johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Ndege iliyomleta Rais wa Ethiopia ndio inatua hapa Chato.
Rais Magufuli na viongozi wengine wanashangilia ndege hii ya Ethiopian inapotua.
Rais Zewde anakuwa kiongozi wa tatu wa kimataifa kufika nchini kukutana na Rais Magufuli kwa mazungumzo kwa mwaka huu 2021, aliyefungua pazia ni waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na kufuatiwa na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi.
Updates:
Ndege aliyosafiria Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Sahle-Work Zewde ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Geita mjini Chato leo Jumatatu Januari 25, 2021.
Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Sahle-Work Zewde mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Geita mjini Chato leo Jumatatu Januari 25, 2021kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari wa mkoa wa Geita mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akizungumza na Wanahabari wa Geita baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
Rais Magufuli amempokea mgeni wake na baada ya kushuhudia burudani mbalimbali viongozi hawa wawili wakaelekea Ikulu kwa mazungumzo.
Baada ya mazungumzo ya faragha ya viongozi hao wawili, Rais Magufuli alitoa muhtasari katika yafuatayo:
“Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimesajili miradi 13 kutoka Ethiopia yenye thamani ya Dola milioni 14.57 ambazo zimetoa ajira 677, tunashirikiana kwenye Sekta ya Usafiri wa Anga na Utalii, Marubani wa Tanzania 75 na Wahandisi wa Ndege 20 wamepata masomo Ethiopia.
“Tumezungumza masuala mengi, ikiwa ni pamoja na kunipongeza kwa kuchaguliwa kwangu kuwa rais kwa kipindi cha pili, pia ameshukuru mahusiano yaliyopo kati yetu na bahati nzuri Ethiopia uchumi wake uko juu nafikiri unaongoza Afrika.
Kuhusu wafungwa 1789 wa Ethiopia
“Nimemueleza kwamba tuna wafungwa wapatao 1,789 kutoka Ethiopia ambao waliingia nchini kwa njia isiyo halali, tumezungumza namna ya kuwaruhusu warudi na nimemwambia hatuna masharti yoyote na kwa kuzingatia undugu tunawaruhusu waondoke free (bila ya masharti).
“Rais Sahle amekubali wataenda kujadili ili wafungwa 1,789 wa Ethiopia ambao wamehukumiwa Tanzania warudi kwao wakasaidie kujenga uchumi, kwa vile wana ndege nimemshauri wanaweza kuleta ndege ikawachukua, na hatuna masharti hata waliofungwa leo tutawaachia.
Ushirikiano wa majeshi na ufundishaji wa Kiswahili
“Tanzania na Ethiopia zinajadiliana kuhusu ushirikiano kati ya majeshi na kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa.
Ushirikiano katika kunufaika na bidhaa za mifugo
“Ethiopia ni nchi inayoongoza kwa mifugo sisi ni wa pili, wao wamenufaika na mifugo yao, wanatengeneza mabegi, mikanda n.k, na wana soko kubwa Ulaya, sisi bado haijatupa faida, tumekubaliana wakaribishe wawekezaji na pia sisi tukajifunze kwao.
Kuhusu kiwanja cha Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia
“Nimemwomba Rais Sahle kuhusu kiwanja chetu kule Ethiopia ambacho tulichelewa kujenga, kwani hela tulizopeleka zililiwa na balozi wetu huko (sio huyu anayekaimu), tukamrudisha nyumbani. Sheria za kule ni kwamba kiwanja ukipewa na usikiendeleze unanyang’anywa, tumemwomba rais aturudishie.
Udugu
“Rais Sahle angependa sana kulala hapa, anasema siku nyingine akija atakuja alale, na mimi nimemkaribisha. Tuna Wambulu na Wairaki hapa ambao walitoka Ethiopia, nimemtolea mfano kwamba Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka kumi ni Muiraki na hata wanafanana na Waethiopia,”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amzawadia picha ya Mlima Kilimanjaro pamoja na kinyago cha Kimakonde cha "UJAMAA" mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Sahle-Work Zewde walipowasili Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya siku moja.