakani kwa kutumia jeshi kujitenga na Ethiopia, hakuna sheria wala katiba inayofuatwa au kutekelezwa. Tangu Eritrea ipate uhuru mwaka 1993 ni yeye tu mwenye mamlaka na nguvu za juu Nchini humo, wala hakuna uchaguzi wa urais.

5. Rwanda [emoji1206]: Ambayo inatawaliwa na Paul Kagame ambaye aliingia madarakani mwaka 1994 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wa Tutsi na Wahutu. Paul Kagame alifanikiwa kupindua jeshi na kuingia madarakani mpaka hivi leo, na hakuna uchaguzi wa urais Nchini Rwanda uliowahi kufanyika.

Na inasemekana ndugu zake na watoto wake wanashika nyadhifa jeshini. Baada ya mapinduzi ya kijeshi, iliundwa serikali ya mpito ambayo Bizimungu ndio alikaimu madaraka ya mpito ya urais hadi miaka ya 2000, ambapo lilitokea shinikizo kubwa la kumtuhumu Bizimungu kuwa mla rusha na mwizi, na zengwe la sintofahamu la hapa na pale kutoka kwenye Muhimili wa mahakama na bunge ambapo taarifa zisizo rasmi inasemekana Kagame ndio alikuwa nyuma ya zengwe, na kupelekea Bizimungu kuamua kujiuzuru. Na mahakama ikaamuru Paul Kagame akaimu urais wa mpito, na mwaka 2003 ukafanyika uchaguzi ambapo amekuwa akishinda kwa zaidi ya asilimia 90 kila mara.

6. Djibouti [emoji1089]: Inatawaliwa na Ismaïl Omar Guelleh na ndiye Rais wa sasa wa Djibouti. Amekuwa madarakani tangu 1999, na kumfanya kuwa miongoni mwa watawala wa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Guelleh alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama Rais mnamo 1999 kama mrithi aliyechaguliwa kutoka kwenye utawala wa kifamilia kwa mkono wa mjomba wake, Hassan Gouled Aptidon, ambaye naye alikuwa Rais na ametawala Djibouti tangu uhuru mnamo 1977.Tangu Ismail aingie madarakani alichaguliwa tena mnamo 2005, 2011 na tena mnamo 2016.


Ukiachilia mbali nchi zinazoongozwa Kifalme barani Afrika, kama Lesotho, Eswatini (Swaziland) na Morocco. Hizo nilizozielezea hapo juu ndio nchi zilizobaki ambazo marais wake bado wanatawala kwa muda mrefu, na wengi hapo wameingia madarakani kwa nguvu za kijeshi au kifamilia.

Na ukitoa Uganda na Eritrea, zilizobaki zote ni makoloni ya Ufaransa na yanaushirkiano wa moja kwa moja kwa Ufaransa. Na mfaransa ndio amekuwa nyuma ya hawa marais kukaa madarakani muda mrefu. Pili Nchi hizi nyingi zina rasilimali nyingi, na Ufaransa ni nchi yenye rasilimali ndogo sana na uchumi wake mkubwa ni kutoka nchi hizi ambazo ni makoloni yake ya kitambo ambayo kila kukicha yanapinduliwa kijeshi.
 
Back
Top Bottom