Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 90 amefanya mabadiliko muhimu kwenye Wizara ya Ulinzi kwa kuongeza watu kwa ajili ya shughuli za ndani na nje ya Wizara hiyo. Mabadiliko hayo yanatafsiriwa kuwa kama kitendo cha kujihami kwa Rais huyo kufuatia Mapinduzi ya Kijeshi nchini Gabon wiki hii ambayo yameshuhudia Rais Ali Bongo akiondoshwa Madarakani na Wanajeshi wa Taifa hilo.
Rais Paul Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982 akihudumu kwa kipindi cha miaka 41, pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu toka mwaka 1975 hadi 1982. Biya ni Rais wa Pili kwa ukongwe Madarakani barani Afrika.
Wananchi wa Cameroon wameonekana katika mitandao ya kijamii watoa maoni kwa kuandika "Next is Cameroon".
Marais wa nchi nyingine za Afrika wanaoshikilia madaraka kwa muda mrefu. Ni wafuatao;
1. Equatorial Guinea [emoji1095]: Inatawaliwa na Teodoro obiang Nguema Basogo, kuanzia mwaka 1979, na huku mtoto wake wa kiume anayeitwa Teodoro Nguema Obiang Mangue akishikilia nafasi ya Makamu Urais (Vice president). Nchi inaongozwa na Baba na mtoto.
2. Uganda [emoji1254]: Inatawala na Yoweri Kaguta Museveni, aliyeingia madarakani mwaka 1986 baada ya mapinduzi ya kijeshi. Huku mke wake Janeth Musevi akiwa Waziri wa Elimu, na mtoto wake wa kiume alishika nyadhifa za juu jeshini.
3. jamuhuri ya Congo [emoji1077]: Inatawaliwa na Denis Sassou Nguesso ambaye ametawala Jamuhuri ya Congo tangu mwaka 1979 hadi mwaka 1992. Ambapo mwaka 1992, Denis Sassou Nguesso alishindwa uchaguzi vibaya mno kwa jumla ya asilimia ya kura 17% nchi nzima, baada ya kushindwa uchaguzi, miaka inayofuata vilizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 1997, ambapo Denis Sassou Nguesso alirejea tena kwenye madarakani kwa kutumia nguvu ya Jeshi. Na aliporudi alibadirisha katiba ili kusimika nguvu kubwa kwenye urais wake. Toka 1979 mpaka sasa ndiye rais anayetawala.
4. Eritrea [emoji1096]: Inatawaliwa na Isias Afwerk ambaye ametawala tangu mwaka 1993 baada ya Eritrea kupata uhuru kwa kujimega na kujitenga kutoka kwenye nchi ya Ethiopia, kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa ikiendelea ambapo pia Djibouti nayo ilijitenga, pia na hivi sasa tunaona Tigray nayo ikipambana kujitenga kuwa Nchi.
Tangu Isias Afwerk aingie madarakani kwa kutumia jeshi kujitenga na Ethiopia, hakuna sheria wala katiba inayofuatwa au kutekelezwa. Tangu Eritrea ipate uhuru mwaka 1993 ni yeye tu mwenye mamlaka na nguvu za juu Nchini humo, wala hakuna uchaguzi wa urais.
5. Rwanda [emoji1206]: Ambayo inatawaliwa na Paul Kagame ambaye aliingia madarakani mwaka 1994 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wa Tutsi na Wahutu. Paul Kagame alifanikiwa kupindua jeshi na kuingia madarakani mpaka hivi leo, na hakuna uchaguzi wa urais Nchini Rwanda uliowahi kufanyika.
Na inasemekana ndugu zake na watoto wake wanashika nyadhifa jeshini. Baada ya mapinduzi ya kijeshi, iliundwa serikali ya mpito ambayo Bizimungu ndio alikaimu madaraka ya mpito ya urais hadi miaka ya 2000, ambapo lilitokea shinikizo kubwa la kumtuhumu Bizimungu kuwa mla rusha na mwizi, na zengwe la sintofahamu la hapa na pale kutoka kwenye Muhimili wa mahakama na bunge ambapo taarifa zisizo rasmi inasemekana Kagame ndio alikuwa nyuma ya zengwe, na kupelekea Bizimungu kuamua kujiuzuru. Na mahakama ikaamuru Paul Kagame akaimu urais wa mpito, na mwaka 2003 ukafanyika uchaguzi ambapo amekuwa akishinda kwa zaidi ya asilimia 90 kila mara.
6. Djibouti [emoji1089]: Inatawaliwa na Ismaïl Omar Guelleh na ndiye Rais wa sasa wa Djibouti. Amekuwa madarakani tangu 1999, na kumfanya kuwa miongoni mwa watawala wa muda mrefu zaidi barani Afrika.
Guelleh alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama Rais mnamo 1999 kama mrithi aliyechaguliwa kutoka kwenye utawala wa kifamilia kwa mkono wa mjomba wake, Hassan Gouled Aptidon, ambaye naye alikuwa Rais na ametawala Djibouti tangu uhuru mnamo 1977.Tangu Ismail aingie madarakani alichaguliwa tena mnamo 2005, 2011 na tena mnamo 2016.
Ukiachilia mbali nchi zinazoongozwa Kifalme barani Afrika, kama Lesotho, Eswatini (Swaziland) na Morocco. Hizo nilizozielezea hapo juu ndio nchi zilizobaki ambazo marais wake bado wanatawala kwa muda mrefu, na wengi hapo wameingia madarakani kwa nguvu za kijeshi au kifamilia.
Na ukitoa Uganda na Eritrea, zilizobaki zote ni makoloni ya Ufaransa na yanaushirkiano wa moja kwa moja kwa Ufaransa. Na mfaransa ndio amekuwa nyuma ya hawa marais kukaa madarakani muda mrefu. Pili Nchi hizi nyingi zina rasilimali nyingi, na Ufaransa ni nchi yenye rasilimali ndogo sana na uchumi wake mkubwa ni kutoka nchi hizi ambazo ni makoloni yake ya kitambo ambayo kila kukicha yanapinduliwa kijeshi.