Rais wa Ethiopia awasili Chato mkoani Geita. Rais Magufuli aahaidi kuwaachia wahamiaji haramu 1789 kutoka Ethiopia bila masharti

Rais wa Ethiopia awasili Chato mkoani Geita. Rais Magufuli aahaidi kuwaachia wahamiaji haramu 1789 kutoka Ethiopia bila masharti

Ndege iliyomleta Rais wa Ethiopia ndio inatua hapa Chato.

Rais Magufuli na viongozi wengine wanashangilia ndege hii ya Ethiopian inapotua.

Up dates;

Rais Magufuli amempokea mgeni wake na baada ya kushuhudia burudani mbalimbali viongozi hawa wawili wanaondoka kuelekea Ikulu kwa mazungumzo.

Tutawaletea yanayojiri huko.
Chato kuna Ikulu?
 
Nje ya mada maramoja..!

Zile 'vurugu' za kuhamia Dodoma ndo zimeisha mitano ya mwanzo na sasa mitano hii mingine tunahamia Chato?
 
Sina uhakika kama Mwalimu (RIP) ali host Mwaliko wa kidola ndani ya Butiama, Sina uhakika vilevile kama Mzee Mwinyi alifanya dhifa ya kitaifa hapo kwake msasani ama Zanzibar - ama Mzee wetu Mkapa (RIP) naye kule Lupaso ama Lushoto, halikadhalika sina uhakika kama Jakaya alifanya mwaliko kama huu huko Msoga !!

Katiba ya nchi inasemaje kuhusu ugeni kama huu !! Je Chato ina Ikulu tayari ? Sipingi kuwapokea wageni hawa ila utatarabiu wa Katiba na Sheria zetu unasemaje tafadhali
Katiba siyo msahafu tena usiishi kwa kukariri!
 
Kwani chato sio Tanzania???
Sio Mitano tena ni milele kabisa....
Uchumi wa kati....
Nchi hii ni tajiri sana....
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu...

Unaijua vieite wewe?!!
Sisi tunatembelea vieitee!!!
 
Bwashee jaribu kusoma ukomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni miaka mingapi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.

Panapo majaaliwa, 2025 ndiyo ukomo wa Mhe JPM kuhudumu nafasi ya URais wa Nchi.

Nadhani itakuwa zamu yako Bwashee kutuongoza kwa miula 2 ijayo sio ??😂😂
Hahahaaaa....... Bwashee mimi ni mstaafu!
 
Katiba siyo msahafu tena usiishi kwa kukariri!
Najua siyo msahafu, lakini ukiamua kuivunja basi utoe na ufafanuzi ili wananchi wasiwe na hofu - Watanzania wanauliza je Chato kuna IKULU ? wana wajibu wa kujua sababu Rais ni wa kwao !!

Tuwe wakweli kuna mahali hapako sawa!!
 
Nje ya mada maramoja..!

Zile 'vurugu' za kuhamia Dodoma ndo zimeisha mitano ya mwanzo na sasa mitano hii mingine tunahamia Chato?
Labda mkakati wa kuhamia Dodoma ilikuwa ni kupunguza distance ya kwenda Chato .....!!
 
Umestaafu kwa nafasi nyingine sio hii kubwa tunayotaka tukupe.

Natamani 2025 iwe zamu yako ili tupate nafasi ya kukusema vizuri hapa Jukwaani tukiongozwa na Bia yetu Magonjwa Mtambuka BAK na zitto junior 😅😅
Tuache Dr Magufuli akamilishe miradi yote aliyoianzisha hata kama itakuwa 5 tena au 10 tena.

Tumechelewa sana kupata kiongozi shupavu kama huyu.
 
Ndege iliyomleta Rais wa Ethiopia ndio inatua hapa Chato.

Rais Magufuli na viongozi wengine wanashangilia ndege hii ya Ethiopian inapotua...
Ama nchi yote tumekua watu wa oya oya hatujui kutetea misingi na uatawala bora ama kiongozi ametuona ng'ombe na kua hatuhoji uhalali wa shughuli na mambo ya kitaifa kufanyika home kwake.
 
Najua siyo msahafu, lakini ukiamua kuivunja basi utoe na ufafanuzi ili wananchi wasiwe na hofu - Watanzania wanauliza je Chato kuna IKULU ? wana wajibu wa kujua sababu Rais ni wa kwao !!

Tuwe wakweli kuna mahali hapako sawa!!
Katiba haivunjwi bali itafanyiwa marekebisho

Bawacha wataongoza majadiliano kwa kambi ya upinzani kwa sababu ndio chama chenye wabunge wengi!
 
Tuache Dr Magufuli akamilishe miradi yote aliyoianzisha hata kama itakuwa 5 tena au 10 tena.

Tumechelewa sana kupata kiongozi shupavu kama huyu.
Kwahiyo Bwashee unadhani wewe hautaweza kufanya zaidi yake wakati Organs zote unakuwa nazo??

Basi ngoja nafasi yako tumpe Mkuu mwenyewe BAK atunyooshe 2025 😂😂
 
Back
Top Bottom